Bei ya mahindi kwa gunia la debe 6 lafika shilingi 9000

Kwa mazao ya chakula bado hiyo bei ya elfu 9 kwa gunia la debe 6 ni bei kubwa sana. Inabidi ishuke mpaka elfu 3 kwa gunia na mia tano kwa debe. Unga bei isizidi Tsh.100 kwa kg.1. Maisha yanakuwa magumu kwa sababu hata mazao ya chakula yamefanywa biashara..! Lazima tufike mahali tujue mazao ya biashara na mazao ya chakula. Zamani ilikuwa mtu akiwa anakuja dar kwa ndugu,anabeba unga,mahindi,viazi nk. Lkn siku hizi hakuna hizo zawadi kwa sababu ya tamaa ya fedha. Mtu anaona kukubebea kilo 20 za Mchele ni hasara! Mwacheni magu asimamie hii show,tunataka mpaka muwe mnapiga simu kubembeleza kuja kuchukua mahindi buree!!!
 
Nimetoka juzi nkasi na s'wanga gunia 18000 na wanunuzi hakuna.na NFRA wana nunua 30000 hatari sana
 
Huku niliko kilo 230 gunia lan kilo 100 ni 23,000/-
 
Huko duniani unakokusema hali ikiwa hivyo wakulima hufidiwa na pia kurahisishiwa hali ya pembejeo kwa serikali zao kutia ruzuku

Sent from my HUAWEI LUA-L21 using JamiiForums mobile app
 
Kwa dar kilo ya unga ni mia 6
 
Mmetucheka sana tuliolima mbaazi tukauza sh. 150/= kwa kilo, sasa ni zamu yenu, hayo mahindi tengenezeni pombe
hahahaha nimecheka sana mkuu sasa huoni kuwa tutatengeneza taifa la walevi???!!
 
Kwahiyo unataka tukuuzie gunia 200/= ilihali tumetumia gharama kubwa kwenye uzalishaji??Umeipa kazi ya bure shingo yako kubeba TIKITI MAJI badala ya kichwa!![emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
HAHAHAHAHAHAHAHAAAAAA
Aisee niko hapa napitia hizi comments nacheka sana,nasahau kwa muda shida zangu
 
Hiyo bei ime "editiwa" mkuu huku kwetu KATAVI ambako zao la Mahindi huzalishwa kwa wingi wastani Wa bei kwa gunia la ujazo Wa debe sita ni sh.36,000/=
 
Za jioni wandugu, naomba tushirikiane kuwaonea huruma wakulima mazao yanashuka bei ilhali pembejeo bei iko juu. Mliokaribu na wanasiasa washitueni 2020 sio mbali
mahindi sio kama NYANYA.. cha kufanya wakulima walio katika UNIONS.. wajikusanye waamue KUWEKA ndani mazao yao.. yakiadimika mtaani waanze kuyaachia kwa mlolongo ulio sahihi ili ku stablize price..
 
Za jioni wandugu, naomba tushirikiane kuwaonea huruma wakulima mazao yanashuka bei ilhali pembejeo bei iko juu. Mliokaribu na wanasiasa washitueni 2020 sio mbali
Wapi huko tudokeze tuvamie
 
Wakulima mungu anatambua kazi yetu njema,we waache tu Hapo wanaosema eti gunia liuzwe 3000 IPO Siku nao watakua wakulima
 
Hifadhini Mahindi ndugu zangu.

Neema yaja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…