Benard Membe: Musiba hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu. Huko uliko naomba hela zangu

Benard Membe: Musiba hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu. Huko uliko naomba hela zangu

Musiba hana hela, kwa hiyo kwanza watafirisi mali yake kwenye kesi moja tu ya Fatma, ukiongeza na hii ya Membe ataonekana hatekelezi amri ya mahakama, hapo sasa ndio atafungwa.
wacha akanyee debe kwanza atie adabu kutukana watu hovyo.
 
Huu uzi hakuna Push gang wa kumpigania jamaa kwel?
“Niwaambie Watanzania wenzangu hakuna Mtanzania awe Ndovu au sisimizi mwenye kusimama juu ya sheria hakuna aliye juu ya sheria, ukimdhalilisha mwenzako ukadhani kwamba utaendelea kupiga miluzi na kufurahia kana kwamba wewe umefika Duniani kama Kiongozi au ndio mkubwa au Mungu Mtu, Mahakama Kuu ni jibu kwamba ukidhalilishwa fika Mahakamani uitafute haki yako nimefika hapa kwa niaba ya watanzania wote na Viongozi Wastaafu walionyanyaswa na kudhalilishwa na Mtu huyu"

"Naomba wajue hili halitotokea tena, hasimami tena kudhalilisha Wazee na Viongozi wake, hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu, hasimami tena kuwatukana Watu walioifanyia kazi Nchi hii kwa uaminifu na uadilifu wote, anasimama Mtu kwa kutumwa na kulipwa akadhani kwamba ataendelea kuishi Duniani katika hali hiyo hamtomuona tena akifanya hivyo na Musiba huko uliko naomba hela zangu"

Bernard Membe

Pia, soma=> Mahakama yaamuru Cyprian Musiba kulipa faini ya Tsh bilioni 6 kwa kumchafua Bernard Membe
 
Ina maana yote aliyosema Musiba hakuna hata la ukweli?
Kila mmoja wetu anajua kuwa kuna mantiki lakini je style ile ya kumsema mwenzako wakati mahakama zipo ni sahihi? Angempeleka mahakamani badala ya kujichukulia sheria mkononi
 
"...nimefika hapa kwa niaba ya watanzania wote na Viongozi Wastaafu walionyanyaswa na kudhalilishwa na Mtu huyu..."

there
 
Huyu alikuwa akilipwa kodi zetu milioni 60 KILA mwezi Ili awatukane watu ikiwemo wajumbe wa Mwenyezi Mungu waliomuonya boss wake asimkufuru Mwenyezi Mungu kupitia vijarida uchwara vyake vya kufungia vitumbua.Leo hawezi lipa hata mishahara watu wake.
 
Kama mnazingatia alphabet then atalipwa Anna [mama Mbona] kwanza halafu Benard and then Shangazi Fatma!

Akishindwa kulipa, pitisheni bakuri watu watachanga tumfunge jela mpaka atakapolipa!!
First inn First served. Aanze kulipwa ambaye hukumu ilianza kutoka.
 
Mzee Membe kumbuka pia kwamba deni kalifungi.
Hilo siyo Deni mkuu, mbona vijana wa Tanzania mmepagawa kiasi hicho?
Hiyo faini ya Mahakama ambayo Musiba akishindwa kulipa hadi Choo chake kitauzwa na akose pa kunyea.
Alimwona Magufuli ndo Mungu wake,sasa hayupo tena, hakuna wa kumlinda Musiba,sijui atakimbilia wapi, nadhani atajiua tu....
 
Kwenye ule msiba Musiba alilia kwa uchungu akijua kabisa kinachoenda kutokea.

Ila hizo pesa mbona nyingi mpaka zinapoteza uhalisia?...huyo bwana akidaiwa milioni hamsini tu zinatosha kumpa adabu.
Mkuu wanataka Musiba ajiue hilo ndo wamelenga baada ya kukosa kipengele cha kumhukumu kifo
 
Mdharirishaji mwingine ni "power kaaya"!

Kijana miaka 31 unamtongoza Mama mwenye miaka 60, huu ni udhalilishaji wa kijinsia!!

Nasubiri kusikia kutoka kwa Rais mwenye ngonjera ya jinsia ya kike atasemaje kuhusu Power kaaya!!
Huo siyo udhalilishaji,na hapo hakuna kesi kabisa.
Kwani kuna Sheria ya kutongoza inayoendana na umri wa watu kutongozana?
 
Back
Top Bottom