Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Kazi yenu mmekamilisha salama,kabla na nyie hamjamalizika, familia ipatiwe mabaki nao wayahifadhi.
 
Mwili wa Ben Saanane mliutupa wapi?
 
Inatisha sana Mkuu. Hii tabia ya kuingiza makada wasio na sifa yoyote katika taasisi hizo imeleta balaa kubwa nchini la watu kuchukua uhai wa Watanzania wenzao kama vile wanaua panya. Hawana woga kabisa wala hawasikii vibaya.
Watu wenye roho za namna hii ndiyo wamejazana huko kwenye vyombo vya dola. Tanzania kama nchi tumefika sehemu mbaya sana. Aina hii ya uzalendo kwangu kwangu HAPANA, ni tabia ya kishenzi sana.
 
For the first time nimesoma uzi nikatokwa chozi hapa JamiiForums. 😭

Ben Saanane Mungu awe pamoja nawe popote ulipo.
Nami nililia sana one na kuapa kutomsamehe mhusika pamoja naye jiwe. Lakini nimewasamehe na msamaha nimeutoa katikati ya ibada kwa kigugumizi.

Baada ya tafakari kubwa niliona ni waliomuua Mawazo, waliomteka Saanane na wengine ma waliompiga Lissu risasi ndio wanastahili Msamaha wangu mwaka huu. Maana ni watu walioiumiza zaidi nafsi yangu.

Kama wapo waliokufa, Mungu awasamehe, kama wapo walio hai Mungu awasamehe na KUWAKUMBUSHA kuwa nao ni viumbe dhaifu tu.
 
Daaaaah so sad
 
hakuna jiwe litasalia juu ya jiwe, kila kitu kitawekwa hadharani, time will tell.
Katika siku 100 ambazo wengine tulimpa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan toka aapishwe Machi 19, siku 75 (sawa na robo tatu) tayari zimekatika huku kitendawili cha kikosi cha wasiojulikana kikiwa bado hakijateguliwa.

Chonde chonde mama, siku zayoyoma na tunasubiri hatua madhubuti zichukuliwe ili kukibaini hicho kikosi cha watekaji, watesaji na wauaji kilichotuweka roho juu kwa miaka mitano. RIP Ben Saanane!

Katika kipindi hicho Watanzania tulihuzunika na tulilia hadi machozi yakatukauka tukiwakumbuka ndugu zetu, rafiki zetu na jirani zetu tuliowapoteza katika hiyo miaka mitano ya mateso.
 
kuna siku ipo tu aliyefanya unyama huu atahukumiwa kama sio hapa duniani bali na Mungu. inaumiza sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…