Mbaya zaidi hao anaowapigania wala hakuna hata mmoja anayemsaidia, wao wapo busy, usiku wanalala na wake zao yeye Mdude ananyea debe.
Mwenyezi Mungu alitupendelea sana binadamu kwani, tofauti na wanyama wa porini, alitupa akili. Hata hivyo tatizo letu kubwa likatokana na uhuru aliotupa wa namna tunavyotumia akili hizo na maamuzi tunayochukua.
Mathalani tunaweza kuamua bora maisha kama wanyama wa porini bila kufikiria namna ya kuboresha maisha tunavyoishi. Lakini pia tunaweza kutumia hizo akili kujipa maisha bora au kwa lugha rasmi kujipa maendeleo.
Changamoto tulizokuwa nazo binadamu toka tunaumbwa ni nyingi lakini pia silaha ya kukabiliana nazo tukajaaliwa, akili. Kwa akili tunapaa angani kama ndege, tunasafiri majini kama samaki na hakuna kiumbe kinatutisha.
Kwa kuwa sote tuna akili, uhasama baina yetu unatokana na utofauti katika maamuzi yetu kimaendeleo. Mashindano ya hatari yanayovikabili viumbe vyote ulimwenguni yako baina yetu sisi kwa sisi...binadamu kwa binadamu.
Wako wasema ukweli na waongo, wapo majasiri na waoga, wapo wenye msimamo na wanafiki, wapo wanaotumia akili na wapo waliozipa akili zao likizo na mwisho wapo wanaoteseka juani ili wavivu wa akili wale kivulini!
Wapo walioteseka na kupoteza maisha ili wenzao wawe huru, wapate haki na usawa na wapo wanaoshangaa Mdude kunyea debe na kujilisha upepo bila wa kumsaidia huku
Son of Gamba yuko busy, usiku analala na mke wake!
Asanteni sana...Baba wa Taifa, Nelson Mandela, Martin Luther King na wengineo...
all you ever wanted was for the world to be a better place to live!
Asanteni mliohangaika na wengine kupoteza maisha kugundua ndege, kugundua dawa, kugundua simu hadi ya mkononi...