Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

Ben Saanane: Ninatishwa kuuawa kwa kuikosoa Serikali

HUYU JAMAA ALIMMALIZA KWA BASTOLA YAKE MWENYEWE .....WASAIDIZI WAKALETA BODY BAG ...WAKAENDA KUMWAGIA ACIDI KAMA LUMUMBA ...KUNA SIMULIZI NYINGI NA ZA KUTISHA ........
Nina video moja akikabidhiwa pistol na kijana wake nashindwa jinsi ya kuipandisha hapa,namna alivyokuwa anaichekecha anaonekana ni mkongwe kabisa kwenye mambo hayo kuitumia etc.
 
Kuna watu wanakuwa mbele kanisani afu lazima wapewe mix wamwage neno..wanafiki watakuwa Kuni za moto huko mbele ya safari
 
Itahitajija tume ya ukweli na maridhiano ,kuweza kupatanisha mambo yooote yaliyofanyika ndani ya miaka sita takribani , hiyo ndio "Bei" ya katiba mpya .....aliyotuasa Nyerere kuwa tunahitaji ili kuzuia asije kuingia mtu mbaya akaitumia vibaya ....
Uzuri sasa kila mmoja ameona na hataki tena mtu wa aina hiyo hata afikiriwe na chama chochote kugombea Urais .
Pengine issue ya katiba inarudi kwa kasi , tume ya uchaguzi na pengine uchaguzi unarudiwa

Nadhani hadi mtendaji mkuu wa hayo mambo akate moto ndio michakato mingine itaendelea. Au kuna lolote mkuu hujaliweka wazi?
 
Safari inaendelea. Vitisho. Haya ndiyo maisha yetu ya Kila siku. Mengine tumetoa Ripoti Polisi huko

Kuna watu hawa miongoni mwa wengi. Yeye anaandika "Ben Saanane unachokitafuta ndani ya Serikali hii utakipata. Kwa elimu na uwezo wako hatukutarajia ungefikia hatua ya ajabu kwa namna uliyofikia.

Hujiulizi kwanini upo huru hadi muda huu You are too young to die. Tunajua utaandika na hili. Andika lakini the next post hutaandika ukiwa na uhuru wa kutosha. Andika but your days are numbered. Unajua kuna rafiki yako alipuuza na hutaki kuandika kuhusu yeye labda kwa kuwa alitangulia. Andika Ben. Andika sana, ongea. Sema lakini utajikuta mwenyewe na chatu"

He's such a coward. Muoga. Muaji anayejitangaza nae ana hofu tupu

Nimemshukuru lakini nimemjibu kwa namba yake hii 0768797982 ambayo ipo polisi.

Haya tunasonga mbele Watanzania. Kama ni Uchochezi sidhani kama upo uchochezi mkubwa zaidi ya huu.

As long as tupo hai, Sauti zetu hazitakoma. Tutaandika, Tutasema, Tutahutubia na tutafanya vitendo

Kitu kimoja tu cha hakika ni kuwa Damu ikimwagika hasa damu ya kimapinduzi hutoa mvuke utakaonyesha na kutiririsha mafuriko katikati ya mito na vijito vya haki. Kama itanyesha mvua ya Radi basi itaambatana na mwanga na cheche zitakazowamulika walaghai, watesaji, wakandamizaji wa hakiWatetezi wa haki watapata mwanga katikati ya giza tororo la Unyanyasaji, unafiki na ubakaji wa taaluma na dhamiri zao kitaaluma na kiimani.

Yesu Kristu aliishi miaka 33 tu duniania. Nina Mwaka Mmoja bado. He fought the right cause. Alikuja Duniani kimungu. Kila mtu anaishi kutokana na makusudi ya Mungu. Mwenyezi Mungu huruhusu kila jambo kwa makusudi yake. Sisi ni akina nani tukatae makusudi yake? Hatukujileta Duniani na hatutaishi milele.

Wasichojua watu hawa ni kuwa nilizaliwa na kubatizwa hatari siku hiyohiyo kama Mkatoliki. Ubatizo wa kifo(Hatari) 13 Desemba miaka hiyo, nikapona kwa fadhila zake Muumba. Nimepata fadhila sana Machoni pa Mwenyezi Mungu hadi muda huu. Wanajisumbua! Nimeishi beyond that favour

Oh nakupenda mpenzi wangu Tanzania. I love you more than words can wield the matter, dearer than eyesight, space and Liberty. Oh I love you Tanzania. My Pride, My fountain of inspiration."

Mlale salama marafiki zangu wapendwa.

Mapambano na Yaendelee, Ushindi U Dhahiiri (Aluta Continua, Victory Ascerta)

Pumzika kwa amani Rafiki yangu kipenzi Alphonce Mawazo. Hukukopa, Ulijiandaa kulipa gharama. Ukalipa Deni. Tunasonga Mbele! Nitalitaka Jeshi la Polisi liunganishe ujumbe uliotumwa na kifo chako katika hatua za uchunguzi.

Ben Saanane
Inatoa machozi kijana wa miaka 33 kuuwawa kwaajili ya kusema kweli. Mungu atalipia damu yako hapahapa duniani. Damu yako haitamwagika bure..
 
Ben acha huu upotoshaji kama unajiita wewe kidume basi endelea ila mimi ni shahidi ndani ya mtandao huu umeshaonywa sana.
Ila mimi nataka kukutabiria jambo. Kama kweli hutobadilika nakuendelea na hii mambo basi kifo chako hutopata nafasi kuja kuandika humu na kwa bahati mbaya watu watakuwa wameshasahau sana sana watajuwa umekufa kama binadam wengine ila kumbuka huna uharakati wowote my dia hata punje ya Dr Ulimboka huna sasa jiangalie usitafute umaarufu wakati kifaru kiponjiani unakizuia kisipite kwa mwili wa nyama utakufa na hao unao walaani wala haiwapati... Take care this is a nation kaa mbali
Mlipomuua mmefaidi nn sasa? We ukifa utasahaulika lakini hebu ona Ben hajasahaulika bado watu wanapigania haki yake na wataipigania milele hadi ipatikane. We siku ukifa the moment wamemaliza kukufukia utasahaulika kabisa
 
Mlipomuua mmefaidi nn sasa? We ukifa utasahaulika lakini hebu ona Ben hajasahaulika bado watu wanapigania haki yake na wataipigania milele hadi ipatikane. We siku ukifa the moment wamemaliza kukufukia utasahaulika kabisa
Ametumbuliwa siku hizi anayo akili
 
Mitandao ina umuhimu sana,, Ben aliweka bandiko humu na maadui zake kama TumainiEl walimjibu hadharani.

Yakaja kutokea ukweli..

Tuache kupuuza wanayosema watu, SO sad
 
HUYU JAMAA ALIMMALIZA KWA BASTOLA YAKE MWENYEWE .....WASAIDIZI WAKALETA BODY BAG ...WAKAENDA KUMWAGIA ACIDI KAMA LUMUMBA ...KUNA SIMULIZI NYINGI NA ZA KUTISHA ........
Kuhusu “simulizi nyingi za Lumumba”, ni kweli kabisa. Hata kuna mmojawapo humu alisema kuwa alitupwa kwenye nyumba/Banda la chatu. Kuna simulizi nyingi sana za kutisha kutoka kwa wana Lumumba. Hata Mwigulu alimuaminisha jamaa kuwa yeye ni best yake kabisa.🤦🏾‍♂️
 
Naona unajitekenya Mwenyewe MKUU......hivi ni SERIKALI GANI DUNIANI inaweza fanya assasination like you have claimed above? Ebu ficha ujinga wako na ACHA KUTAFTA KIKI ZA KIPUUUZI....who are you by the way? Kama ungekuwa una cha maana cha kuleta kwenye nchii hii chama chako kisinge kutupa CHOONI kwenye uchaguzi wa kupata nafasi za UBUNGE.

Ebu tuambie ni lipi la maana mpaka sasa ushalisema mpka kufikia kutishiwa na SERIKALI? SERIKALI HUWA HAITISHI.......ebu acha kutuona sisi mapoyoyo afu TAMBUA KUANZIA LEO HIYO YA KUFANYA ASSASINATION IPO HUKO KWENU......afu hakuna CHAMA NDANI ya nchi hii ni mafundi wa kutengeneza propaganda za UWONGO hiki CHAMA..sasa naona mpka wanachama nao wameambukizwa KILA SIKU KUSEMA UWONGO KUTAFTA KIKI NA HURUMA ZA WANANCHI.
Ongeza sauti mkuu
 
Back
Top Bottom