Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Mafinga na kitonga kwakweli bei zimezidi maradufu kulingana na vyakula husika ubora hakuna yani ni tabu tupu
 
Kumbe victims wa hili tuko wengi nishakulaga mishikaki hata sijuagi ni ya nyama gani pale msamvu kma unaenda dom kila mtu anasema lake wengine punda wengine ndege pori yaani kyaaa ila yote kwa yote mungu anawaona sio kwa kunionea kule mtanzania mwenzenu
 
Tumbo linaweza kukufanya ukutane na simba porini,mana likivuruga huchagui wapi ujisaidie mana unakuta mda huo kinyesi kinagonga hodi kyupini
 
Juzi wakati natoka Kigali tulisimama eneo fulani. Basi kama mnavyojua wanaume wa Dar tunapenda Chips zege. Ile najitosa kutoa oda, mhudumu ananiambia chips zege ni tsh 6000.

Nikabaki kutoa macho badala ya kutoa hela.
Sasa si unaona, toka lini zege inauzwa 6000. Tunaomba wale waloshinda kwa kishindo watusaidie shida hii. Si wote wenye uwezo wa kununua chakula kwa gharama hizo.
 
Mafinga na kitonga kwakweli bei zimezidi maradufu kulingana na vyakula husika ubora hakuna yani ni tabu tupu
Tuzidi kupiga kelele ili wahusika washughulike hili tatizo. Inakera sana
 
Yule jamaa wa mabasi yaABC naye kafungua hoteli yake pale Morogoro wali nyama sh 7000 mshikaki 3000 marufuku kubakia kwenye basi abiria wote mnashushwa mnalazimishwa kwenda hotelini.
 
Tatizo siyo hizo migahawa bali tatizo hali ni mbaya mifukoni mwa watanzania wengi maana hizo bei bado zinaonekana za kawaida tu ni sawa na usd 3 lakini kwa mwananchi anayeishi chini ya dola moja kwake ni habari mbaya sana kwake. Hali ikiwa nzuri kimaisha wala hutaweza kufikiri hayo yote.
Maisha ni magumu sana mfano ni miaka minne na miezi kadhaa serikali haijaongeza mishahara kwa wafanyakazi kwa mujibu wa sheria (according to annual increment act) lakini viongozi wa vyama vya siasa wapo wanahangaikia matumbo yao tu, wabunge nao kimya, sasa sijui nani mtetezi wa raia wa kawaida
 
Yule jamaa wa mabasi yaABC naye kafungua hoteli yake pale Morogoro wali nyama sh 7000 mshikaki 3000 marufuku kubakia kwenye basi abiria wote mnashushwa mnalazimishwa kwenda hotelini.
Unaona sasa, haka kasecta kamesahaulika sana. hakuna anayekaangalia kuhusu mlaji, isipokuwa wale watu wa mapato na afya wakishapita basi. mlaji atajijua mwenyewe.
 
Ni kweli kwasababu watanzania walio wengi ni wakulima na wafugaji ambao kwa vyovyote vile wanaishi chini ya dola moja. na katika secta ya uma kama hali ni mbaya basi hata ule mzunguko wa hela ni shida. ni maombi yetu sasa serikali iliangalie hili suala la hii migahawa ili walaji watendewe haki.
 
Mimi siku hizi nimembuni binu mpyaaa nikifika kwenye hivyo vihoteli kama nina njaa naagiza chai ya rangi na mandazi au chapati. Uwezekano wa vitu hivyo kuwa vimechacha ni mdogo, na ukiwa na 2000 inatosha.
 
Mi nimi
Tuzidi kupiga kelele ili wahusika washughulike hili tatizo. Inakera sana
nimeishia kumwaga chakula maranyingi....
 
Yule jamaa wa mabasi yaABC naye kafungua hoteli yake pale Morogoro wali nyama sh 7000 mshikaki 3000 marufuku kubakia kwenye basi abiria wote mnashushwa mnalazimishwa kwenda hotelini.
Uongo,sijawahi shushwa abc na nasafiri nalo mara kwa mara
 
Hili sidhani kama linahitaji mamlaka kulidhibiti. Kwa kifupi limejengwa na sisi watanzania wenyewe.Kwani mtu unashindwa kujibebea chakula chako? Mama una watoto wadogo, unaandaa chakula kinachobebeka kirahisi unakula na wanao njia nzima.

Mimi najibebea mahindi ya kuchemsha na mayai. Nikifika hizo hoteli nakwenda kuwajazia choo tu, sigusi vyakula vyao. Kwanza si salama wala havina ladha. Chips mafuta kibao ,halafu nyeusi.Wali ladha ya udongo,kha!

Abiria tukiamua wanafunga hizo hoteli ndani ya siku moja tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…