Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Baada ya safari kuelekea sehemu ambayo sikuitambua, tulifika sehemu husika na nilitambulishwa kwao laivu baada ya kufika hapo.

Moyo wangu ulijaa maumivu sana, nilitokwa na machozi, jasho lilinitoka na Katu sikuamini kwamba nimebaki peke yangu na watu ambao sijawahi kuonana nao katika maisha yangu et kwa Sabab ya mawazo mbadala.

Tulijadiliana kwa muda huku wakiwa na nyuso zenye hasira, kwa muda ule sikuwa na jambo ambalo ningeweza kulifanya.

Baada ya mazungumzo yalioegemea upande mmoja nilipitia kipindi kifupi ambacho ninakirudia rudia kama vile nafungua ukurasa wa kitabu.

Kwa mbali niliona Giza Nene likija upande wangu na nikaanza kutafakari mambo kadhaa kwa haraka ninini nimekifanya kibaya? Ukweli ambao unasemwa? Ooooh nchi yangu Tanz.

Niliwaza kuhusu familia yangu,ndugu jamaa na marafiki, watakumbuka chochote kutoka kwangu ooooooh yes japo nafumba macho kwa Mara ya mwisho Ila sikuishi bure katika sayari hio.

Sikugeuzwa zwazwa na kishangilia elfu saba ili kulinda maslahi ya kikundi fulani

Nimeacha mbegu bora, kujiamini na kusimamia haki.
Mti unakatika Ila kuna matawi yanachipua.
Nikasema kimoyomoyo mbegu hii iishi milele vizazi na vizazi.

Baadae nilijiona nikiwa huru kabisa wale watu waovu na wadhalimu,walifanikiwa kutimiza lengo lao na nikatenganishwa........kivuli kikabak

Nilipotizama chini pale nilikuwa nimelazwa nilijaribu kupaza sauti lakin hawakunisikia.nilipiga kelele sana sikusikiwa

Nikashuhudia wakinipeleka sehemu ambayo si muhimu sana kuielezea kwa sasa nami nikawafuata kwa spidi sana na nikiendelea kuwazuia Ila sikuweza kukamata sehemu yoyote ya mwili wao.

Nikajiona (((nikipotezwa)))

Nikiwa katika hali ya kutafakari watesi waliondoka huku wakicheka na kufurahi kutimiza udhalimu ule bila kujua kuwa niliwafuata kwa nyuma yao wote kwa pamoja na kwa muda mmoja japokuwa walikuwa wakiishi maeneo tofauti na walielekea sehemu tofauti.

Niliporudi nyumbani kutoa taarifa nilishangaa kuwa naingia bila kufunguliwa,nikaketi sebuleni,nikasalimia Ila sikuitikiwa,..,..,.., nikaomba maji ya kunywa sikusikiwa....nikapiga kelele kubwa glasi iliokuwa mezani ikadondoka.... cha ajabu wakaulizana Leo mbona upepo mkali hivi hadi unaangusha vyombo......hapo ndipo nilipogundua (am not the same as always).

Nikatafakari sanaaa sanaaa muda ukapita kama upitavyo
Nikaona harakati za kunitafuta zikipamba moto na kila nikiwaambia i am here hawajibu kitu(hawasikii)

Wengine wakakana kabisa kunisikia,wengine wakabeza sana,wengine wakajisahaulisha kwa namna walivobeza kwenye mitandao.

Nami nikajiapiza kuwa sitoiacha sayari hii na kwenda zangu kwa amani mpaka pale ambapo watesi wangu ntaondoka nao, hawatolala kwa amani sikuzote za maisha yao kwa sababu damu ile walioimwaga kila nikiiangalia baaaado haijakauka.

Marafiki zangu wengi wakawa wanapita wakielekea ndani ya malango ya amani.....nawasimamisha tunapige stories za sayari ile kabla hawajaingia

Wanauliza mbona nipo nje pekeyangu? wananisihi B.. Samehe tu ebu ingia ndani kuna maisha mengine huku, siwajibu kitu chochote....huwa ninawaza tu ......muda utakapofika nitakaposhusha hasira zangu zote kwa watesi wangu na kushuhudia wakilia na kusaga meno ndipo nitakapoiacha sayari hio na kuingia kwenye malango ya amani nikapumzike.

NB: ni fikra tu za usiku kabla sijalala.
 
Ben, una uhakika gani kuwa huyo aliyekutishia ni mtu kutoka serikalini? Isije ikawa umechezewa tu na vijana wa mtandaoni nawe umekimbilia huku kutafuta kiki. Nijuavyo mimi hakuna hit man mjinga aandike vitisho hivyo na namba ya simu juu. Na wewe una umuhimu au impact gani mpaka utake kuuawa wazi wazi namna hii? Hakuna logic katika hili na naamini ni katika juhudi za kutafuta kiki tu kwa sababu mmekosa mahali pa kutokea.

Anyway jipe moyo shujaa wa Rombo na daima kumbuka kuwa ili chuma kiwe imara ni lazima kipite kwenye fukuto. You will be OK na huko mbele utakuwa mpinzani aliyekomaa. Good luck!
Vipi ameshatafuta Kiki? Usitoe hukumu alikuwa anatoa maelezo jinsi anavyotafutwa leo mmeshampoteza.
 
Ningepata hata ak 47 mimi...


Nitakuja kuwa muasi kwenye nchi yangu mimi...

Huu mstari kwenye hii poem naupenda sana sijui kwanini mimi...

Mother," shouts the boy,
"When I grow up
I will carry a gun
And not a pen."
"My son," shouts the mother,
"My son," cries the mother
"You will never live to carry a gun
There is no meat for us."


R.I.P Kamanda Ben
 
Back
Top Bottom