Sean Paul
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 1,330
- 3,289
Ufisadi.Sio siri hili jambo linaniumiza sana moyo wangu sijui kuna ushirikina gani kwenye suala la sukari hapa nchini kwetu.
Maana licha ya kuwa tuko jirani na bahari kuu tuna ardhi nzuri na tuna kila fursa ya kunufaika kuliko majirani zetu lakini bado tunapata mateso ya kununua sukari kwa gharama kubwa kuliko jirani zetu wote.
Tangu nakua mpaka sasa ni mtu mzima mwendo ni uleule nakumbu ka nilisoma na jamaa mmoja alikuwa akienda na baiskeli kuchukua sukari za magendo Zambia na kuiuza Tanzania Kisha analipa ada.
Ndugu zangu wafanya maamuzi hebu kuweni serious basi.
Pia, soma=> Munde Tambwe: Kwanini Tanzania Bei ya Sukari ni kubwa kuliko Zambia, Malawi na Rwanda? Kuna Tatizo mahali tuambiane ukweli!
Vibali vya kuagiza sukari wanapewa hao hao wanaoshindwa kuilisha nchi na sukari wanayozalisha hapa ndani. Kwanini sukari isiagizwe tu kama nguo?
Mnalinda viwanda vya ndani, viwanda mnavilinda miaka kibao havibadiliki vya nini sasa?
Bashe na genge lake wamekumbatia wahindi wanaendelea kuwatajirisha huku wao wakipokea bahasha.