Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Nikisoma ujumbe huu wa Ben, machozi yananilenga. but naomba kokote alipo huyu kijana awe yu hai.... ninaamini kwa hili siko peke yangu humu.

ndiyo maana wengi wetu kwa kiasi kikubwa we have taken solace tuliposikia EN yamemfika yaliyomfika. it's not that we are being heartless or anything but kwa kilichowakuta kina Ben, Lissu, nk - kama ni kuitwa heartless then be it!
 
Demokrasia ni kama kitendo cha wanaume watano kugombania mwanamke mmoja. haiwezekani wote tunapigania kuwa na huyu mwanamke halafu mimi kama mshindani nikusifie wewe ili umpate, lazma nikuponde. ndo demokrasia ilivyo, lazma criticism iwepo, lazma uchunguze udhaifu wa mwenzako na uexpose kwa jamii ili uvute wanajamii upande wako.
 
Kuna wataalamu wabobevu humu ndani mwanzoni kabisa waliandika ati kwa ujuzi walionao mafundi wa kuua watu hawawezi kutoa vitisho vya nmna ile. Eti huyu mtu anatafuta kiki. Mungu jaaliwa hawa wote nao wajumuishwe katika orodha ya wauwaji siku ya hukumu
 
Kama si mtu wa Serikalini Mkuu kwanini Serikali haikuchunguza ili hali namba ya simu aliiweka wazi?

Ben, una uhakika gani kuwa huyo aliyekutishia ni mtu kutoka serikalini? Isije ikawa umechezewa tu na vijana wa mtandaoni nawe umekimbilia huku kutafuta kiki. Nijuavyo mimi hakuna hitman mjinga aandike vitisho hivyo na namba ya simu juu. Na wewe una umuhimu au impact gani mpaka utake kuuawa wazi wazi namna hii?

Anyway jipe moyo shujaa wa Rombo na daima kumbuka kuwa ili chuma kiwe imara ni lazima kipite kwenye fukuto. You will be OK na huko mbele utakuwa mpinzani aliyekomaa. Siasa zina gharama. Good luck!
 
MWENYEZI MUNGU awalipe wabaya wako wote walioshiriki kuutenda ubaya huu sawa sawa na ubaya wao [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Ben! It was too early for you to disappear [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
LOoo, jameni, mbona hii mada huwa inajitokeza hapa mara kwa mara, kama kumbukumbu ya kutonesha 'donda ndugu'?

Si bora ingewekwa iwe ya kudumu (zilizogandishwa kama hizo nyingine hapo kwenye ukurasa huu huu!)
 
Back
Top Bottom