Bei mpya za mafuta ni janga, Serikali punguzeni kodi za mafuta Wananchi wapumue

Nodus

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2011
Posts
398
Reaction score
1,105
Dar es salaam sasa mafuta ni 3820 kwa lita na mikoa mingine imefika mpaka 4060 kwa lita ya Petroli.

Tunakubali kuwa vita zimechangia mfumuko huu wa bei lakini serkali ina kodi na tozo nyingi mno kwenye mafuta, kwa nini iangushe mzigo wote kwa mlaji huku yenyewe ikiendelea kupata makusanyo.

Na hatutaki mapunguzo ya kisiasa ya asilimia 2, Bunge lilete emergency resolution ya kusamisha kodi na tozo za mafuta kiujumla mpaka mgogoro uishe, hapo ndipo mseme kuwa nyinyi ni bunge la wananchi.




Narudia tena hatutaki mapunguzo ya kishkaji ya asilimia 2 au 10, Kodi na Tozo zisimamishwe mwananchi apumue



Jana hiyo hiyo Namibia wamefanya kweli, bunge letu tunawasubiri
 
Serikali haina msaada hapa, sababu haiwezi kujibinya, kubana matumizi, haiwezi kuasamehe hizo kodi sababu ndio matumizi yao
Karibu nusi ya bei ya mafuta ni kodi na tozo za serikali na zinakatwa percentage wise kutokana na CIF Price hii ina maana bei za maguta zikiongezeka basi makusanyo ya kodi na tozo nayo yanaongezeka.

Serikali wanaweza kuamua kutoka percentage wise kwenda fixed price per liter na bado bei ikapungua bila kupunguza makusanyo
 
- mwanzoni uliandika 'misenge'
-Hata wasingeshabikia Vita ingepiganwa tu, hawawezi kuzuia vita
- Kodi za kwenye mafuta zipunguzwe hiyo ndio solution
Kupunguza tozo kwenye mafuta ili kupunguza makali ya bei ya mafuta ni wazo zuri lakini pia huenda likawa suluhisho la muda mfupi tu

Kama bei za mafuta kwenye soko ka dunia zitazidi kupanda hizo tozo hata zikiondolewa zote haitakuwa na faida yoyote.

Imagine unanunua mafuta Tshs. 5,000/L na hakuna tozo yoyote itakuwa imesaidia chochote?

Cha muhimu mlango bahari ufunguliwe kwa sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…