Bei za Mafuta: Spika Tulia asema Bunge ndio linatunga Sheria sasa kama Serikali haitekelezi basi kuna tatizo kubwa

Bei za Mafuta: Spika Tulia asema Bunge ndio linatunga Sheria sasa kama Serikali haitekelezi basi kuna tatizo kubwa

Mbunge wa Sengerema Mh Tabasamu amesema tenda za mafuta wangepewa TPDC na Puma ambako serikali ina hisa zake basi bei ya mafuta isingepanda kwa kiasi ilichopanda.

Tabasamu amesema waagizaji wa mafuta wanaoleta sasa bei yao ni mara mbili ya ile waliyoquote TPDC wakati wanaomba tenda. Lakini TPDC akanyimwa na leo tunalia mfumuko wa bei kila kona ya nchi.

Spika Tulia amesema mh Tabasamu ana hoja nzito sana lakini ni lazima tuangalie sheria ya procurement inasemaje.

Ni sisi wabunge ndio tumetunga hizo sheria, je zinafuatwa na serikali? Na kama hazifuatwi hali inayopelekea bei kupanda hovyo basi kuna tatizo kubwa, amesisitiza Dkt. Tulia.

Chanzo: TBC

Samia yeye kama samia anasemaje kwwni
 
Mama wamemuweka bize kuzindua vitu vya ovyoovyo huku wao wakolipitisha mambo ajabu.

Nilishasema huyu Makamba ni tatizo haaminiki kabisa
 
Ujanja ujanja mwingi sana kwenye nchi yetu na anae umia ni raia wa kawaida.
Kuna rais nchi hii alikuwa muaminifu sanaaa aliyoyashuhudia akiwa hai alikufa kwa kiharusi tungali twamuhitaji. Ilikuwa funzo sana kwa kijana wake yule mjanja mjanja aliyeonekana muaminifu zaidi ya Mamvi, huyu kijana wa mwalimu tulipo mpa nchi aliamua awe mtiifu kwa familiar yake na anafanya hivyo hata leo
 
January anahitaji utulivu wa kisaikolojia wakati huu.... sijui kama mi pekeangu nakumbuka hili ..... nilimsikia mama anasema waziri aliondoa tozo ya shilingi 100 kwa lita ila hakufanya tathmini vizuri, narudisha hyo tozo mafuta yatapanda bei na nauli zitaongezeka... lazima niwaambie ukweli.
 
Back
Top Bottom