Be Forward wamekuwa wajanja na waongo, magari yanaletwa mabovu

Mnataka ku-suggest kwamba hiyo kampuni ni ya hovyo kiasi ambacho hawajui documents muhimu za kumpa mteja wao? Hivi ukinunua gari ni wewe mteja unaomba documents au ni muuzaji anatakiwa akupe?
 
Customer care yao ni mbovu mno.
 
Hii ni hasara sana mkuu. Pole sana
 
Kwani ukinunua gari yard unapungukiwa nini? Kumpa mbongo mwenzio maisha unaon abora upeke kwa weupe.
 
Kwa kweli mtu akianza kulia kuhusu gari roho huniuma maana Nina kapremio old mwaka wa 15 huu hakajanisumbua chochote nguvu ya kutosha safari popote hata mbinguni naenda muhimu nipate barabara.
 
Auction sheet na condition report hapa ndio wengi tunapigwa sana, kuna gari nilitaka kuilipia SBT nikaomba hizi document nikaambiwa unazipata baada ya kulipia nikaona huyu ni mbuzi kwenye gunia tayari. Hawa mawakala tunatakiwa kuwa nao makini eti ukishalipia ndio ujue lina hali gani.
Kwa huu uchumi unaagiza gari mbovu inauma sana bora ukashikishwe na madalali wa magomeni
 
Mmh hicho kirusi mtafute msukuma mmoja muizie bei ya mkokoteni angalau atafunga ng"ombe pale mbele waende sawa.
Hauna gari hapo
 
Naona wengi wameikubali. Coworker ana ndogo yake RVR haijawahi msumbua karibia mwaka sasa


Mimi ninayo mwaka wa pili na haijawahi nisumbua mkuu. Chuma imetulia
Mkuu uliyonayo ni Outlander au RVR?
 
UshaaMbiwa recondition cars au used cars unategemea ukute gari nzima
alafu wauzaji hao utakuta wanawaambia njoo ujipatie gari vrand new from japan,brand new unaipataje yard

Ova
 
Una tumia 10ml kutengeneza gari ya 20+ml /-25ml [emoji41]
 
pole mkuu
najua umeandika kutokana na machungu uliyonayo. nashauri
siku ingine kama unafanya manunuzi makubwa kama hivi hakikisha unapata usaidizi kutoka kwa wahusika wanaofanya izo shughuli itakuepusha na hasara km ivi.

ila kama unaona unaweza kuendelea kununua mwenyewe hakikisha unazijua abc za kufanya manunuzi huko mitandaoni baadhi ya izo abc zimeelezwa hum km kuangalia ripoti za gari unalonunua km kuna kitu hakiko saw huwa hawafichi mfano km A/c mbovu wanakuandikia hawakufichi uchague mwenyewe. sasa tatizo letu sisi waswahili hatusomi na apo ndo wanapotunyooshea.

uzuri wa beforward kwanza ni kampuni kubwa sana nadhani kwa ukanda huu hamna wengine wenye ukubwa km wa ao jamaa. wana stock kubwa za kwao wenyewe wanaziita BF na za watu wa nje wanaoleta kuuza apo yani 3rd party. izo stock zipo nchi mbalimbali. izi kampuni zingine zote ulizotajiwa humu sijui nikyyo, autocom, autorec, sbt n.k ni vikampuni vidogo vidogo vyenye magari machache machache sana kulinganisha na hao jamaa.

kuna jamaa namfaham ananunua sana kupitia beforward na sijawahi kusikia anawalalamikia. na uzuri wa hawa uwa wanaweka izo ripoti za magari yao mtandani unaziona wazi tu.

so usikatishwe tamaa na yaliyokutokea bali uchukue kama mafunzo kwa uko mbeleni iwapo utapendelea kuwa unanunua mwenyewe au la kavipi waone wahusika mahsusi wa izo kazi wakusaidie.
 
Kwahiyo umetumia zaidi ya million 36
 
Kampuni ya uhakika haijalishi umenunua mwenyewe au la watakupa bidhaa nzuri TU kwani wao ndio wanatakiwa wawahakikishie bidhaa Bora wateja wao nje ya hapo hiyo kampuni ni janja janja imebaki kuuzia jina
 
Hii Sasa chai. Alphard 26m kabla ya ushuru? Una mañana ukijumlisha na ushuru unataka kusema ulilipa over 40m?

Tunajua magari Boss!
 
Mkuu tuna mtu Japan next time unakuja hapa unaomba ushauri kabla ya kuagiza hiki kisima cha busara ingawa wahuni wapo humu pia ungeunganishwa kule angeikagua kabla ya kuja usingejuta ka unavyojuta sasa.
 
Autocom wana magari mazuri very clean japo stock yao sio kubwa, binafsi nimeacha kuagiza be forward.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…