ChangeTZ
Member
- Nov 13, 2018
- 52
- 129
LAZIMA tujue kuwa anguko la CHADEMA mwaka huu ni la kihistoria. Haijawahi kutokea tangu kuanza kwa Mfumo wa Vyama vingi mwaka 1992. Labda kwa wasiofahamu dhambi ya kumkataa Jasusi au Kachero (Membe) kwenye Chama hicho ndio mwanzo wa kujiangusha wenyewe. Membe hakuridhika kukataliwa na CHADEMA akaamua kwenda ACT - Wazalendo ili iwe route ya kuwavuruga wote wawili.
Ubaya ulianzia wapi?
Baada tu ya mazungumzo na Viongozi waandamizi wa CHADEMA na Membe kutokubaliana kwa kuwa Membe alionesha kuwa anakwenda kwenye Chama na CASH za kutosha lakini Viongozi hao waliona ni bora aliyepigwa risasi (Lissu) kwa kuwa wananchi watamuonea huruma.
Alichofanya Membe baada ya kutemwa CHADEMA
Kwa kuwa Membe alikosa njia ya kuingia na kuibomoa CHADEMA aliamua kujiunga na ACT Wazalendo ili kuwapasua vizuri wote wawili kwa pamoja na lengo la kwanza likatimia.
CHADEMA na ACT Wazalendo walijikanyaga wapi?
Siku ambayo Mgombea wa Urais wa CHADEMA Lissu alipoenda kwenye Mkutano Mkuu wa ACT Wazalendo na kuhutubia kama vile ndio mgombea wa ACT Wazalendo pale ndipo alipovuruga atmosphere bila wao kujua. Hapo Membe alikuwa anawasoma tu nyumbu wanavyojikanyaga. Na, baada ya Mgombea wa Urais Zanzibar Maalim Seif na Zitto Kabwe kutangaza kumuunga mkono Lissu kwenye Urais, hapo ndipo Membe akaona mikakati yake inakwenda sawa akaamua kujitokeza na kuwaambia Watanzania kwamba yeye ndiye mgombea halali wa Urais ACT Wazalendo. Hapo tunaona namna alivyowachanganya Mazezeta ya ACT na CHADEMA. Hii inaitwa akili Kubwa.
Na, Maalim Seif akaanza kujikanyaga na yeye kujibu alafu sasa na akili ya uzee akasema kuwa wao walikubaliana wote kwenye Kikao wamuunge mkono Lissu. Haya yote walikuwa wakiyafanya bila kujua lengo la Membe ni kuwachanganya Wanachama wa Vyama vyao. Hili ndio lile bao la dakika 89 alilokuwa akilizungumzia.
Mwisho wa siku Wanachama wakaone isiwe tabu wakajikalia zao majumbani na hawakwenda kupiga kura na matokeo yake ndo haya CHADEMA na ACT wameangukia pua.
Mwisho.