Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Kwa hili namtete mzee wangu huyu huwa anadondosha like za bure mpka tunashindwa kujua ameLIKE kweli au ni ile SEEN.
 
Ila hii post haijaanzishwa nawewe,sasa kipi kilikuvutia katika ile koment mpaka uka like
 
Nimejifunza kitu kwenye bandiko laako hili maana JF imegeuzwa kijiwe stori, uzushi na matusi mwanzo mwisho.
 
Naona ujumbe huu umefufuliwa toka ulikokuwa. Kibinadamu, inasikitisha kwamba matatizo haya yalionekana yakija kwa huyu. Sielewi ni ushujaa wa aina gani aliokuwa nao hadi kufikia hatua ya kuonesha kutojali. Naamini Ushujaa siyo kuumia au kufa bila kujali. Huo ni ushujaa wa kihayawani. Ile tunavyoona simba anakanyagwa na nyati yeye yumo hadi roho inamtoka.

Baadhi yetu pia tuliandika, eti kwani wao hawatakufa? Yote haya ambayo Ben alikuwa akiandika ni msukumo wa kisiasa lakini, siamini kama siasa ni kazi muhimu kiasi hicho! Hata kama unajenga magorofa kwa kazi hiyo. Mbona tumneambiwa kuna corona tukageuza mtindo wa maisha. Mbona waalimu waliacha kwenda mashuleni? Au Ualimu haulipi kama siasa? Mbona kuna nchi wamekaa lockdown hadi kupewa msaada wa chakula? Kuna mipaka ya kujiita shujaa, ikizidi ni uhayawani!
 
Hivi ndugu yetu ndiyo basi tena, ndiyo tumemsahau kabisa
 
Ni kweli mkuu wewe Pasko tunakufahamu vizuri, hata tusipokubaliana una like.
Ni kama mwalimu ambaye ana acknowledge kuwa amesoma daftari(post)
 
Hakuna Jambo limewabadili Mtazamo watanzania Kama hili na la lisu. Halafu mtu anahama chadema anaenda kule kwa watekaji dah aiseee
Nakumbuka siku walipotaka kumdedisha Lissu, huyo Lowassa, Sumaye, Waitara nk, walionyesha sura za huzuni sana! Sikutegemea kama hao, na wengine waliokuwa upande huo, wangeungana na hao WAUAJI!
 
Sidhani kama Ben amefariki,maana kuna siku nadhani mwezi wa kwanza au wa pili mwaka huu alichangia mada kwa ID yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…