Be Forward wamekuwa wajanja na waongo, magari yanaletwa mabovu

wabongo kwenye swala la ufuatiliaji na kusoma ni ziro huenda mleta mada kaona alfad kitonga kaishobokea bila kuangalia matatizo ya gari na kama kitu hujua wafuate wajuzi wa mambo utapata muongozo bora sana. ungeenda be foward ofisi zao zipo na wanakupa uahirikiano safi tu....

wadau tupunguze kununua gari za bei nafuu na zilizo kimbia kilomita nyingi
 
Huu ni ujinga wa kiwango cha lami! Unawezaje kuuza gari wakati huwezi kuensure wateja wako wanapata nini? Mimi hayo mengine mimi sijui najua ni Be forward kama wao wanadeal na matapeli huo ni uzembe wao. Hii issue nitaenda nahyo mbali
 
Tuambie ulifanyaje kuepuka hizo risks zilizotajwa humu maana ni wewe tu umekuwa positive na Singida
Kampuni niliyotumia ilikuwa inaitwa Car junction, na kwa kipindi hicho sikufanya lo lote la ziada, niliona gari kwenye mtandao nikanegotiate bei halafu nikatuma pesa.

Lakini kila miaka ikisonga matapeli huwa wanazidi kila nchi kwa hivyo sishangai kama mambo kwa sasa yamebadilika
 
Kuagiza ni Bora zaidi SEMA kama hujui uliza maana Kuna website ukiingiza you chasis numba unapata full history ya gari hasa kwa zilizopo Japan
Gari imesajiliwa lini
Imeshamilikiwa na watu wangapi
Accident history
Km ilizoingia nazo kwenye auction
Grade iliyopewa
Service history
Aina ya matumizi iliyokuwa inafanya(town trip or high way)
Hiyo gari ninauhakika hiyo engine huwenda ilibadilishwa maana engine za 2az za chino ya 2005 zilikuwa na shida ya nati kati ya Brock na cylinder head kufunga Kwa mizunguko michache hivyo kuleta tatizo la kuachia kutokana na compression ya engine hata ukaze vipi
Hiyo gari imeharibiwa na mafundi uchwara gear box haikuwa na shida
Hapo ilibidi kupeleka block engineering lakini sio reliable au ununue block ila hakikisha imetengenezwa zaidi ya 2005/6
Pia badili oxygen air sensor pia inachangia gari kukosa nguvu
 
Ilikuwa Singapore Mkuu ila kupitia ofisi yao ya Japan na Tanzania.
Ungekuwa umepekua vizuri humu ungepata kujua kuwa kwa magari ya kutoka Singapore, huwa hakuna mkaguzi.

Yale magari huwa yanakuja hivyo hivyo. Na ishasemwa humu gari za Singapore body huwa zuri. Wahuni sana wale. Ila injini na gearbox huwa shida.

Kingine ni kwamba kwa zile gari za Singapore, Be Forward huwa ni kama wakala tu ambaye watu binafsi wanauza kupitia site yake. Yeye anavuta commission.
 
Mnanipa tumbo joto ndo kwanza juzi nimetoka kulipia
Ila ni ya japan
Sikuomba hizo karatasi ila ndo nimemuokba sasa hivi
Nilinunua kupitia watu wao wa bongo
Ofis zile ocean road
 
Hahaaa.....hao jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…