Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 9,548
- 28,817
Baada ya BBC kutembelea viwanda vya magari ya umeme Beijing na Hefei kisha ikatembelea Beijing Auto Show 2026, maonyesho makubwa zaidi ya magari duniani:
"China imepiga hatua kubwa ya kiteknolojia, ubunifu, ufanisi na kasi ya maendeleo inayovutia na kutisha kwa wakati mmoja. Kiasi kwamba hata makampuni ya kigeni yaliyokuwa yakitawala soko la China zamani sasa yanajikuta yakipumulia kwa tabu kuendana na kasi 'ya mnyama' huyu wa viwanda."
—BBC
—BBC
Uwezo wa China hauishii tu kwenye magari yenyewe.
"Kwa sasa kampuni nyingi duniani zinanunua components nyingi na muhimu zaidi ya 315 kutoka China ili kuunda magari ya umeme."
—Ripoti ya Rhodium Group.
—Ripoti ya Rhodium Group.
"Ni nafuu kwa asilimia 30 kutengeneza gari dogo la umeme aina ya SUV nchini China kuliko katika nchi zilizoendelea zaidi, hasa kutokana na gharama za chini za betri na mitandao ya kisasa ya mnyororo wa usambazaji wa bidhaa. (supply chains)
Hilo limewezekana kupitia miaka mingi ya msaada wa serikali. Serikali ya China imewekeza makumi ya mabilioni ya dola katika sekta ya utengenezaji wa magari ya umeme (EV) na betri katika miaka ya hivi karibuni pekee."
—Ripoti ya Rhodium Group
Hilo limewezekana kupitia miaka mingi ya msaada wa serikali. Serikali ya China imewekeza makumi ya mabilioni ya dola katika sekta ya utengenezaji wa magari ya umeme (EV) na betri katika miaka ya hivi karibuni pekee."
—Ripoti ya Rhodium Group
Kampuni nyingi za magari za nje sasa zinategemea China kutengeneza magari yao kwa ajili ya dunia, lakini ndani ya China zimeanza kushindwa vibaya na kampuni za ndani. Sehemu yao ya soko imeshuka sana.
Kampuni za magari za Magharibi sasa zinaanza kutegemea sana teknolojia na ubunifu wa China, mfano:
Kampuni za magari za Magharibi sasa zinaanza kutegemea sana teknolojia na ubunifu wa China, mfano:
- Stellantis imeungana na Dongfeng kutengeneza magari China.
- Volkswagen ikinunua teknolojia ya magari ya umeme kutoka XPeng kwa sababu China imekuwa mbele sana kwenye teknolojia ya EV.
- Toyota, Ford na Nissan sasa zinaongeza utafiti na uzalishaji China ili kujifunza kutoka kwa wataalamu wa huko.
"Ushuru mkubwa (tariffs) hauwezi kuizuia China. Ukifunga soko moja, kampuni za China zitatafuta soko lingine na kuendelea mbele. Kampuni zitakazokubali kushirikiana na China ndizo zitakazonufaika na kukua zaidi. Lakini wale wanaojaribu kuizuia China wanaweza kubaki nyuma huku dunia ikiendelea kusonga mbele."
—James Pearson (Mtaalamu na Mshauri kuhusu masuala ya viwanda na biashara)
—James Pearson (Mtaalamu na Mshauri kuhusu masuala ya viwanda na biashara)
CREDIT:
The world's carmakers are struggling to compete with China
The BBC visited China’s EV factories and found they are dominating the ecosystems shaping the global auto industry.