Kwenye hili la mabehewa naona wengi wanachanganya mambo, yawezekana kwa kutojua, au wanajua lkn wanapotosha makusudi. Wengi wanatumia picha ya set ya EMU train kubeza behewa zilizoletwa bila kujua kwamba hivyo ni vitu viwili tofauti
Ikumbukwe kwamba TRC walitutangazia wameagiza:
1. Vichwa vya treni na behewa
2. Set kadhaa za EMU train
Hivi ni vitu viwili tofauti, hiyo namba moja ipo kwenye muundo wa treni za kawaida(ordinary) ambapo kichwa cha train ( Locomotive) ndicho self propelled unit na behewa ni non propelled unit, kichwa kinafunga mabehewa na kuyavuta, hizi kikawaida hutumika kwa safari ndefu
Namba mbili ambayo ndiyo picha inayotumiwa na wengi kukejeri ni set ya EMU trains ambazo july 2021 TRC waliingia mkataba na kampuni ya Hyundai Rotem ya korea kusini, hizi EMU ni tofauti na hizo hapo namba moja, kwenye EMU kichwa na mabewa vyote ni self propelled unit, maana yake ni kwamba kichwa na behewa vyote vina motor za kuviendesha, treni hizi ni za mwendo kasi na zinatumika kwa safari za masafa mafupi. Kifupi ni kwamba mnakejeri kwa kutumia picha za vitu viwili tofauti.
Tuwe wavumilivu, mambo mazuri yanakuja, hata ikiwa kwa kuchelewa