Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Uwajibikaji gani wewe unaoutaka??Acheni kuwalaumu wadau, bila wenyewe kuwajibika.
Tatizo letu liko hapo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uwajibikaji gani wewe unaoutaka??Acheni kuwalaumu wadau, bila wenyewe kuwajibika.
Tatizo letu liko hapo.
Nimeshakujibu hoja hii, wamefanikiwa sababu Bei yao ilikuwa kubwa Sana, Even hio Bei elekezi yao kwa sasa ni kubwa kushinda Bei yetu.Usiniwekee maneno mdomoni mjomba. Hivyo jifunze kwanza kusoma mada kabla ya kuchangia.
Kwa msingi huu ulichoandika hakihusiani na mada, uko nje ya mada na hivyo wako utatusaidia tuuite je.
Mada ni kuwa serikali ya Kenya imelazimishwa kushusha na waandamanaji.
Ulinganifu na sisi ni kuwa vipi wenzetu wanafanikiwa lakini siyo sisi.
Jitathimini kama umejikita kwenye mada hiyo. Kama sivyo itapendeza ukijitendea haki mwenyewe kutupa mrejesho kuwa hukuelewa.
brazaj mfano wako wa maandamano ya Kenya kumhushisha Laila unakosea sana. Ukijikumbusha vita ya Mau Mau utaona kwamba wala si suala la Laila Wakenya kuwa vile.
Lakini pia unajua ushawishi wa Laila Nairobi unatokana na nini. Tafuta kwa karibu habari za Kibera ujielimishe. Mbona siyo Kenya Nzima walioandamana??
Maandamano huratibiwa kwa watu waliotayari kuandamana ila huwezi kuratibu maandamano kwa watu wasio tayari kuandamana. Watanzania ni waoga wa kuandama dhidi ya serikali. Kenya hata bila ya Raila wataandamana tu maslahi yao yanapotishiwa!!
Nimeshakujibu hoja hii, wamefanikiwa sababu Bei yao ilikuwa kubwa Sana, Even hio Bei elekezi yao kwa sasa ni kubwa kushinda Bei yetu.
Uwajibikaji gani wewe unaoutaka??
Unataka unga ushuke Tz si ulime shamba lako...unafata wakenya ambao wamezungukwa na jangwa
Kwaiyo we unataka tufanye nini Tuandamane aza wewe kwanza na baba ako kisha wengine tutafuata
Wala sioni kama ni suala la kuoneana aibu au vinginevyo, kwangu naona tatizo lipo kwetu na ndio maana wengine husema wacha kina Mbowe walambe asali, wameshahangaikia sana watu wasiojitambua badala yake hakuna walichoambulia zaidi ya kufungwa jela wao binafsi.
Kama watanzania tungekuwa tunajitambua, yule Mbowe asingefungwa jela miezi sita, lakini kwa wakenya hali ni tofauti, wakijaribu kumkamata Raila, wakenya wataingia barabarani naturally, ndio maana nakwambia wakenya movement zao zinaanzia inside, wala sio lazima awepo kiongozi wa kuwaamsha.
Acha porojo. Kuna utopolo mmoja alidai kila kitu kitapanda bei. Hiyo ni kabla ya vita ya Ukraine. Vilivyokuja kupanda kabla ya hiyo vita, baadae ikawa kisingizio kuwa vita ndio imepandisha bei ya kila kitu. Serikali dhaifu, hushirikiana na wafanyabiashara kuumiza wananchi. Mfano tu bando za makampuni ya simu.Mbona hujatuonyesha mchanganuo wa bei zilivyoshuka badala yake unaongea ujinga ujinga tuu.
Tanzania Huwa haiigi upuuzi, uzalishaji na soko ndio vitaamua bei.
Mengi unayoandika naona hayaendani na kile ninachokisimamia, mimi pointi yangu hapa ni moja tu, watanzania ni waoga.Nimeyasoma vizuri mawazo yako, hata hivyo nashindwa kukubaliana nawe ndugu mjumbe.
Ikumbukwe kutofautiana kimawazo hasa katika mapambano ya ukombozi ni jambo la afya tu. Ndiyo maana SA kulikuwa na ANC pia PAC wote wakiwa marafiki wa Tanzania ya Nyerere. Bado Chris Hani aliyekuwa mwanachama wa PAC akawa mkuu wa majeshi ya ukombozi ya ANC, Umkonto we Sizwe.
(Aibu kwake mjumbe huyu UmkhontoweSizwe lakini).
Anasema Chidumule, hata watoto mapacha hutokea wakati hukosa kuelewana sembuse mimi na wewe?
Kwa kauli yako hii:
"... ndio maana wengine husema wacha kina Mbowe walambe asali, .."
Tegemea siku moja kusikia kina Mdee kurejea CDM na longo longo za kuwa wamesamehewa.
Nikuombe kuitunza post yako hiyo Inshallah tutakumbushana siku moja isiyokuwa mbali sana.
"Hii nchi haitakombolewa na wahuni, walamba asali au wale vijana wa hovyo."
Kutokuangaliana usoni niliko jatrbu kukuonyesha hakuna maana ya kuoneana aibu peke yake kama unavyojatibu kuninukuu. Hapa nimemaanisha dhana nzima ya kutoelezana ukweli kwa sababu zozote zile.
Sababu za kutoelezana ukweli zipo nyingi zikiwamo pia uchawa, hofu, opportunism (u - mkakati), malengo fiche, hujuma, nk.
Opportunism pia malengo (fiche) yenye mwelekeo wa njaa binafsi si ya kupuuza. Ikumbukwe ukombozi wa nchi hii ni muhimu zaidi kuliko mtu au jambo lolote linalolenga maslahi binafsi.
Raila anaitikisa Kenya na watu wasiofika 5,000 kwenye harakati zake za ukombozi Nairobi. Kenya haiandamani nchi nzima wala si watu wote.
"Inafahamika kuwa hata huko walamba asali, wahuni na hata vijana wa hovyo wapo. Kwamba yaliyoko kwetu na kwao yapo. Hata hivyo ujasiri wa viongozi wao wenye misimamo isiyotetereka ni jambo la kupigiwa mfano sana."
Mbowe asingekamatwa Mwanza kama kungepatikana watu angalau 2,000 tu kuwa naye kibindoni kama inavyotokea kwa Odinga.
Mkutano aliokamatwa Mbowe ulikuwa wa chama.
Unamaana walikosekana wanachama 2,000 kati ya wanachama 8m + wa Chadema kuweka mazingira ya Mwenyekiti Mbowe kutokukamatwa?
Unadhani dhima zaidi ya kuhakikisha Mbowe hakamatwi ilikuwa kwa nani? Wafuasi zaidi (wanachama) wa Chadema au watanzania (wasio na vyama, TLP, CHAUSTA, hadi wa CUF huko) unaojaribu kuwaangushia jumba bovu?
Kwani BAVICHA jukumu lao nini Kumbe? Kwamba kumbe BAVICHA wanadhani nani ampiganie zaidi Mbowe kuliko wao?
"Niwaombe joni, Paskali na wenzao wa maana wanilinde kwa maana siasa siyo uadui."
Uzi huu hapa chini unahusika:
Upinzani - walio waoga (cowards) si Wafuasi
"Vita hivi ni vya kupiganwa Kwa vitendo na sisi siyo kwa kusakizia wengine kama ilivyoelezwa kwenye uzi huo hapo juu. Mbona Raila halii lii kuhusu kuungwa mkono? Mbona hakuna popote duniani wapigania haki walukowahi kulia lia kuhusu kuungwa mkono? Mbona si Maalim Seif? Mbona si wakati wa Chadema ya Dkt. Slaa?"
Hata hivyo, kama una maana wafuasi japo 2,000 hawakupatikana na hata BAVICHA nao hawapo, labda uwe wazi kuwa Chadema hawakuwa tayari kumlinda Mbowe au hawakuwa na mkakati wowote kuhusu usalama wa viongozi wao muhimu. Hakuwezi kuwa na jambo kingine ndugu mjumbe.
Kwamba chama hakikuwa tayari kumlinda #1 wao. Labda kama unafanya masikhara.
Kama ndivyo wa kulaumiwa ni Chadema na kuwajibishana kukafuata. Shughuli hizi zinahutaji mpanga mikakati mkuu mahiri sana (Chief Strategist). Haiwezi kuwa bora liende.
"Ukweli uko wazi na unajulikana. Tuwe na ujasiri wa kumfunga paka kengele."
Kuna hii post hapo juu. Kwangu ni namba #126 (kwenye uzi huu) nikimjibu bwana Allen Kilewella akiuliza wajibu ninaoutaka. Sijui kwako inaweza kuwa inasoma ni posts namba ngapi kutokana na tofauti hasa zikihusisha wajumbe tunao ignore. Ninadhani ina maelezo zaidi kuhusu mkwamo wetu tunaojaribu kuuangazia na hata kutaka kuwalaumu nao wasiohusika:
Hii ni moja ya zile za kuruka ruka nilizosema. Niijibu hii kwa ufupi kwa reference. Ikikupendeza soma angalau:
Post #61, 63, 66 na 67 kwenye uzi huu:
Nguvu ya Umma Senegal, funzo jingine kwetu
Baada ya posts hizo 4 soma pia post #1 ikikupendeza.
Uwajibikaji huo umeelezwa bayana.
Ikikupendeza tafadhali kwani ninajua si joni, Paskali au wenzao atatokea hapa kutia neno.
Niliwahi kusema tunalazimika kuyaandika haya waziwazi vigezo na masharti yote yakizingatiwa katikati ya fisi na mamba wenye uchu na njaa kali.
Ni hayo tu ndugu mjumbe.
.
Kwani Kila kitu kilipanda bei? Mbona Sukari,mabati,nguo nk havikupabda bei?Acha porojo. Kuna utopolo mmoja alidai kila kitu kitapanda bei. Hiyo ni kabla ya vita ya Ukraine. Vilivyokuja kupanda kabla ya hiyo vita, baadae ikawa kisingizio kuwa vita ndio imepandisha bei ya kila kitu. Serikali dhaifu, hushirikiana na wafanyabiashara kuumiza wananchi. Mfano tu bando za makampuni ya simu.
Sijui unazungumza nini, ila "serikali dhaifu hushirikiana na wafanyabiashara kuumiza Raia". Iko hivyo.Kwani Kila kitu kilipanda bei? Mbona Sukari,mabati,nguo nk havikupabda bei?
Kwahyo unataka bei elekezi ya unga wa ugali? ..siurudi kjjn kwako ukalime mahindi,Kumbe kwa nini kuna Bei elekezi kwenye sekta zingine kama mabasi, vituo vya mafuta nk?
Au una maana saaa kila mtu na lake? Kwamba huafiki nauli ya bus kanunue lako? Huafiki bei ya mafuta petrol station kafungue yako?
Mkuu waache walale usingizi wakiamka itakuwa kumekucha. Watanzania tunafunzwa siasa mashuleni/vyuoni kama somo la lazima na huenda athari ya hilo ni haya tunayoshuhudia sasa. Tumekuwa watu wa maneno mengi vitendo hakuna.Hauko sahihi ndugu.
Maandamano yanataka hamasa na organization ya kutosha. Ni jukumu la watu kufanikisha hayo. Hayawezi kuja kama mvua.
Ulichoandika ni visingizio vya kawaida vya viongozi dhaifu wenye kuvitumia vyama zaidi kama fursa za kimapato yao binafsi. Zingatia viongozi hawa wanalipwa.
Kenya bila Raila, hakuna hamasa wala maandamano tunayoyaona sasa.
Raila kaitisha maandamano yakawepo. Alipoitisha kusitishwa yakasimama. Kenya hawajaandamana Kwa sababu tu ya sababu zilizotolewa.
Kama maandamano yalikuwa ni kwa sababu zilizotolewa tu, mbona hayakuanza bila Raila au bila kuyaitisha au hayakuendelea bila yeye baada ya yeye kuyasitisha?
La msingi tufahamu Kenya wamehamasishwa na wako organized vilivyo. Hiyo haikutokea kwao kama ajali na haitatokea kwetu kama ajali.
Hayupo anayemlenga chadema, viko vyama vingi ikiwamo wao. Aliyeshindwa kuwa organize na kuwahasisha watu hata akathubutu kutamka kukosa uungwaji mkono angali vipi ofisini leo?
Kwa nini utaratibu wa kupata viongozi kwenye vyama hivi across the board usiwe huru, haki na kidemokrasia kupitia primaries za wazi kama ilivyo kwake beberu? Watu wakagombea Kwa kuzingatia agenda na malengo yetu ya ukombozi na wakapimwa kwa outputs zao?
Watu wenye uwezo wa kuendesha kwa ufanisi kwenye malengo yetu wapo wengi.
Kwanini tusiwape nafasi hizo walio tayari tuone matokeo?
Zingatia Liz Truss alikaa ofisini Kwa siku 45 Kwa kutokukidhi matarajio.
Tupateje viongozi wasiofika vigezo vyetu Kwa utaratibu huu.
Ya nini kuliita koleo kuwa ni kijiko kikubwa?
Mawazo kama yenu mkuu yanaturudisha nyuma sana.
Cc: Zawadini
Anashindwa kuhusianisha utawala na maisha ya watawaliwaMkuu JF kuna majukwaa mengi. Hili linaweza kuwa siyo size yako.
Ni ushauri tu. Siyo (nothing) personal.
Sitaki bei elekezi kwenye lolote na wewe kafungue kituo chako cha mafuta, kanunue basi au dala dala lako nk shida iko wapi?Kwahyo unataka bei elekezi ya unga wa ugali? ..siurudi kjjn kwako ukalime mahindi,
Mengi unayoandika naona hayaendani na kile ninachokisimamia, mimi pointi yangu hapa ni moja tu, watanzania ni waoga.
Hata mifano unayotoa naona haiendani na hiki nachozungumzia, kwa mfano unawazungumzia wale waliojitokeza kumpokea Lissu uwanja wa ndege kama ndio waandamanaji walijitokeza, huu mfano wako sio sahihi.
Kwasababu ile shughuli ya kwenda kumpokea Lissu haikukutana na kikwazo chochote, hapakuwepo na vitisho vyovyote toka kwa jeshi la polisi tofauti na kwenye maandamano mengine, kwanza shughuli yenyewe ilikuwa ni kumpokea, kisha "maandamano" yakafuata baadae kama kumsindikiza, kwangu ile ilikuwa ni kama sherehe tu.
Nikuulize, hivi wakati ule Chadema wakiitisha maandamano na kina Mambosasa wakisema watakaojitokeza watavunjwa miguu, uliwahi kuwaona watu wakijitokeza? hii ni tofauti kabisa na Kenya unapotolea mfano, wakenya hawako kama sisi.
- Nimeona mahala Mdude anasema patakuwepo na maandamano ya amani kutaka waliohusika kwenye upotevu wa pesa ripoti ya CAG wachukuliwe hatua.
Ngoja tuone kama patakuwepo na vitisho toka kwa jeshi la polisi na reaction ya waandamanaji itakuwaje, japo inawezekana wakaruhusiwa kuandamana bila vitisho sababu awamu hii ya Samia haijawa na vitisho.
Mambo mengine unayozungumzia naona hizo ni fikra zako tu, mimi siungi mkono kina Mdee kurudishwa Chadema kwa sababu yoyote, na hata ule mfano niliotoa kwa baadhi ya watu kusema bora kina Mbowe walambe asali sababu watz ni wajinga na waoga, huo ni mtazamo wao niliokuandikia, sio wangu.
Mkuu waache walale usingizi wakiamka itakuwa kumekucha. Watanzania tunafunzwa siasa mashuleni/vyuoni kama somo la lazima na huenda athari ya hilo ni haya tunayoshuhudia sasa. Tumekuwa watu wa maneno mengi vitendo hakuna.