Bei za nauli za treni za kwenda Morogoro na Dodoma zinatakiwa ziwe juu zaidi ili kuweka uwiano wa biashara kati ya mabasi na treni

Katika kuhakikisha kwamba sekta ya usafirishaji wa abiria nchini inakuwa na uwiano mzuri wa kibiashara kati ya mabasi na treni, kuna haja ya kuangalia upya bei za nauli za treni kwa safari za kwenda Morogoro na Dodoma.

Ili kuboresha uwiano wa biashara na kutoa nafasi kwa mabasi kuendelea kushindana, napendekeza nauli za treni ziwe juu zaidi. Hatua hii itasaidia kuimarisha sekta ya mabasi na kuhakikisha kuwa vyombo vyote vya usafiri vinaweza kuendelea kutoa huduma kwa tija, huku abiria wakipata uhuru wa kuchagua usafiri kulingana na vipaumbele vyao bila kuathiriwa sana na tofauti kubwa za bei.

Kwa kuongeza nauli za treni, sekta ya mabasi itapata nafuu ya ushindani na hivyo kusaidia kudumisha watoa huduma wengi kwenye soko. Hii siyo tu kwamba itachochea ukuaji wa sekta zote mbili bali pia itahakikisha huduma za usafiri zinapatikana kwa wingi na kwa ubora zaidi kwa wasafiri.
ujinga umeandika
 
Kinacho wavutia watu kwenye treni ni speed ya treni ili wafike haraka. Kwa hiyo unataka watu wa mabasi waongeze speed kama ya treni. Watu wa mabasi hawawezi kuboresha speed ya mabasi kufikia ya treni.
wamiliki wa mabasi ya abiria wanatakiwa wafanye wanachoweza wafikirie wanachoweza POSITIVE THINKING bila kuathiri biashara ya mwingine sgr.
 
Sijakengeuka boss
Basi wahurumie raia wa chini nao wafaidi mema ya nchi yao.

Siyo wewe unatumia masaa 3 Dar to Dom, halafu unataka wenzio wahenyeke kwa kusafiri masaa 9. Kuweni na utu angalau kidogo mkuu.

Kama hiyo njia ya Dom haikulipi kwa sasa, unaweza kupeleka mabasi yako kwenye ruti zingine zisizo na reli kama Mtwara, Songea, nk
 
Katika kuhakikisha kwamba sekta ya usafirishaji wa abiria nchini inakuwa na uwiano mzuri wa kibiashara kati ya mabasi na treni, kuna haja ya kuangalia upya bei za nauli za treni kwa safari za kwenda Morogoro na Dodoma.

Ili kuboresha uwiano wa biashara na kutoa nafasi kwa mabasi kuendelea kushindana, napendekeza nauli za treni ziwe juu zaidi. Hatua hii itasaidia kuimarisha sekta ya mabasi na kuhakikisha kuwa vyombo vyote vya usafiri vinaweza kuendelea kutoa huduma kwa tija, huku abiria wakipata uhuru wa kuchagua usafiri kulingana na vipaumbele vyao bila kuathiriwa sana na tofauti kubwa za bei.

Kwa kuongeza nauli za treni, sekta ya mabasi itapata nafuu ya ushindani na hivyo kusaidia kudumisha watoa huduma wengi kwenye soko. Hii siyo tu kwamba itachochea ukuaji wa sekta zote mbili bali pia itahakikisha huduma za usafiri zinapatikana kwa wingi na kwa ubora zaidi kwa wasafiri.
Vp unaonaje moro wafanya 50000 na dodoma wafanye 100,000 unasemaje mdau

Ova
 
Wachawi mmeanza mnajifanya wema kumbe mnataka kuua, wewe hajawahi kusafiri kwenda mikoaani si ka basi qala treni leo unajifanya mchimi wakati ni mpigadebe wa basi la Katarama!
 
Nina mashaka wakati wa mvua kama hawajafanya hujuma kule kwenye mito ya Gulwe na Godegode ili kuharibu miundo mbinu ya reli...
Hili mbona liko mbioni kutokea kaka, kwani ile ya kutoka dar kwenda Arusha ilikuwaje? Si hao hao makanjanja wanaomiliki mabasi waliifanyia uhuni wakishirikiana na viongozi washenzi wa serikali kuiua na baishara ya mabasi isiyumbe?

Amini na nakwambia Raisi Samia asiposimama kidete hii SGR inaweza isimalize hata miaka mitano njia zake zitaota nyasi na vyuma vitaibiwa vikapimwe kwa wanunuzi wa vyuma chakavu.
 
Ach
Pia, nauli zipandishwe ili kupunguza walalahoi kujazana kwenye treni, halafu wakiwa nadani ya treni wanatamani kushuka/kuondoka na kila wanachokiona e.g feni, taa, koki, na makava ya viti.
Acha dharau
Jifunze kuwa na adabu
 
Wachawi mmeanza mnajifanya wema kumbe mnataka kuua, wewe hajawahi kusafiri kwenda mikoaani si ka basi qala treni leo unajifanya mchimi wakati ni mpigadebe wa basi la Katarama!
Unatakiwa kukocoment mawazo boss usitaje majina ya vitu wala kuwasema watu
 
Kila siku mnawaza namna ya kuhujumu Serikali tu, watu wa namna hii ni wa kuwapiga risasi tu, kuendelea kuishi nao ni kuangamiza Taifa.
Nani akuhujumu mkuu bei ziongezwe na watu watapanda mbona mwendokasi wanapanda.
 
Back
Top Bottom