Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Watu wa mabasi ndo wahusika. Hizi hoteli unakuta ni zao so lazima wakupeleke pale. Sehemu nyengine staff hula bure.
Wadau wanaseme, dereva anapoingiza basi kwenye hoteli tayari ana 60,000 yake mfukoni plus kula bure chakula akitakacho yeye na wasaidizi wake. Haki ya abiria hapa iko wapi? mamlaka kwakweli watusaidie tu
 
Wapuuzi sana yani af wanakupeleka sehem ambayo hakuna vibanda vungine vya chakula ili ulazmike kununua kwao tu... Ni miradi yao hii ya kutupiga hela af bora hata wamgekua wanapika vizuri
 

Aiseee umenichekesha mno usiku huu!

Boss, Fanya mpango wa hilo hotpot la kuchimbia dawa likitengenezwa na mi nilipate itapendeza zaidi maana nasafiri kama Vasco Dagama halafu maliwato si rafiki kabisa na ukibana mkojo safari nzima ni janga lingine.
 
Nangurukuru zamani ulikuwa unaweza nunua maji chupa ya kilimanjaro lakini ni maji ya mtoni na yako na seal kabisa sijui walikuwa wanafanyaje fanyaje.
 
Huko sio kupanga bei ni kuwalazimisha watu wale kwa hiyo bei
Nasema hivyo kwa sababu mabasi husimama kwenye hizo hotel na ndo pahala pekee penye hizo huduma kwahiyo abiria hana mbadala lazima ale hapo
Nashauri mabasi yalazimishwe kukaa muda wa kutosha kwenye stendi za mikoa ili watu waingie kwenye mabanda ya mama lishe ambako vyakula bei zake huwa ni nzuri
 
Nkijua nasafiri kesho

usiku wa leo ntakula Nyama choma si kawaida

pakikucha naenda zangu safari yangu,safari nzima ntaanza kuskia njaa

nikishafika niendapo ila mara zote gari ikifika sehemu ya kula nakuaga nimeshiba

pale nanunuaga maembe/papai wananimenyea nalila pale pale.
 
Nangurukuru zamani ulikuwa unaweza nunua maji chupa ya kilimanjaro lakini ni maji ya mtoni na yako na seal kabisa sijui walikuwa wanafanyaje fanyaje.
Pale yani wanajifanya wajuaji sana, ngoja tutafte dawa yao.
 
Naunga Mkono hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa tutarudi enzi za miaka ya 80's, nakumbuka tukiwa tunasafiri na bi-mkubwa ilikuwa lazima apike chakula cha safari kwenye kimfuko cha naironi then kinatunzwa kwenye kikapu... mzee ukijisikia njaa tu bi-mkubwa anafungua kifuko acha kabisa.
Hiyo ht maza alikua nayo..enzi tren halziengui...mnapikiwa maandazi na maji dumu lita 5!kituo Mwanzaaa...!khaaa hahahahaha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…