Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Bei ya vyakula vya mahoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri wa mabasi iangaliwe na mamlaka husika

Watu wa mabasi ndo wahusika. Hizi hoteli unakuta ni zao so lazima wakupeleke pale. Sehemu nyengine staff hula bure.
Wadau wanaseme, dereva anapoingiza basi kwenye hoteli tayari ana 60,000 yake mfukoni plus kula bure chakula akitakacho yeye na wasaidizi wake. Haki ya abiria hapa iko wapi? mamlaka kwakweli watusaidie tu
 
Wapuuzi sana yani af wanakupeleka sehem ambayo hakuna vibanda vungine vya chakula ili ulazmike kununua kwao tu... Ni miradi yao hii ya kutupiga hela af bora hata wamgekua wanapika vizuri
 
Nikisafiri huwa nabeba hotpot lenye mixer pilau kidogo,mweupe kidogo,kuku kavu,ng'ombe kavu,majani kidogo,pilipili kwa mbali,maji kubwana soda kubwa ya kopo.
Hilo hotpot linaitwa traveller hotpot lina vyumba kibao na linatunza joto masaa 56 na ni ndogo yani saafi na bei yake ni rafiki.
Nilinunua baada ya kupata shida kama hizo hotel za kitonga kule.
Yani saizi nagharamia kuchimba dawa tu lkn napo natafuta hotpot la kuchimbia dawa.
Wakisema kushuka kwenda kula na kuchimba dawa hotelini mi nashuka na hotpot langu nakaa chemba nafanya yangu nafunga tight.
Hela zenyewe zipo wapi bna.

Aiseee umenichekesha mno usiku huu!

Boss, Fanya mpango wa hilo hotpot la kuchimbia dawa likitengenezwa na mi nilipate itapendeza zaidi maana nasafiri kama Vasco Dagama halafu maliwato si rafiki kabisa na ukibana mkojo safari nzima ni janga lingine.
 
Nangurukuru zamani ulikuwa unaweza nunua maji chupa ya kilimanjaro lakini ni maji ya mtoni na yako na seal kabisa sijui walikuwa wanafanyaje fanyaje.
 
Soko huria, serikali ikipanga bei za mazao tunailalamikia, wacha soko lipange bei, ni fursa pia kwa wanaotaka kuuza cha kula kwa bei ndogo wakafungue mahoteli ili ushindani uwe mkubwa.

Mwisho kabisa sio lazima kula njiani, nunua maji na korosho za kutosha utakula unapoenda kama una watoto mwambie mama yeyoo awapakilie vyakula.
Huko sio kupanga bei ni kuwalazimisha watu wale kwa hiyo bei
Nasema hivyo kwa sababu mabasi husimama kwenye hizo hotel na ndo pahala pekee penye hizo huduma kwahiyo abiria hana mbadala lazima ale hapo
Nashauri mabasi yalazimishwe kukaa muda wa kutosha kwenye stendi za mikoa ili watu waingie kwenye mabanda ya mama lishe ambako vyakula bei zake huwa ni nzuri
 
Nkijua nasafiri kesho

usiku wa leo ntakula Nyama choma si kawaida

pakikucha naenda zangu safari yangu,safari nzima ntaanza kuskia njaa

nikishafika niendapo ila mara zote gari ikifika sehemu ya kula nakuaga nimeshiba

pale nanunuaga maembe/papai wananimenyea nalila pale pale.
 
Nangurukuru zamani ulikuwa unaweza nunua maji chupa ya kilimanjaro lakini ni maji ya mtoni na yako na seal kabisa sijui walikuwa wanafanyaje fanyaje.
Pale yani wanajifanya wajuaji sana, ngoja tutafte dawa yao.
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikikerwa na hili jambo.

Bei ya chakula cha hizi hoteli/migahawa ya njiani kwa wasafiri haiendani na huduma wanayopewa lakini naona mamlaka husika zimekaa kimya. Na hili naomba lisichanganywe na suala la wakulima kujipangia bei, msafiri sio mkulima ni mtu anayekuwa hana option maana pengine amesafiri masaa kumi na mbili au ishirini bila kuonja kitu na analazimishwa anunue chankula kwa bei ya juu. Au anaenda hospitali kupeleka mgonjwa.

Kiuhalisia sahani ya wali nyama ni 1500 - 2000 lakini kwenye hiyo migahawa wali nyama wanauza 5000 - 6000. Mbaya zaidi vile vidada vihudumu vinanyodo utafikiri vinahudumia hoteli ya nyota tano kumbe mgahawa wa barabarani tena kwa wasafiri (ref: nangurukuru). Ukiviambia dada ongeza kidogo basi ili nishibe kanakukata jicho utafirikiri umetoa mawe kumbe umetoa 6000.

Wanaosafiri wengine ni wagonjwa, watu wa vijijini na wengine hawajiwezi kabisa, unapomlazimisha mtu kuwa tutachimba dawa hoteli fulani na kupata chakula hapo ni ukiukwaji wa haki za wasafiri. Kwanini mamlaka wasimoderate na kucontrol hili suala? ikiwezekana sehemu ya kuchimba dawa ijitegemee na sehemu ya kula ijitegemee ili hao watoa huduma wasiwalipishe watu bei kubwa kisa umechimba dawa kwao.

Madereva na makondacta wao huwa hawalipii hiki chakula kwasababu ni deal kwa mwenye hicho kihoteli. hii ni ajabu sana, ndio maana inapelekea hawa madereva wanawapeleka abiria sehemu ambayo mwisho wa siku watalazimika kulipia hata kama hawataki.

Naomba mamlaka husika waaanze na Nangurukuru, Singida, Shinyanga, Morogoro, Alj jazeera na sehemu zingine ambazo mimi sijafanikiwa kupita huko kwasababu inakera sana na ni ukiukwaji wa haki za wasafiri kabisa kuwalazimisha kupata huduma wasipopenda halafu mbaya zaidi kwa bei ya juuu kuliko uhalisia.

Bei ya choo cha kulipia inajulikana ni 300, Bei ya wali maharage inajulikana 1500-200, bei ya wali kuku inajulikana ni 3000-4000, bei ya kile kitake away inajulikana kuwa ni 300. Iweje tutozwe bei zisizoendana na uhalisia?

Wakuu wa nchi wao husafiri na private mara nyingi kwahiyo hii inweza isiwe na mashiko sana kwao, lakini kiuhalisia vyombo vya dola na mamalaka za miji na halimashauri ambako huduma hizi hutolewa inabidi walichukulie serious.

Wakuu Nawasilisha, naomba ndugu zangu tusaidiane kupinga huu unyanyasaji kwa abiria.

Pia soma

Naunga Mkono hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa tutarudi enzi za miaka ya 80's, nakumbuka tukiwa tunasafiri na bi-mkubwa ilikuwa lazima apike chakula cha safari kwenye kimfuko cha naironi then kinatunzwa kwenye kikapu... mzee ukijisikia njaa tu bi-mkubwa anafungua kifuko acha kabisa.
Hiyo ht maza alikua nayo..enzi tren halziengui...mnapikiwa maandazi na maji dumu lita 5!kituo Mwanzaaa...!khaaa hahahahaha!
 
Back
Top Bottom