KERO Bei ya Vitunguu Maji Singida na Manyara ipo chini, inatuumiza Wakulima

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakulima wa vitunguu maji tuna changamoto, bei ya vitunguu iko chini sana Mkoa wa Singida na Manyara. Wakulima tunapata hasara sababu ya pembejeo za kilimo zipo juu lakini wanunuzi wanajipangia bei ndogo na pia wanaweka ujazo ambao serikali imekataza.

Ombi letu waruhusu wanunuzi kutoka nje ya nchi, watusaidie kwenye bei pamoja na ujazo.
​
 
Hayo mazao ya viungo hayana regulator so watu wanajipigia tu, poleni maana Mtaendelea kuteseka Hadi pale ww mkulima utakapopata chimbo lako la kujipatia pesa, mazao kama hayo yanahitaji mifumo mizuri ya kiteknolojia au namna ya kuyaongezea thamani.
 
Bei ndogo isiyo tajwa. Huu uzi auna maana.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Poleni wakulima. Hii si tu wizi na unyang'anyi unaofanywa mchana kweupe.
 
Watu ambao hawajaenda shule huwa wanafanya biashara kipumbavu sana. Kwanini ujazo uwekwe hivyo?
 
This is totally unfair kwa wakulima huo ujazo tuna uitaje kitaalamu?
Uku masokoni kg 1 ya vitunguu tuna nunua Tsh 1000 hii ikimaanisha bei iliyo nunuliwa shambani n ya chini au nusu ya hiyo.
Kwa mkulima gharama zina rudi? Kuna mamlaka yoyote inayo simamia hizi bei na ujazo wa aya mazao.?
 
Iko chini kiasi gani?
 
Si Bora huko kilo 1000 huku nilipo Musoma kilo 1 ni 3000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…