Bei ya sukari yaanza kupaa na bei ya unga yazidi kuongezeka

Bei ya sukari yaanza kupaa na bei ya unga yazidi kuongezeka

kilo zaidi ya elfu 4. haipatikani.

mtaani kwako hali ikoje!?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Jamani bei ya sukari imeanza kupanda sasa kilo ni 3200 huku bei ya unga nayo ikipanda sana hadi 2100 kwa kilo

Sukari ni baada ya serikali kupiga marufuku kuingiza sukari kutoka nje?

Nashindwa kuelewa kwanini bidhaa nyeti kama sukari izuiwe kutoka nje kwa maneno eti wanalinda viwanda vya ndani?
Viwanda vya ndani vinalindwa vipi wakati sukari inapanda?

Nakumbuka wakati wa tatizo la sukari nchini mwaka 2016 kama sikosei ilisababishwa na haya haya mambo ya kuzuia sukari kutoka nje isiingie mwisho tukaliingiza taifa kwenye hatari kubwa

Serikali inapaswa ihamasishe export zaidi lakini haimaanishi kubana watu wanao-import bidhaa nchini hususan sukari na vyakula muhimu ambavyo uwepo wa bidhaa shindani unasaidia kuondoa mfumuko

Serikali kwanini suala la mfumuko haitilii maanani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi maccm wakienda dukani wanapata nafuu ya bei? Maana kusifia hadi kero!
 
Back
Top Bottom