Bei mpya za mafuta ni janga, Serikali punguzeni kodi za mafuta Wananchi wapumue

sasa kama wenye dunia wameamua wabondane, sie wengine tuamue vipi? Ni kushabikia tu upande mmojawapo, wabondane tani yao mpaka mbabe apatikane
Sawa ila ndio pale inasemwa ngumi za panzi zinazoumia nyasi
 
Wese linakwenda kukata sio kupanda bei, tutapaki magari tuu!
Nakumbuka longtime around 90's Sumbawanga huko, mshua alikuwa anapaki ki Peugeot chake 505 ana print kwenda kazini, mji mzima hamna wese. Sheli ipo moja tuu mji mzima.
Wese likija mnaenda nunua kwenye madumu tena kwa foleni, enzi hizo hao EWURA sijui watu gani hamna nchi hii.
Watu wanaishi na stock ndani ya wese, ni kupiga pipe tuu. 😁
Ajali za moto kila uchao, kisa wese. 😁
 
Sioni serikali yenu sikivu ikipunguza tozo. Acha tuone next months soko litasemaje
Labda usikivu wa makalioni, hawana usikivu wowote tu, hawa na akili za trump zimekosana kidoogo sana, huwa kuna kauli wanatoa unaona kabisa anaeambiwa wanahisi ni mjinga saana.

Serikali yetu ni watu wasio na huruma na wananchi wa taifa hili,
TUTAKOMA
 
Kama tulikuwa na akiba ya mafuta ya miezi 3,huku vita ya Irani ina mwezi moja tu why bei zipande huku yalinunuliwa kwa bei ya zamani
 
Algeria,Nigeria,Egypt,Angola & Libya wote hao wanazalisha mafuta-tunaweza kupunguza machungu kwa kununua kutoka hapa hapa Africa.
 
Wafia dini na walokole watapita hii komenti kama wanaaga maiti.
 
Je hayo mafuta ya 5000/ yakiwekwa tozo yatakuwa na Bei ile ile?
 
"Imagine unanunua mafuta Tshs. 5,000/L na hakuna tozo yoyote itakuwa imesaidia chochote?"
Kama mafuta yanauzwa 5000/- ukiweka tozo ndani yake Bei yake itakuwa zaidi ya 6000/-+ huoni hapo Kuna tofauti
Bado haujanielewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…