BBC: Wanajeshi 100 wa Korea Kaskazini wauawa katka vita vya Ukraine

BBC: Wanajeshi 100 wa Korea Kaskazini wauawa katka vita vya Ukraine

View attachment 3180182

Takriban wanajeshi 100 wa Korea Kaskazini wameuawa katika mapigano katika vita vya Ukraine tangu waingie kwenye mapigano upande wa Urusi mapema mwezi huu, mbunge wa Korea Kusini amesema.

Lee Sung-kwon, akizungumza na waandishi wa habari baada ya bunge kupewa taarifa na Idara ya Kitaifa ya Ujasusi ya nchi hiyo, alisema wengine 1,000 wamejeruhiwa.

Alisema waliopoteza maisha ni pamoja na maafisa wa ngazi za juu, na inaweza kuelezewa na wanajeshi hao kutofahamu eneo hilo, na vita vya ndege zisizo na rubani.

Ripoti za kwanza za majeruhi wa Korea Kaskazini zilikuja mapema wiki hii. Iliibuka mwezi Oktoba kwamba Kaskazini ilikuwa imetuma wanajeshi 10,000 kusaidia juhudi za vita vya Urusi.

Siku ya Jumatatu msemaji wa Pentagon ya Marekani alisema Wakorea Kaskazini waliuawa, bila kutaja idadi, na siku moja baadaye afisa wa Marekani ambaye hakutajwa jina alisema kuwa kulikuwa na "mia kadhaa" waliouawa au kujeruhiwa.

Wanajeshi wa Korea Kaskazini, ambao hakuna hata mmoja wao aliye na uzoefu, wanaaminika kuwa walitumia wiki zao za kwanza nchini Urusi katika mafunzo na kisha katika majukumu ya usaidizi.

Majeruhi hao wanadhaniwa kutokea katika eneo la Kursk nchini Urusi, ambako wanajeshi wa Ukraine wanalinda eneo dogo lililotekwa wakati wa uvamizi wa ghafla mwezi Agosti.

Jumamosi iliyopita, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema Urusi imeanza kutumia "idadi kubwa" ya Wakorea Kaskazini katika mashambulio yake huko Kursk.

Hawafikiriwi kuwa wametumwa nchini Ukraine kwenyewe, ambapo wanajeshi wa Urusi wamekuwa wakisonga mbele katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo katika miezi ya hivi karibuni.
NATO wanatafuta namna ya kuingia front kwenye vita ya ukraine
 
We ndo umejiweka msemaji wao,warusi daima wanakanusha mambo ya uongo,juzi TU hapa Trump aliposema warasia Laki 6 wamauwawa vitani mbona msemaji wao kaja mara Moja kujitetea,Sasa wewe kibalakashia unatoka wapi?
Taarifa unatoa wewe halafu unataka mtu mwengine athibitishe hizi akili za wapi? wewe mtoa taarifa ndio unatakiwa kuthibitisha sio Urusi, ndio maana jana Putin kaulizwa kuwa vipi NATO wamesikia onyo lako kuhusu silaha mpya ya ORESHNIK akasema WAULIZE WENYEWE, acha kuleta porojo kama hakuna uthibitisho
 
Sawa basi endelea kuamini wakorea hawafi vitani Ukaraine,akili za madrasa sipotezagi muda nazo
 
Sawa basi endelea kuamini wakorea hawafi vitani Ukaraine,akili za madrasa sipotezagi muda nazo
Kufa vitani ni kawaida wewe, ila ukileta figure bila uthibitisho ni upuuzi huo , wewe endelea kupoteza muda na kiboko ya wachawi
 
Nikifuatilia vyanzo kama;
Spetnaz
Slava russia
Lord bebo
The world is patriotism
Nakutana na habari tofauti kabisa na zinazoripotiwa hapa kwenye hivi vyanzo kila baada ya siku moja zinatolewa video za mamia ya wanajeshi wa ukraine na wapiganaji kutoka mataifa washirika wakiwa wameuwawa na kuna video moja ya mwanajeshi mmoja wa urusi aliua askari 9 wa ukraine kwa kisu hadi soja mmoja wa ukraine akamsifu mwamba "dude you fought well, you are highly skilled please stop torturing me let me die at ease"
 
😂 Ukitusoma makanjanja utashangazwa na mengi.
 
Back
Top Bottom