Behewa za SGR zaanza kuwasili nchini Tanzania

Behewa za SGR zaanza kuwasili nchini Tanzania

Kila uchafu wenu Kwa MAGUFULI acheni upumbavu mbwa nyie
kama ulimpenda sana ungekufa naye tu mzee, naona hutaki hata kukosoa wakati hata yeye mwenyewe alisema sio malaika. hakuwa malaika, kuna mazuri alifanya mengi, na mapungufu pia. usimwabudu sana kama alikuwa malaika. sote tulimpenda though tuliona mapungufu kadhaa ambayo lazima yasemwe ili yasijirudie kwa viongozi waliopo.
 
Yaani hata mimi nimewaza hivyo
Je tungeagiza chassis tu na body tukaungaunga kwetu tungeshindwa?

Mbona meli tunatengeneza
Hapo tutakuwa tunapigwa kwa kila kitu
Naaona hata shuka na mito inatoka China
sio meli tu, kuna mabasi mazuri kabisa yanasafiri kwenda mikoani, yana bodi nzuri tu kama hayohayo mabehewa, na mengine yanaweza kuzidi.
 
Hayo mabehewa sio ya SGR ni ya MGR(reli ya zamani) na kwa mtazamo sio ya umeme. Ya umeme yanakuwa na mkonga juu kwa ajiki ya contact ya umeme. SGR yetu ni ya umeme
 
Kaonjesha wa moo kafungashiwa wa mee
Baada ya kugugo tangu asubuhi nimeyakuta mabehewa ambayo mwaka 1968 niliyaona kweye jarida la burudani la Spear na Zoro crime busters wakiwa ndani ya treni wakipambana, mabehewa hayo hayana tofauti na haya.
 
Hayo mabehewa sio ya SGR ni ya MGR(reli ya zamani) na kwa mtazamo sio ya umeme. Ya umeme yanakuwa na mkonga juu kwa ajiki ya contact ya umeme. SGR yetu ni ya umeme
Kwahiyo ya mitumba na kunguni zake ni sawa tu! Bipi bei ni ya mpya au ya mitumba?
 
Hapa Godfather wako Meko ndiyo alicheza uhuni alitoa tenda kwa kampuni ya Kikorea na wahuni wenzake wakala 10%

View attachment 2425073

Meko alitoa tenda kwa kampuni ya Kikorea hii Hapa ndiyo imetuletea haya Mabati. Unayoyaona zilitakiwa kuja 36 naona wametuletea 14 tu.


Baada ya serikali ya Samia kutokuvutiwa na hizi chuma Chakavu ikatangaza tenda uuindaji wa mabehewa 1430 ambayo kampuni ya China wanaitwa CRRC ndiyo washindi wa hii tenda. yView attachment 2425081

Mabehewa yake yataanza kuingia kuanzia September 2023.
Eti Kishindo kingine[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119]
Rais akisoma comments hizi kwenye Uzi anaweza zimia.

Watz hawana shukurani[emoji1787][emoji1787]
 
Nimejikutà naaanza kuuchukia huuu mradi hata kabla haujaanza. Heri Muasisi wake JPM angekuwa hai tusingeona huu utumbo
 
Nimejikutà naaanza kuuchukia huuu mradi hata kabla haujaanza. Heri Muasisi wake JPM angekuwa hai tusingeona huu utumbo
Kiukweli hata mimi nimejikuta nauona huu mradi nimzigo ambao hauna faida yaani maana yake tu tunapoteza hela tu angalau wangeshusha bei ya mafuta tu
 
Behewa 14 za SGR zimeanza kuwasili nchini Tanzania kutoka nchini Korea View attachment 2424514
Kwa jinsi nilivyo ziona ndani, madirisha yako upande mmoja tuu!, upande wa pili, hayana madirisha!, hii maana yake ni kama yalikuwa ni ya zile underground fulani!.
.

Kwenye mambo ya SGR, Watanzania tunapaswa kuambiwa ukweli wa kila kitu!, serikali yetu lazima iwe very transparent see through kwenye kila kitu including mikataba na financial maters kufuatia kuwahi kupigwa huko nyuma kwenye rada, kwenye ndege, kwenye meli na sasa kwenye reli
Maswali haya yajibiwe kikamilifu
Wanabodi,
1. Taarifa ya TRC inasema vichwa vipya na mabehewa mapya, lakini ukweli ni kuwa ni vichwa mitumba na mabehewa mitumba kama ya mwaka '1947'!.

2. Ukiyaangalia kwa ndani, haya mabehewa ni kama yana madirisha only one sided!, hiki ni kuashiria originally haya ni mabehewa ya underground trains na sio ya terestrial train!. Sisi SGR yetu ni terestrial, moja ya faida kubwa kusafiri na treni ni pamoja na kuenjoy kitu kinachoitwa scenery enjoymement, madirisha makubwa both sides abiria kuona nje, hizi behewa za madirisha ya upande mmoja, hebu mfikirie abiria wa Kigoma, seat ya upande usio na dirisha!, kuna tofauti gani na chumba cha jela?.

3. Mkataba ni wa ukarabati na kutiwa nakshi nakshi kwa vichwa na mabehewa mitumba!, na sio kuundwa kwa vichwa na mabehewa mapya!, kwanini Watanzania hatuelezwi ukweli?.
Hakuna ubaya nchi kununua vichwa mitumba na mabehewa mitumba, kitu muhimu ni Watanzania tuelezwe ukweli!.

4. Je, hivyo vichwa viliundwa lini, wapi?, jee originally vimetumika wapi na kwa muda gani kabla sisi hatujauziwa?

5. Mitumba hiyo imenunuliwa kwa bei gani, ikakarabatiwa kwa bei gani, na kusafirishwa kwa gharama gani?

6. Tufanyiwe comparative analysis, kama tungenunua vichwa vipya na mabehewa mapya, tungetumia gharama kiasi gani, compared na kununua vichwa mitumba na mabehewa mitumba, ili tujue tumeokoa fedha kiasi gani kwa kununua mitumba hiyo?

7. Japo gharama za kununua vitu vipya ni juu ila maintance cost ni ndogo, unaweza kununua mitumba kwa bei poa kumbe ni mitumba choka mbaya, hivyo maintenance cost ikawa juu.

8. Sii wengi wanajua kazi ya CAG sio kutoa tuu zile ripoti za hesabu za serikali, CAG ni Mdhibiti na Mkaguzi, ufhibiti unafanywa kabla ya manunuzi, je, kulifanyika tathmini yoyote rail worthness report ya vichwa na mabehewa hayo mitumba kabla hayajanunuliwa?. Then CAG atufanyie value for money audit, msikute mitumba hiyo tumepewa bure, huku watu wakipiga kubwa tunauziwa kwa bei ya mapya!.

9. Ukiingia mkataba wa manunuzi, kwa matengenezo, mzigo ukanunuliwa, delivery ndio ikachelewa, huwezi kuvunja mkataba huo ukabaki salama, hivyo kesi ikifunguliwa, Tanzania tunashindwa hata kabla kesi haijaanza!.

10. Tulivunja mkataba wa Dowans, tulishitakiwa, tukashindwa, tukadaiwa tukasema hatulipi!, watu wakajiapisha "over my dead body", hatulipi!.
ukweli ni kuwa tumelipa kwa siri, Watanzania hatukuambiwa!.

11. Tulipo vunja mkataba wa Dowans, Zitto akashauri tuitaifishe mitambo ile, Wabunge wetu wakagoma kuwa Tanzania hatununui mitambo chakavu, mitambo mitumba!

12 Mitambo ile ikanunuliwa na Simbion, tukaingia nao mkataba ule ule wa Dowans, watu wale wale walio ikataa dowams, ndio hao hao danced to the tune na Hilary Clinton kuzindua Simbion kwa mkataba ule ule tuliovunja!, kwa gharama zile zile!, na capacity charge ile ile!, na tukawalipa!.

13. JPM alipoingia tukavunja mkataba wa Simbion, tukashitakiwa, tukashindwa, JPM akagoma kulipa!, ila baada tuu ya JPM kuitwa kule alipoitwa huku nyuma, sisi sio tuu tumelipa!, bali pia tumeinunua ile mitambo ya Simbion kwa bei ya ajabu!, sasa mitambo ile tuliosema ni chakavu, mtumba, na serikali yetu hatununui, mivitu chakavu, sasa ndio tumeinunua!, sasa mitambo ile ya Simbion ni mitambo yetu, ni mali yetu! na malipo yote yaliisha fanyika chap chap fasta fasta!, bila bajeti yake kuombwa popote!, bila Bunge letu kuijadili, bila CAG kuidhinisha malipo hayo!, na haya yote yamefanyika bila iWatanzania kuambiwa!.

14. NB. Unapohoji vitu kama hivi, huchelewi kunyooshewa vidole vya kukosa uzalendo au kutokuwa na nia njema!, no!, wala sijasema kilichofanyika ni wrong!, no!, ninachosema hapa ni sisi
Watanzania wa sasa ni waelewa, tuwe tuu tunaambiwa ukweli,

15. Kwa vile mambo kama haya kwenye manunuzi makubwa yaliwahi kutokea kule nyuma kwenye ununuzi wa Rada mtumba toka BAE, watu wakaweka cha juu kikubwa tuu, tukalipa fasta!, Mama Mzalendo wa kizungu, Linda Chalkel akabaini, akatupigania tukarudishiwa chenji ya Rada!.

16. Ununuzi wa ndege ya rais Gulf Steeam bei ikapaishwa zaidibya mara tatu!, John Cheyo akaonyesha bei ya kiwandaji watu wakatia pamba masikioni tukalipa fasta!.

17. Kuna vifaa vya kijeshi chakavu tumeuziwa hapa!, tangu vimenunuliwa havijawahi kutumika mpaka leo!. Hivi naomba nisivizungumzie wala msiniulizie!, maana hata sisi waandishi wa habari haturuhusiwi kuzungumzia mambo ya jeshi na usalama wa taifa, ila fedha zilizotumika sio fedha za jeshi au za usalama wa taifa, ni fedha za Watanzania, kuzungumzia vifaa vya jeshi, tuliuziwa nini mitumba ni vifaa vya nini na viko wapi, hii ni no!, hatuzungumzi, lakini tulilipia fedha kiasi gani, ni haki ya Watanzania kujua!.

18. Tukanunua Boti mtumba ya MV Bagamoyo, ikafanya safari moja tuu mahali pa 30 min, ilitumia masaa 3!, Hii pia sasa ni kufaa cha kijeshi!, isizungumzwe!, ila fedha zake ni fedha za Watanzania!.

19. Hivyo kweli hivi vichwa na mabehewa haya, ni bora tukaelezana ukweli tangia mwanzo!.

20. Namalizia kwa msisitizo, hakuna ubaya kutumia vitu used!, tena vingine ni vizuri, imara, bora, madhubuti kuliko hata vipya!, na Watanzania walio wengi, kutokana na low purchasing power due to umasikini uliotopea, wengi wetu affordability yetu ni mitumba kuanzia magar
i, nguo hadi mitambo, hivyo tumezoea, tunachohitaji ni kuambiwa ukweli tuu!,
tutaelewa tuu kuliko...

Wasalaam.
Paskali.
Maswali haya yanahitaji majibu ya kina na sio blah blah!.
Kama mtu kuuliza maswali kama haya, kutapelekea kuhojiwa uzalendo wake, mimi naomba kutumia kinga ya kihabari na kanuni ya kwanza ya mwandishi wa habari no seek the truth, and write nothing but the truth!, kuna kitu ninadhamiria sio tuu kuandika bali kukitengenezea a video documentary ya safari ya SGR ya Tanzania, tulipotoka, tulipo na tunapokwenda, ili huko mbele, likija kujitokeza liji white elephant fulani hivi ambalo sijui kama ni mimi tuu naliona, angalau dhamira yangu isinisute, niliona kabla, nikasema kabla, nikaandaa documentary kabla, nikaonyesha kabla, ili angalau jamii ya Watanzania wajue kuna watu waliona kabla na walisema kabla!.

Na labda kuwasaidia Watanzania wenzangu wasio jua, kwenye ile kashfa ya rada, BAE walikiri kutoa mlungula wa kickbacks, lakini sheria yao inawaruhusu non disclosure ya waliowapa mlungula, ilo usipoteze wateja wapya wapenda mlungula, kibiashara mlungula wa 10% ni halali!, ila ikijulikana kuwa umetoa mlungula, unapaswa ama uwataje uliowapa mlungungula, wakamuliwe wautapike huo mlingula, ama uwahifadhi usiwataje, na badala yake utozwe faini kwa uliowapa mlungula, na kuurejesha ule mlungula, na hicho ndicho kilichofanywa na BAE, kuwahifadhi waliowapa mlungula, na badala yake ikakubali kulipa faini na ndipo tukarejeshewa ile chenji ya rada.

Hii maana yake, kuna viongozi wetu walikula mlungula BAE akawakingia kifua kuwahifadhi kwa kulipia faini na ule mlungula ukarudishwa nchini kama chenji ya rada, endapo BAE wasinge wakingia kifua kuwahifadhi na kuwalinda, amini usiamini, hayo majina ya waliopokea mlungula na kuzihifadhi fedha zao kule Credit Suisse, yangetoka, Watanzania msinge amini macho na masikio yenu!.

Kashfa hii iliobuka kwasababu tuu kulitokea lijinga limoja, mgao wake yeye ukauhifadhi visiwa fulani ambavyo viko chini ya milki ya Uingereza, ndipo Muingereza akabaini, lakini kama wote wange bank Swiss banks, kule fedha zao ni very secure, hata bank manager, hajui majina ya customers na clients ni secret codes tuu zinatembea, hivyo wala kashfa ya rada isinge ibuka!.

Hivyo watu tunaoulizia kuhusu haya mabenewa, naomba mtuelewe ni wazalendo wa kweli wa nchi hii!.

Paskali
 
Kaka Pascal Mayalla umeeleza vizuri,, watuambie ukweli tu,, watanganyika wa mwaka 2010 siyo kama wa leo wa mwaka 2022 wanawachora tu,, siku wakiamua mtakimbia hii nchi viongozi wangu wa CCM na watafukua mpaka makaburi yenu..
 
Back
Top Bottom