Kufuatia maandamano ya kizalendo Kenya, serikali ya huko, imeamua kushusha bei za vyakula.
View attachment 2588177
Upinzani unataka bei ya unga kwa kilo isizidi 2,000/- za kitanzania, vinginevyo wanarudi Tahrir.
Unga prices to drop from next week, President Ruto pledges
Hakuna mahali popote Kenya (au kwingine) wanakodai kuwa hizi ni harakati za wajaluo au kuwa hata ni za kikabila, isipokuwa Tanzania. Maana kamili ya kuwa mtanzania ni mjuaji mno!
"Hivi pilipili usisozila zinakuwasha nini?"
Wakenya wana matatizo Yao wanayoyatambua. Kwamba ni yao na kuwa hawana mjomba wala shangazi wa kuwatatulia.
Wanajua mfumbuzi wa matatizo yao ni wao wenyewe. Hawatafuti visingizio, mchawi wala kujaribu kuyakimbia. Wanajua matatizo hukabiliwa, tena kwa vitendo si kwa maneno.
"Maneno matupu hayavunji mfupa."
Inafahamika kuwa hata huko walamba asali, wahuni na hata vijana wa hovyo wapo. Kwamba yaliyoko kwetu na kwao yapo. Hata hivyo ujasiri wa viongozi wao wenye misimamo isiyotetereka ni jambo la kupigiwa mfano sana.
Kushuka kwa bei za bidhaa muhimu Kenya ni kwa manufaa ya wakenya wote.
"Liko kama mtego wa panya wenye kunasa waliomo na wasiokuwamo."
Tunataka haki? Hatutaki tozo? Tukutane Tahrir.
Huu ndiyo ulio ukweli mchungu. Mengine yote ni manjonjo tu.