Tetesi: BBC wapo njiani kuja na mazito kuhusu kitabu cha Kabendera na kifo cha Ben Saanane

Tetesi: BBC wapo njiani kuja na mazito kuhusu kitabu cha Kabendera na kifo cha Ben Saanane

Nawasubiri BBC waweke mambo hadharani kama walivyoweka yale maozo ya TB Joshua hadharani. Kuna ushenzi wa hatari aloufanya Magufuli lazima mambo yote yaanikwe juani!
Kabisa mkuu, jamaa alichukua mpaka pesa ambazo watu tulichanga kwa ajili ya maafa ya kule kagera ili ndugu zetu wale na kulala, yeye akachukua pesa zote.
 
BBC wazee wa propaganda.

Hatuna madhara kimataifa, maza sio threat kwao, hawawezi kumfanyia hivyo. Kwa kifupi mabeberu hawana maslahi na Tz.
Ukisikia mtu anamwita mwingine beberu jua ana matatizo kichwani, hizi lugha nilizisikia mwaka 1971 nikisoma shule ya msingi, hadithi za Kibanga kampiga mkoloni leo kwenye majina ya utandawazi hata Nyerere mwenyewe aliacha kutumia msamiati huu kabla hajafa
 
Ukisikia mtu anamwita mwingine beberu jua ana matatizo kichwani, hizi lugha nilizisikia mwaka 1971 nikisoma shule ya msingi, hadithi za Kibanga kampiga mkoloni leo kwenye majina ya utandawazi hata Nyerere mwenyewe aliacha kutumia msamiati huu kabla hajafa
Nani kakwambia naishi kwa kufata Nyerere alisema nini??
Wale ni mabeberu hutaki ni beberu utake ni beberu.
 
Hawa jamaa BBC wana watu wa kila aina ktk kila nyanja pale wanapohitaji habari fulani kwa kina. Wana military analysts, intelligence n.k
Kwamba hao experts wamekaa wakisubiri kitabu cha Kabendera (mfuata upepo) ndio waingie kazini?

So Lame!
Wakiingia mzigoni wakitoka wanatoka mambo mazito.

Kusema kwamba M16 na CIA ni dhaifu mbele ya TISS?
 
Tujiulize Marekani ina uthibitisho upi hadi kudai Makonda anahusika na mauaji? Wana uthibitisho wa mauaji gani ambayo Mheshimiwa Paul Makonda anahusika?

Its just matter of time, kuna nyakati zinakuja na kila kitu kitakuwa open.
Hebu tupunguzie chumvi zako pls!

Mauaji ama vendetta yake against Gay pips & their societies?’

Uwongo mwepesi.
 
Ukisha kuwa na taifa lenye idara ya usalama dhaifu lazma bbc wapate kile wanacho kitaka.. Kwa Tanzania sahau hilo.. hawato pata chochote kipya tofauti na kile tulicho kwisha kukiskia..
Unajidanganya, wengi ya wafanyakazi wa mashirika ya utangazaji na misaada ni mashushu wa nchi za magharibi usishangae hata ndani ya ikulu wapo
 
Mkuu ni wazi kwamba ukiwa unamiliki silaha, kuua ni swala la kugusa tu kama ni mtu wa jazba za kijinga.

Nashangaa watu wanao sema haiwezekani, ukute mzee wa watu alimuita kwa nia njema tu waongee personal kwamba kijana kwann unaniandama, sasa kijana wa watu badala ya kuuma na kupuliza yeye akawa anapuliza tu, akijua jamaa ataplay old school sijui na sheria.

Ndipo bwana mkubwa akaona hunijui, ngoja nisambaratishe kichwa
You people are simply going Loco!

Mnatengeneza fake scenarios guided by your hate & stupidity!

Well, let’s be entertained hakuna namna.
 
Habari wakuu!?

Kwa wale wanaowafahamu wazungu hasa shirika la BBC, hawa jamaa huwa wakipata taarifa ndogo huwa wanakaaa ofisini kwa wiki kadhaa au hata mwezi ama miezi kufanya uchunguzi kisha baada ya hapo wanaanza kufumua mengi zaidi ambayo yamejificha.

Kule Kenya wao ndio walichimba zaidi kuhusu mauaji ya mchungaji Makenze, kule Nigeria walifumbua mengi zaidi kuhusu shutuma za TB Joshua.

Kwa hili linaloendelea hapa Tanzania kutoka ktk kitabu cha Eric Kabendera, tutarajie taarifa nyingi zaidi zitakazotufanya tubaki midogmo wazi kutoka BBC.

Ninaamini kwa sasa wanachambua page after page na matukio ambayo watayagudia zaidi ni la Ben Saanane na kupigwa risasi kwa Tundu Lissu.

Yamkini kwa sasa wameshaanza uchunguzi wa kitabu hiki na wanaandaa nakala kadhaa kisha waanze kurusha hewani ni nini hasa kilitokea kwa Ben Saanane na kwa Lissu pia.

Mind you. Magharibi ma Ulaya walimpiga stop aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda asikanyage USA kwa kumhusisha na mauaji nchini.

Pia kule Uingereza wakatoa habari kwamba TIGO ilihusika na kutoa taarifa zilizosababisha Lissu kupigwa risasi. Hawa jamaa wakiamua kutuwekea mambo wazi watayaweka wazi kwelikweli, kile tunachokitamani kujua ukweli wake, huenda hawa jamaa wakawa nao tayari.

Mungu ibariki Afrika.
Mungu ibariki Tanzania.
Mbona BBC siku hizi watu wanaidharau sana,Wanaaandika yalieyanayowapendeza wazungu wa Magharibi tu.Na wamedharaulika zaidi namna wanavyoripoti vita ya Ukraine na kule mashariki ya kati. kwa hiyo waje na habari ya Kitabu cha KIbendera au wasije nayo,Tanzania ipo palepale na haiyumbishwi na ujinga.
 
Screenshot_20250105_100653_Edge.jpg
 
Back
Top Bottom