Bendera ya Israel ndani ya magari ya Dar ni siasa tu au kuna la zaidi?

Bendera ya Israel ndani ya magari ya Dar ni siasa tu au kuna la zaidi?

Hili ni swala la kiimani zaidi. Sipendi kuingilia au kukosoa imani ya mtu maana hiyo ni kati yake na Mungu wake.Ukizingatia hizi dini ni za kuletewa,tungetawaliwa na wachina au wahindi si ajabu tungekua ma monk,Hindhu,Singh nk. Tuheshimiane kadili ya imani zetu
 
-Period..kama ni mkristo haya maneno utayakuta kwenye Biblia hata mtu ungewaita eti wanadharau wanajisikia,mara ni wabaguzi haisaidii nani sio mbaguzi??nani hajisikii?? nani hana dharau??tuanzie hapo.Wala tusiwasingizie hapa kwetu vipi hakuna hayo??mara'' aaah hawa tutafanya makosa makosa yote lakini si kuwapa ikulu''hiyo ni nini??''hawa ni hizbu zanzibar ni ya weusi''hayo mambo mwanadamu kaumbiwa lakini ayashinde.Lile ni taifa teule lilivushwa bahari ya shamu kwa muujiza wa kutisha na Mungu,kuna taifa lilishawahi kufanyiwa hivyo hapa duniani???kwanza hilo neno Israel tu wamepewa si na mwanadamu bali ni Mungu mwenyewe aliwapa kwa nini wasijisikie fahari??
Unazungumziaje juu ya imani yao isiyomtambua wala kumwamini yesu kama masihi?
 
Huna haja ya kijiuliza sn, historia ya Taifa la Israel ndio pekee inajulikana toka kuumbwa kwa dunia hii,, wakati historia ya Tanzania imeanzia hapo juzi wakt wa Mjerumani,,

Pia kwenye Biblia imeandikwa kila Ailaanie Israel nae Atalaaniwa na kila Aibarikie Israel naye pia Atabarikiwa , hivyo watu kutundikwa kwa bendera za Israel watu wanatafuta Baraka ndio maana unaziona kwa watu waliobarikiwa zikiwa ndani ya Magari,,

Bendera hizi huzikuti kwenye Bar, Casino, au kwenye Guest house bali unazikuta kwenye uwepo wa Mungu pale watu wanapohitaji ukaribu wa Mungu uwe nao wawapo safarini nk.
Nikiweka kwenye bar kitatokea nini?
 
Na hapo ni ndipo ninaposhindwa kumshangaa mungu wenu anayewapanga watu kwa magroup.. Kwamba huyu in first class mja na huyu ni second class mja.. Tena huwapanga hivyo wala so kwa uchamungu wao ! Bali ni kutokana na kuzaliwa by chance katika taifa hilo tu ! What a miracle ![emoji57]
Ila kupanga foleni kwenda miji ya watu kufanya Hijah ni sawa kwa nini isiwe pale Makete ndio patakatifu,kwanini Quraan haikushwusha kwa lugha ya kisambaa na mbona hakushushiwa Tuntufye Mwakajila mshangae mungu wako kwa haya kwanza kwa nini kapendelea upande mmoja au weusi ni laana,tunalazimishana tukufuru bila sababu wakati mnajua haya maandiko yana upana wake inafika kipindi inabidi dawa ya chizi kua chizi.
 
Mbona hao waisraeli hawabebi bendera za Tanzania. Na haya mambo yanafanyka kwenye nchi za kiafrika maana Marekani PAMOJA NA ushosti wote na Israeli huwezi ona raia wake wakitembea na hizo bendera never ni sisi tu wafuata mkumbo bila kuelewa.
Halafu kuna kitu nakishangaa kwa hawa wakristo wanaobeba hizi bendera maana sio wote. Wanasena wanamuamini YESU Kristo but wanapeperusha bendera za watu wasiomuamini YESU kristo
Ok sisi wakristo ile bendera inatukumbusha kipind ya daud na inaitwa star of David .na daud ndo chanzo cha masihi Yesu.wao waamin wasiamin ila sisi tunaamin
 
Ni sawa tu na watu kushabikia Man U, Liverpool etc!
Wapo wanaoweka bendera zaa Jamaica na Ethiopia!
Wapo pia wanaoweka picha za misikiti ya Makka, madina na Jerusalem!
Ni symbol ya Imani ya mtu na kwa wakristo waliowengi bendera hiyo inasymbolize imani yao kwa kanisa!
Ni sawa tu na ushabiki wa Barcelona watu wanawekka bendera za team yao!
Na kuna bendera nyingi na fulana nyingi za team za uingereza wenye magari na mitaani kuliko hata hizo za Israel!
 
ISAYA 62:10 , “Tokeni nje! Tokeni nje! Mkaandae barabara ili watu wangu wapate kurudi! Jengeni barabara, ondoeni vikwazo, na
MPEPERUSHE BENDERA YA ISRAELI . ”
Sasa wasikie wana Israeli wanasemaje juu ya Yashua (Jesus)

 
Za saudi Arabia tunatundika mbona Sana..... ila Nadhani za Israel zina market zaidi....
Ishu sio market,ishu ni motive inayosukuma watu kufanya hivyo hakuna mtu anaelazimisha watu wafanye hayo wanayofanya,mpaka inaonekana tishio
 
Waafrika wengine ni kama ng'ombe tu.
Waisraeli wanamuita mtu mweusi NYANI halafu Nyani hao hao wanashangilia Waisraeli.
Dah....
Utumwa wa akili mbaya sana
Hata kama wanatuita hivyo hao ni binadamu,vipi Mungu anatuitaje sisi.
 
Mbona hao waisraeli hawabebi bendera za Tanzania. Na haya mambo yanafanyka kwenye nchi za kiafrika maana Marekani PAMOJA NA ushosti wote na Israeli huwezi ona raia wake wakitembea na hizo bendera never ni sisi tu wafuata mkumbo bila kuelewa.
Halafu kuna kitu nakishangaa kwa hawa wakristo wanaobeba hizi bendera maana sio wote. Wanasena wanamuamini YESU Kristo but wanapeperusha bendera za watu wasiomuamini YESU kristo

Kwani wamarekani wanatembea na Bendera za Tanzania? Mbona hapa zimejaa za Marekani kila mahali na hadi watu wazitumia kama leso na hakuna anaehoji?

Tatizo ni mwamko wa watu kuanza kupenda za Waisrael tu? Acha weeeeewe!!!
 
kun

nadhani ni kasumba tu kwa baadhi ya wafuasi wa yesu kudhani bendera ya kizayuni ya israeli inawakilisha israel ya ndani ya biblia takatifu. israel ya leo ni nchi ya mazayuni wabaguzi wakubwa. ni nchi sawa na apartheid south africa.
Haijalishi
 
kun

nadhani ni kasumba tu kwa baadhi ya wafuasi wa yesu kudhani bendera ya kizayuni ya israeli inawakilisha israel ya ndani ya biblia takatifu. israel ya leo ni nchi ya mazayuni wabaguzi wakubwa. ni nchi sawa na apartheid south africa.
sio wafuasi wa Yesu tu. kwani hata wafuasi wa Muhamadi wanajua ukweli ila hawataki kuukubali,mbona hata qoran imekiri kuwa waisraeli ndio "waliokabidhiwa kitabu" unajua maana ya sentensi hiyo?
 
Nakubaliana na wewe kwamba kuna watu kama wewe ambao mnaikubali tabia yake ya ubabe wake huko mashariki ya Kati.Lakini pia ukubali kwamba kuna watu wanaiona Israel kama "taifa teule" na hapa kuna utata kwani ni zaidi ya Itikadi za kisiasa bali tunakwenda hadi kwenye Itikadi za kidini.

Kuna watu wanaodhani kwamba Waisrael ni wakristo (kwa maana ya asilimia) lakini waisrael kwa asili hawaamini kama Yesu ni Masihi Mpakwa mafuta wa Bwana Mungu Yehova. Ndiyo maana wakati kuna baadhi ya Wakristo wanakwenda Hija Israel waisrael wenyewe wanawashangaa na kuwaona kama ni watalii wa kawaida wanaokwenda kutalii maeneo ya Kihistoria yasiyo na mashiko ya Kiimani.

Kama ambavyo kuna mtizamo hasi kwamba Wapalestina wote ni waislam, wakati wapalestina wapo na wakristo na wao pia wanaporomoshewa mabomu na waisrael kama wanavyopromoshewa wenzao waislam kwenye nchi yao!!

Kwa kuongezea; Waisrael sio Wakristo bali walio wengi ni wayahudi ambao bado wanafuata imani, mila na desturi zao tofauti na ukristo.....kuanzia mavazi hadi sikukuu...kwa wale wanaotaka kujua zaidi google neno HANUKKAH! Kwangu mimi wanaoweka Bendera ya Israel hakuna tofauti na wanaopeperusha Bendera ya Marekani, Simba, Yanga, au Kubandika Picha za Messi, Ronaldo etc...
 
Back
Top Bottom