Benchika, kocha mwenye maamuzi magumu sana

Benchika, kocha mwenye maamuzi magumu sana

Ni kweli sisi simba watu kadhaa kadhaa ni makolokolo, ila nyie pale jangwani wenye akili kichwani wanajulikana kabisa.
Si bora sisi wako wawili tu wenye akili, lakini hapo umbumbumbuni wote ni Mbumbumbu pro max [emoji125][emoji23]
 
Ulitaka shabiki afanyaje? Wasionyeshe matumaini, wasiridhike na mabadiliko ya timu, Wasiende uwanjani mpaka timu ishinde kombe.

UJINGA mwingine upo madimbwini tu.
Umbumbumbu ni kipaji kinachopatikana kwa Makolokolo pekee duniani [emoji119][emoji2]
 
Mashabiki bwana? Leo sifa zote zitamwagwa!

Ajichanganye tu afungwe na bingwa la nchi ndipo moto utakapowaka 🤣🤣
Sometime piga kimnya tu kama wewe siyo mshabiki maandazi.
 
Huyu kocha leo nimemvulia kofia, kumchezesha Duchu ambaye tangu asajiliwe hakucheza mchezo wowote halafu leo unamuingiza akashikilie bomba ilikuwa jambo la hatari sana, kumuingiza kiungo Abdallah Hamis ambaye naye hakuwah kucheza hata siku moja ilikuwa ngumu kumeza, kupaki basi kuanzia dakika ya 60 ni uamuzi mgumu ambao ulitufanya wengi tushike bomba, kujaza mabeki saba nyuma haijawahi kutokea kwa muda mrefu sana, maamuzi magumu ya Benchika ambaye anafanana kwa sura na Bongo Zozo.
Hivi ni vitu vya kawaida ...kwenye Objective Football"! Utasemaje haijawahi kutokea Kwa muda mrefu..Simba iliwahi fanyahivo kule South Afrika na vigogo wa South !
 
Muda ni lesson hatari sana kwa jambo lolote lile, tuendelee kusubiri muda (Mwalimu) tujue ni mihemuko tokana na ushindi wa mechi ya Makolokolo SC vs Wydad Casablanca au ni kweli sifa anazopewa Kocha mpya.
UUnateseka kutokea pande zipi?
 
Alitaka kasi zaidi kwenye kujilinda na kushambulia kwa counter attacking japokuwa John bocco mda mwingi alikuwa off position team inapokuwa na mpira na kushindwa kuendana na kasi nadhani chilunda angeingia badala ya bocco mambo yangekuwa tofauti leo pale kwa mkapa.
Kazi za boko zilikuwa 2. Kulinda timu kwenye mipira inayopigwa cross kwenye box la Simba na kuwaondolea mabeki wa kati wa Wydad uhuru wa kupokea mipira na kusogea mbele.
 
Achana na ushindi itazame timu inavyocheza.
Mkuu, hii Game Wydad alikuwa anaondoka na goli zisizopungua 5, ni vile tu upepo haukuwa upande wao, ofkoz Simba ina mabadiliko ila sio makubwa sana.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Hongera kwake Benchika na benchi lake kwani sio makocha wengi wanaweza kujilipua kama alivyofanya yeye leo na kubwa zaidi imemlipa.

Siku hizi mpira umekuwa mchezo wa kasi sana na matumizi makubwa ya nguvu, Ndio maana Benchika aliamua kuingiza vijana wengi mwishoni kwani angewaacha mafaza zile goli zingerudi. Na huu mtego ndio Robetino alikuwa anashindwa kuufyatua mix kocha wake wa viungo. Simba walikuwa wanacheza vizuri dakika 65/70 baada ya hapo wanapoteana kutokana na pumzi na stamina ndogo halafu ikifika wakati huo Robetino alikuwa anatoa wazee halafu anaingiza wazee wengine kushika bomba matokeo yake timu ilikuwa inashindwa kuhimili vishindo.

Na mbaya zaidi yeye na benchi lake walikuwa wamekariri baadhi ya wachezaji halafu muoga wa kujaribu wachezaji wengine zaidi ya wale waliowakariri. Na bora aliondoka maana angeendelea kuwepo Simba ingewaacha hao wakina Duchu, Mwenda, na wengineo halafu ingesajili tena wachezaji wenye uwezo kama hao kwa kifupi kabisa Robetino na benchi lake walikuwa wanaenda kuwapoteza mazima hao vijana.
 
Muda ni lesson hatari sana kwa jambo lolote lile, tuendelee kusubiri muda (Mwalimu) tujue ni mihemuko tokana na ushindi wa mechi ya Makolokolo SC vs Wydad Casablanca au ni kweli sifa anazopewa Kocha mpya.
Ni kama roho inauma hivi....hebu kunywa maji mengi upunguze na UTI
 
Back
Top Bottom