Be Forward wamekuwa wajanja na waongo, magari yanaletwa mabovu

Ilikuwa Singapore Mkuu ila kupitia ofisi yao ya Japan na Tanzania.
Mama yanguuuuu!!!!!
Toka lini Singapore wakawa na magari yenye uhakika? Sometimes uwe unauliza Kwanza kabla ya kuagiza.
Singapore wanatembea na mikweche Tu na ukitaka kulia kilio cha mbwa Koko agiza gari Toka Singapore.

Pole sana
 


Don’t buy used car from Be Forward..!! Gari zao zimechoka sana sana, wanaziosha na kuzipiga polish na little maintenance alafu wanakwambia iko vizuri sana, ujue Be Forward ni ya Mkinga mtanzania yuko Japan, kusema ukweli, magari mengi mno ya Be Forward ni mabovu sana na customer care yao mbovu sana..

I always buy cars from Japan kwa kufuata mwenyewe huko Japan au kupitia mitandao kama SBT Tz au TCV etc..!!
 
Ni kama bahati hivi kupitia huu uzi. Ningepata hypertension mwaka huu dadeki

Nashukuru mkuu, nitatfuta SBT na TCV nione option zake. Je hao wana ofisi hapa TZ?? Maana Be forward wapo Kariakoo na Posta na baadhi ya mikoa, ila huduma zao ni mbaya sana. Inasikitisha
 

Pole sana mkuu. Inasikitisha sana hii.
 
Unacho sema kinafanana na ukweli, mwenyewe nimekuwa mhanga wa hiyo mambo ya hao jamaa.Ushauri wajirekebisha kabla ya kuchelewa,muda na gharama ya ujenzi wa kampuni ni zaidi ya manufaa ya wasio waaminifu ndani ya kampuni 🥴
 
Magari mengi kutoka Singapore ni mabovu wanatabia ya kupiga rangi iliyaonekane mapya.

Kama bado unaipenda hiyo gari nakushauri badilisha engine, kama ni model ya 2014 engine yake ni 2AZ-FE ambayo inatumika kwenye baadhi ya Harrier , Kluger, Rav4 etc.

Sina uhakika sana ila bei inaweza kucheza kwenye 3m to 6m inategemea na hali ya engine bongo zipo nyingi tu.

Ukipata na fundi mzuri gari inaweza ikakaa vizuri....
 
Umesema kweli....mdogo wangu aliagiza forester kutoka Singapore. Gari ilisumbua sana bahati nzuri alipata mteja akauza...

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Pole sana mkuu!!

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
jina lenyewe tu JANJA JAPAN
 
umemaliza kila kitu. nashangaa sana sana wanaoagiza gari toka nje wakati yard za magari kibao mchawi fundi wa uhakika kuikagua na kumaliza mchezo. wacha yawakute.
 
Ndio hivyo na gari ipo juu ya mawe, inaniumiza sana. Mbaya zaidi Be forward hawakutaka kunisaidia kwa lolote. Imenikatisha sana tamaa ya kutumia Be forward, na sifahamu sana mitandao mingine ambayo ni genuine ya kuagiza magari

Mitandao nina experience nayo
1. TRUST (japanesevehicles.com), the best tho wana gari chache
2. Autocom japan
Mingine ambayo nimesikia watu wanakubali
3. Enhance auto

Bahati mbaya beforward nimeshasikia na kuona malalamiko kadhaa, yani huko ni akili kumkichwa.
 
Nashukuru sana mkuu ngoja nifuatilie hili
 
Dah! Pole sana Mkuu. Kwa Alphard hiyo hela ilipaswa upate gari isiyo na shida kwa kiwango hicho. Hao watu wamekuonea sana.

Ya kwangu iliwahi kupata shida kama hiyo, na ikawa inakunywa mafuta balaa, ila Kuna dogo mmoja mtundu aliiokoa ikatulia kabisa.

Sijawasiliana naye muda mrefu, maana niko safari, ila kesho nikipata namba zake nitakutumia. Yeye yuko Dar. Anaweza kukusaidia.

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…