Hivi umewaza mataifa kama Japan,China na Singapore wangekuwa na akili za kipumbavvu kama hizi zako leo hii wangefika hapo alipo kimaendeleo?
Kwamba na wao wangesema wabaki kwenye usafiri wa mabasi tu na wasijiangaishe kabisa na kufanya mapinduzi ya usafiri wa tren, leo hii wangekuwa Wana tren za kisasa zenye uwezo wa kusafiri Bara na Bara??
Hivi unajua kwamba kama wote tungekuwa na akili hizi za kupuuzi leo hii hata hiyo Simu usingekuwa nayo na badala yake ungekuwa Bado unatumia barua kuwasiliana na watu walioko mbali na wewe? Una habari kwamba ujio wa simu umeua kabisa matumizi ya posta?? Sasa vuta picha kwamba wamiliki wa posta nao wangesema simu ziuzwe kwa bei ya juu sana kiasi kwamba ni raia wacheche wawe na uwezo wa kuafford hili majority waendelee kutumia barua, je tungekuwa Bado tuko wapi kimaendeleo?
Watu wenye akili za kipumbavvu kama zako wavivu wa kufikiri ndio wamefanya mpaka leo hii watanzania Bado tunaitegemea TANESCO kwenye huduma ya umeme shirika ambalo matatizo yake ni Yale Yale tu miaka nenda miaka Rudi..!!
Majitu kama wewe ambao mmejawa na akili za kimwinyi na msiojua kuendana na mabadiliko ni kikwazo kikubwa Sana Cha maendeleo.
Hapo Kenya Sasa hivi wanautumia Starlink ya Elon Musk kwenye huduma ya internet, na ujio wa starlink umefanya makampuni makubwa ya mitandao ya simu kama SAFARICOM kupunguza bei ya vifurushi vya internet sambamba na kuongeze speed hili kukabiliana na ushindani wa ghafla wanauopata kutoka Starlink..
Wafanyabiashara wa kibongo mnapenda kumonopoly biashara halafu akili za kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia hamna, yaani mko tayari kulirudisha taifa nyuma kimaendeleo hili tu biashara zenu zistawi wajinga sana nyie.