Beatrice Mdogo wa Martha Mwaipaja aanika mabaya ya dada yake kwamba ana fedha nyingi lakini hamsaidii mama yake

Beatrice Mdogo wa Martha Mwaipaja aanika mabaya ya dada yake kwamba ana fedha nyingi lakini hamsaidii mama yake

Michango mingi humu siyo ya kilichoongelewa na mdogo mtu bali ni maisha yao wao ya kila siku ndiyo wanayoitumbukiza kwenye wanachoita kuchangia.
Mimi pia nashangaa! Nimejiuliza ina maana wote tumeangalia video hizi hizi ama kuna nyingine?

Kinachosemwa na huyo dada ni tofauti kabisa na yanayojadiliwa hapa!

1) Walipata upako wakiwa wadogo kutoka kwa mwanamke wasiemjua.

2) Waliaminishwa Mrema ndio Nabii Eliya.

3)Waliingizwa katika Ibada ambayo walikuja kutambua baadae (hivi karibuni) kwamba ni tofauti kabisa na Mungu waliyedhani wao wanamuabudu.

4)Mama yao amepatwa na matatizo mpaka ya Afya ya akili kwa miaka yote hiyo tangu walipoingia maagano na huyo Mwanamke (stranger) aliyewapa “upako” mabinti zake.

5)Walikutana na huyo Mwanamke baada ya kufukuzwa katika makazi yao ya family na ndugu wa baba yao.

Sasa, ambacho mnajadili hapa kati ya hizo keys ni kipi?!

Beatrice kajaribu kufungua Pandora’s box….
 
Wanataka uwape pesa watumie tu, halafu wakipata zao wanapiga kimya. Siku hizi ni mwendo wa kuchinjia baharini tu qumanyoko
 
Wachungaji sio Waganga wa Kienyeji.....! Wala Mungu hafanyi kazi Kwa namna ya Kibinadamu...!

Yesu alipokua akiponya Watu... aliwaambia nenda ila USITENDE DHAMBI TENA...!

Sijui kama unaelewa maana ya maneno hayo, na Biblia inasema Mapepo yanapomtoka Mtu, huenda kutangatanga na yakikosa pa Kukaa, hujaribu kurudi kwa Mtu yule yule, yakikuta Mtu yupo Msafi hayawezi kuingia Tena, ila yakikuta Mtu Yuko mchafu, yanaiingia yakiwa na Nguvu mara 7.

Kanuni za Mungu zipo wazi Ndugu, Sasa unakuta Mtu ana Mapepo kaombewa Mapepo yameondoka, anarudi kwake, kumbe anaishi na Mwanaume hajafunga nae Ndoa, ama anaishi na Mwanamke hajafunga nae Ndoa, means anaendelea kuzini, ama hajaacha njia zake Mbaya ambazo zilipelekea tatizo lake... Mapepo hayataondoka...

Mafuta ya Upako hayatakusaidia, Keki ya Upako haitakusaidia.
Kitu pekee kitachokusaidia ni kuamua kuishi Maisha safi ya kumpendeza Mungu ama Kwa Lugha nyingine Maisha Matakatifu...!

Tena ukiamua kuishi Maisha Matakatifu Huna haja kupoteza muda kuombewa, hayo Mapepo yataondoka yenyewe haraka Sana (Mimi ni Shahidi)

Tatizo letu Binadamu tunataka Mungu atufungue na akishafanya hivyo tunataka kuendelea na Maisha yetu ya zamani, Starehe, Ngono, Na Dhambi zingine Mbaya...!

Always huwashauri Watu, kama Kuna Watu wanatakiwa kuamua kumgeukia Mungu Moja Kwa Moja ni Watu wenye Mapepo na Majini Mahaba....! Na ipo sababu Kwa Nini baadhi ya Watu husumbuliwa na hizo Spirit, na siku wakijua Sababu.... WANGEACHANA NA UCHAFU WA HII DUNIA NA KUMTEGEMEA MUNGU.
Nani alikuambia kuzini maana yake ni kutokufunga ndoa, tatizo mnaleta tafsiri zenu za vichochoroni. Ndoa zimeanza kufungwa lini na hiyo dhambi ikaanza lini
 
Kumlea Mama yako aliyekuzaa unachokaje ?

Je mama yake anatumia pesa kiasi na matumizi kiasi gani hadi afike hatua ya kutia huruma na kulia lia

Yeye betreace pesa zote alizonazo anashindwa kumuhudumia mama yake na yeye kujihudumia?

YouTube yake pekee inamuingizia pesa kiasi gani?

Labda anabidi akae akombewe na mchungaji ili atolewe ROHO ya kulalamika
Tunza wazazi wako
 
Pesa walimpa mtaji au walimkopesha? Waafrica sisi hamnazo kweli unaenda kwenye media kulilia hela za mtu mwingine
Yuko sahihi maana anamkumbusha kile Mkristo anachopaswa kukifanya. Kuna andiko linasema Mkristo asiyewapenda wa kwao ni mtu mbaya sana (pengine mpagani ana nafuu).
 
Back
Top Bottom