Ziro Buyu
Member
- Nov 1, 2016
- 39
- 39
Nipende kuipongeza serikali katika jitihada zake za kuboresha huduma za Usafifi wa Mabasi ya Mwendokasi Dar (DART).
Hivi karibuni DART wamefanya ukarabati wa vituo vya mwendo kasi kwa kuweka mifumo ya ukataji tiketi kwa kutumia Kadi ambapo kadi hiyo ni Kwaajili ya DART Tuu inauzwa Tsh 5000. Tukumbuke kunakadi ya N Card gharama ya kuipata ni 1000 ambayo inatumika maeneo mengi. Sasa kadi ambayo haina matumizi katika maeneo mengi inauzwa Tsh 5000 wakati N Card 1000.
DART walishakuwa na mfumo kama huu wa Kadi, wananchi wakanunua na wakawa nazo halafu mifumo yao ilipogoma wakawaacha wananchi na kadi zao pasina kusema chochote.
Nashauri kwanza, kwanini hiyo huduma ya DART ya isiongezwe kwenye N Card ili hata mifumo yao kifeli tena kuwe hakuna hasara kwa wananchi. Pili, Bei ya kadi ni kubwa ukilinganisha na huduma inayotolewa lakini pia tunajua LATRA ndio hupanga bei za nauli sasa hii bei ya kadi ni kigezo gani kilichotumika kupanga kadi iuzwe bei hiyo. Mwisho Kama ni muhimu DART kuwa na kadi yao basi zitolewe bure iwe kama namna wanavyogharamia tiketi za karatasi.