BBT yaanza kukwama. Tulisema hapa kuwa BBT ni shimo la kuzikia fedha za Kodi zetu

Kwahiyo unashauri tufunge vyuo vya kilimo? Kati ya makosa makubwa yanayoweza kufanywa ni kudharau taaluma na ilmu. Kukifanya kilimo kimazoea kumepitwa na wakati, hizi ni enzi za matumizi ya sayansi kila mahala.
 
BBT ni pesa za wahisani zinazikusudiwa kupigwa tuu na serikali. " A special tailored mutual donor funds " pesa ikiisha na promo itaisha na wanufaika wataishia pa bure. Nimesikia wamepelekea JKT😁
 
Kwahiyo unashauri tufunge vyuo vya kilimo? Kati ya makosa makubwa yanayoweza kufanywa ni kudharau taaluma na ilmu. Kukifanya kilimo kimazoea kumepitwa na wakati, hizi ni enzi za matumizi ya sayansi kila mahala.
Vyuo vya kilimo ni kwa ajili ya kuandaa wataalam wa kilimo,we unafikiri huko vyuoni wanasoma kulima mahindi, mpunga,nyanya miaka yote mitatu!?
 
BBT ni mkombozi wa wanyonge wacha kebehi
Hizi story za kuwa kilimo ni mkombozi huwa sizielewi vizuri, maana wakulima wengi ndio wenye ugumu wa maisha. Fuatilia vizuri utakuta barmaid hapa mjini ana maisha mazuri, na ndio anayetuma hela kwa ndugu zake wanaomiliki zaidi ya hela 5 huko kijjini!

Ukitaka kujua kilimo ni janga katika nchi hii, aende barmaid bank na mkulima mwenye heka 5 wakitaka mkopo uone nani atakopeshwa mapema. Hapo ndio utajua kilimo ni Nini.
 
Sasa waamekwama nini hapo na hayo ni mafunzo?

Tanzania kunakosekana soko la ng'ombe? Unaishi Tanzania hii au nje ya Tanzania?
 
Acha mboyoyo onyesha soko la ng'ombe lilipo.mboyoyo nyingi zakuitetea serikali zimeshapitwa na wakati.
Pugu lipo, vinguguti lipo, saa 24 hapo hukosi mnunuzi wa ng'ombe. Minada ya mifugo imejaa Tanzania nzima.
 
Yaani unaanzisha project bila ya kuwa na uhakika wa soko? wamekosa hata soko la arabuni......bwashee bhana.
 
Viwanda ndiyo jawabu sahihi.

Kutegemea soko la mpaka upewe mashariti ya kukubali ushoga ndiyo wanunue kwa bei nzuri ni ujinga

Kwani sasahivi ng’ombe hai si wanasafirishwa kwenda uarabuni,soko lipo la kutosha.
 
BBT ni Kilimo Cha kwenye Tablet, sawa na zile stori za kilimo cha matikiti za whatsapp
Mimi ni mtaalam wa kilimo cha umwaviliaji kwa zaidi ya miaka 35 sasa. Kati ya hiyo miaka, nimefanya na Waholanzi zaidi ya miaka 15, Waisraeli zaidi ya miaka, nane,.miaka iliyo baki niko binafsi, Bashe alipo kuja na hii hypothesis yake ya BBT nilikuwa mstari wa mbele kuipinga, na hadi sasa naipinga. Ni ndoto za alinacha.
Nilisema kabisa, kilimo sio sawa na kuuza magazeti.
Tuwe na huruma na pesa za umma
 
mkuu tatizo nafikiri ni elimu na zana bora za kilimo...alafu hiyo kichwa yako nafikiri inauwelewa mdogo sana ,mkopo wa benk unafahamu taratibu zake..yani barmeid apeleke makalio benki na mkulima mwenye aridhi ya heka tano kisha anyimwe mkopo ilihali kama barmaid hana mali yoyote ya isiyohamishika hebu changamsha bongo toka hapo ufipa ndugu mbowe anawadanganya sana hamjui tuh
 
Hujawahi kukopa inaonekena, ingekuwa kuwa na ardhi kunakupatia mkopo Kila mkulima angekuwa nao. Hao mabarmaid wanaweka hela bank na bank statement zao zinawabeba, sio hizo ardhi zinazotoa gunia tatu na robo kwa heka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…