Benaco Ngara: Madereva wa Malori wa Tanzania, wamejichukulia sheria mkononi kuzuia Malori yote kutokea Rwanda kuingia nchini

Benaco Ngara: Madereva wa Malori wa Tanzania, wamejichukulia sheria mkononi kuzuia Malori yote kutokea Rwanda kuingia nchini

binafsi nilijua tutafika huku,sababu ya maamuzi ya kijinga.

sikutegemea mr slim angekuwa mpuuzi kiasi kile,labda maamuzi yake yaliambatana na chuki,wifu na roho mbaya tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kunyanyasika vilivyo nchini Rwanda madereva wa malori wa Tanzania wamejichukulia sheria mkononi kuyazuia malori yote kutokea Rwanda kuingia nchini.

Inasemekana baada ya Rwanda kuudhibiti ugonjwa wa Corona vilivyo nchini mwao, kitisho pekee kwa sasa kimebakia kuwa kutokea kwa wageni wanaoingia nchini mwao.

Katika hili inasemekana madereva wa malori kutokea nje wamekuwa ndiyo kitisho kikubwa. Takwimu zinaonyesha kuwa madereva kadhaa tokea Tanzania wamepatikana na virusi hivyo kwenye kuingia huko. Kutokana na hali hiyo, inasemekana Rwanda imebadilisha utaratibu wa malori kuingiza mizigo na sasa kuwataka madereva wa kutoka nje (Tanzania) kuishia mpakani. Utaratibu mpya unawataka madereva walioko (salama) ndani ya Rwanda pekee kuyafikisha malori Kigali na kuwarudishia mpakani.

Utaratibu wa ajabu kabisa. Nani atamwamini mtu asiyemjua na gari lake? Kujibu hilo madereva wa Tanzania nao wamechukua hatua zao na kuanzia jana inasemekana hali huko ni tete. Hakuna lori kutoka Rwanda wanaloliruhusu kuingia nchini. Vinginevyo nao wanawataka waishie mpakani kwa hali ile ile kama inavyotakiwa kwa wetu kufanya.

My take: Serikali inabidi kuingilia kati haraka iwezekanavyo na kuchukua hatua. Yawezekana hawa ndugu tuliowaachia mpaka wazi kwa kuwahurumia ya kwamba watataabika mno, huruma yetu hawaihitaji kabisa!

Kudos madereva wetu si mbaya mkuki kwa nguruwe kuwa ni ule ule kwa binadamu pia.

View attachment 1440070
Hali ndiyo kama hii


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule jamaa si yupo karbu aende kwa miguu tu apo mpakani..si hajari ata ivyo[emoji28][emoji28][emoji28][emoji23][emoji23]
 
Mamlaka husika iingilie kati haraka iwezekanavyo kutatua suala hili kiustaarabu.

Isifikie hatua ya kuwekeana visasi.

Maana baadae mambo yakishatulia (Maisha baada ya gonjwa hili la mlipuko) isije ikawawekea wakati mgumu Ndugu zetu wanaoenda huko Rwanda, au Ndugu zetu wanaoishi huko Rwanda
 
Kitaagizwa kikosi kazi hapo kucharaza viboko watanzania na magari yaruhusiwe kuingia tz.
Hilo sitoshangaa kabisaa, lakini hivi tujiulize kama madereva wa Tz Wana Corona na hawaruhusiwi kuingia nchini Rwanda kwanini hawa madereva wa Rwanda waje huku kwetu, hawajui kwamba wanakuja kuichukua hiyo corona kuipeleka kwao.
 
Mamlaka husika iingilie kati haraka iwezekanavyo kutatua suala hili kiustaarabu.

Isifikie hatua ya kuwekeana visasi.

Maana baadae mambo yakishatulia (Maisha baada ya gonjwa hili la mlipuko) isije ikawawekea wakati mgumu Ndugu zetu wanaoenda huko Rwanda, au Ndugu zetu wanaoishi huko Rwanda
Yaaani watuwekee sisi visasi!! Sawa waweke tu hakuna tatizo kama raia wao huku ndio wengi zaidi.
 
Bandari ya mombasa itafanya kazi saana.

Ujinga ni mzigo unaoelemea mno. Mbaya zaidi mzigo huo ubebwe na mpumbavu, hata akiingia ndani ya chombo cha usafiri yeye ataendelea kujitwika limzigo lake.
 
warwanda wajiulize kwanza nani anamtegemea kati ya tanzania na rwanda nani anahitaji malori kuingia nchini mwake
nani mwenye bandari hapo 🤣 🤣 🤣

Aliimba mwungwana mmoja: "tuwasifu madereva wetu Tanzania ...."
 
Back
Top Bottom