Bei za bati na bati imara ni zipi kutoka kampuni gani?

Bei za bati na bati imara ni zipi kutoka kampuni gani?

Hatarini za majukumu wana JAMIIFORUMS nimeandika uzi huu kuulizia au kujua bati imara na nikampunigani ya kuzalisha bati hapa nchini ina toa bati imara na inayodumu kwa muda mrefu bila kupauka.

Kumekuwepo utitiri wa viwanda vingi, hofu ni kwamba uzalishaji wake katika bidhaa zao ni wa mashaka.

Mfano; kuna kampuni moja niliwahi kufanya nao biashara pc kama 200 nilicholetewa zile zilikuwa siyo bati ni karatasi aisee nilijuta kufanya biashara na wale jamaa pamoja na kwamba walitoa kiwandani ila uchakachuaji ni levo nyingine huenda wamesomea kufanya vitu chini ya kiwango.

Kwa mafundi na wataalamu wa mabati kampuni ipi inazalisha bati nzuri na kwa bei ya kawaida, maan sisi wengine siyo tunaunga unga ndio maana nikasema bei rafiki ili niimudu kwa bajeti yangu niliyonayo.

Nahitaji bati 108 nyeupe G30 kwenye kazi hii
Utapewa blaa blaa nyingi lakini ukweli ni ALAF pekee kwa Tanzania.
Ukiwa uko vizuri zaidi wahi NABAK Afrika.
1. Ubora na gharama ni mapacha
2. Ubovu na chee ni wana ndoa
 
Alternative ya Alaf ni mabati ya Sunshare, hutajuta
 
Sunshare-Kwa bati za migongo mipana Bei zao zipoje mkuu!?
Zipo chini compared to Alaf... Kwa sasa sijajua bei zao zilivyo lakini check page zao Instagram wapo utapata mawasiliano yao, bati zao hazichuji wala kufubaa na ni bei rafiki kwa Mtanzania
 
Utapewa blaa blaa nyingi lakini ukweli ni ALAF pekee kwa Tanzania.
Ukiwa uko vizuri zaidi wahi NABAK Afrika.
1. Ubora na gharama ni mapacha
2. Ubovu na chee ni wana ndoa
Sasa hivi kuna lodhia nao wanazalisha mabati, kiwanda chao ni kikubwa kuliko Cha ALAF, pia uzalishaji unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi, nadhani amekuja kupambana na mkongwe ALAF ngoja tuone
 
Hivi Alaf bati la gauge 28 wanauza shngapi anaejua wakuu
 
Hivi Alaf bati la gauge 28 wanauza shngapi anaejua wakuu
Mengine sijui.

Najua aina ya ROYAL ROMANTILE, gauge 28 kwa mita niliagiza kiwandani kwa Tsh elfu 27 na point.

Bati moja la mita 3 nilinunua Tsh almost 84k.
 
Mengine sijui.

Najua aina ya ROYAL ROMANTILE, gauge 28 kwa mita niliagiza kiwandani kwa Tsh elfu 27 na point.

Bati moja la mita 3 nilinunua Tsh almost 84k.
Hii ipo juu sana bati la m3 tsh 84k? Duu
 
Nakutumia price list ya bei ya kiwandani, niliyotumiwa.

Kama upo Dar, unaweza kuwatembelea.

IMG-20241209-WA0003.jpg

Nilitaka gauge 28 rangi kwangu sio kipaombele

Ila nahisi kuugua kwa hizo bei nyumba inataka pc 85
 
Back
Top Bottom