Be Forward wamekuwa wajanja na waongo, magari yanaletwa mabovu

sio befoward tu kuna kampuni inaitwa janjapan ukiingia kwenye site yao bei kuweka ni ngumu ni kama wao uwacheki na kusema ofa yako alafu pili picha zao si nzuri na kama kuna tatizo au mapungufu hawa waziweki,pili ile document ya kukuonesha gari spection toka kwao sio kila gari.
ila kama ujawazoea na utaalamu lazima wakupige za uso wa mfungo mpaka pasaka
 
Hilo gari litakuwa na Majini
 
Mitsubishi Outlander SUV 7 seaters unaizungumziaje mkuu?
Hii ni chuma ninayo ya 2008 wala sijutii kuwa nayo comfortability+durability inajitahidi.. six gear simulation huwezi ifananisha na tako la ngedere toleo la mwaka 2008!!

Nilinunua mwaka2022 hadi leo hii haijawahi niletea kwere.. safari ndefu nakwenda nayo mara nyingi karibu kwenye Mitsubishi outlander Mr Kolo [emoji1787] (joke)
 
Hii ni chuma aisee,ni SUV ya bei ya chini kuliko SUV zote..
 
Basi baridi mtopolo,ngoja niendelee kuweka hesabu vizuri.
 
Basi baridi mtopolo,ngoja niendelee kuweka hesabu vizuri.
Fanya hivyo bwana ngada.. chuma iko vizuri cha muhimu cheki site tofauti tofauti ulinganishe bei. Mimi niliagiza kupitia autocom Japan. Shida ya hawa wanastock ndogo sana ya hizi gari, uzuri wao bei yao iko poa na msimu huu vile uchumi wa Japan umeyumba wanauza bei nafuu kiasi
 
Pole mno mtoa hoja kwa yaliyokufika,next time mkuu usihangaike kutafuta gari,panda Taqwa mpaka kwa Madiba,unaitafuta gari yako safi,unaitengeneza na una drive mwenyewe hadi Dar more than 3500km kutegemea umeinunulia wapi kule SA,kama ni kimeo haifiki huku,haya magari ya kuletwa na meli ni shida
 
naomba kufahamu hizo kampuni za Japan zenye ofisi Dar
 
Asante kwa ushauri mkuu, nitaufanyia kazi.
 
Gari za singapore ni kama kubeti. Nina washkj kadhaa wanalia gari za huko.

Sema zinatamanisha sana aisee, nna mwana ana rav 4 ya mwaka 2006 aisee ina body kit kali, mlango wa nyuma kama wa vanguard, ina sunroof na speed 260 (kwa shape nje ukiichek utadata). Halafu pia ni diesel na ni manual.

Ila since kaagiza limefika linamsumbua sana aise.

Ila kwa specs kama hizo ni ngumu kupata gari za japan

So watu wanakimbilia singapore ndo wanaliwa kichwa
 
Ni kama bahati hivi kupitia huu uzi. Ningepata hypertension mwaka huu dadeki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…