Bendera ya Israel ndani ya magari ya Dar ni siasa tu au kuna la zaidi?

Bendera ya Israel ndani ya magari ya Dar ni siasa tu au kuna la zaidi?

Waungwana kuna mambo maishani huwa yanapotazamwa humuachia mtazamaji kila aina ya tafakuri kichwani mwake. Ndani ya miaka kadhaa ya hivi karibuni, kumezuka tabia ya watu kuitundika bendera ya Israel kwenye sehemu ya chini ya kioo cha ndani ya gari, kile ambacho dereva hukitumia kutazama magari yanayokuja kutokea nyuma ya gari.

Mwanzoni nilidhani ni mahaba binafsi ya mtu mmoja, lakini kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo mashabiki wa bendera hiyo maarufu duniani, walivyozidisha tabia hiyo.

Huwa najiuliza kama Waisrael na wao wanayo tabia ya kuitundika bendera ya Tanzania, katika sehemu ile ile ambayo sisi tunaitundika bendera yao ndani ya magari yetu. Huwa najaribu kujiuliza iwapo Mtanzania anayekatiza katika mitaa ya Jerusalem au Tel Aviv anaweze kukutana na gari ambalo ndani yake kuna bendera ya Tanzania imetundikwa, na muisrael akiendesha gari huku akiufurahia uwepo wa bendera yetu.

Haya ni mawazo yangu, kwani tabia hii imenifanya nijiulize iwapo upendo unaotoka mioyoni mwetu kuelekea kwa Waisrael, unaweza na wenyewe kuwa unathaminiwa na Waisrael bila ya sisi Watanzania kujua ni jinsi gani tunavyothaminiwa.
Kuwapo kwa bendera hiyo inamaanisha kuwa wao wanafurahia Kimtindo waisrael wanavyowafanyia wapalestina, kindanindani watu hao pia ni wadini na ni lazima watakuwa Christian's extremists.
 
Hiyo nchi ilibalikiwa from beginning that's why. Unavoona sayansi na teknolojia, chanzo ni Israel. na wavumbuzi wa mambo mengi duniani ni Wayahudi. so unavoona bendera nyingi kwa daladala ni wanapata mibaraka coz Israel. maana Sir God alisema JAMAA ZOTE ZA DUNIA ZITABARIKIWA KUTOKANA NA TAIFA LA ISRAEL
Nani kakwambia Sayansi na Technologia imeanza na Israel. Fuateni mdundiko tu. Dah ndio mkapelekwa ugahibuni katika Utumwa Mamboleo

Might is not right
 
Nalipenda mno neno "Israel" kuliko neno "Tanzania" maana neno Israel limeasisiwa na Mungu Mkuu
muumba wa mbingu na nchi; Mungu wa Ibrahimu; Mungu wa Isaka; Mungu wa Yakobo na baadae huyu ndiyo Israel; Maana ya jina lenyewe ni mshindi: Lakini neno Tanzania limeasisiwa na binadamu kwahiyo ni la kawaida tu. Hakuna nchi ya kusimama kupigana na Israel na ikashinda si Urusi,Marekani, Ujerumani wala China.

Fimbo ya enzi haitaondoka mikononi wa Yuda mpaka atakapokuja yeye mwenye kumiliki: Wafilisiti na Waarabu wote wanaifahamu vyema hii fimbo tokea enzi za Musa, Joshua na Daudi mwana wa Yese pia Mfalme wa Israel. Hii historia ilikuja kujirudia ule wa miaka ya 1962-1968-9 pale nchi takribani 9 za kiarabu ziliposalimu amri kwa taifa lenye watu wasiozidi milioni moja.
Pumba!!!
 
Usitoke mishipa ya shingo kwa kulazimisha jambo,kitu muhimu uelewe tu israel haiwezi kusimama kwa miguu yake bila hizo nchi za magharibi kwanini hao waisrael wasiyafanyie kwao mambo yote na pesa ibaki hapopapo kwao na ikiwezekana wao ndio wapeleke misaada huko u.s na kwingineko? Acha kutetea ujinga
Msambichaka Mkinga kaongea jambo LA KWELI mkuu... Fuatilia historia utasoma hii kitu.
 
Tafuta kwenye Biblia mwanzo hadi mwisho hukiti jina la Tanzania wala Tanganyika,,

Israel ni jina teule limetoka kwa MUNGU YEHOVA mwenyewe kapewa mzee Jacob,, Tanzania ni jina tu kama ulivyo jiita wew Emmadogo,,

Mataifa yote yanayo ichukia Israel hulaaniwa na Mungu ,, vita haiishi nchi mwao,, Libya, Misri,, Syria,, Iraq,, Lebanon,, Yemen,,Afganstan,, Somalia,, Sudan nk.

Lakini nchi zote duniani zenye mapenzi mema na Israel zina wingi wa Amani na furaha kwa raia wao,, na ndio limbo lip kwa watu wa mataifa yenye chuki dhidi ya Israel,,
Cc kahtaan FaizaFoxy big show Elungata
 
Utafsiri wa biblia ni mpana sana.Israel sio tu mahali pale ni dunia nzima na watu wake .atakaye wapenda watu wangu atabarikiwa.atakaye walaani watu wangu naye atalaaniwa pia
 
Nalipenda mno neno "Israel" kuliko neno "Tanzania" maana neno Israel limeasisiwa na Mungu Mkuu
muumba wa mbingu na nchi; Mungu wa Ibrahimu; Mungu wa Isaka; Mungu wa Yakobo na baadae huyu ndiyo Israel; Maana ya jina lenyewe ni mshindi: Lakini neno Tanzania limeasisiwa na binadamu kwahiyo ni la kawaida tu. Hakuna nchi ya kusimama kupigana na Israel na ikashinda si Urusi,Marekani, Ujerumani wala China.

Fimbo ya enzi haitaondoka mikononi wa Yuda mpaka atakapokuja yeye mwenye kumiliki: Wafilisiti na Waarabu wote wanaifahamu vyema hii fimbo tokea enzi za Musa, Joshua na Daudi mwana wa Yese pia Mfalme wa Israel. Hii historia ilikuja kujirudia ule wa miaka ya 1962-1968-9 pale nchi takribani 9 za kiarabu ziliposalimu amri kwa taifa lenye watu wasiozidi milioni moja.
Cc

kahtaan
Pol Pot
Mahmood
FaizaFoxy
Elungata

[emoji2] [emoji2]
 
kinachokuuma katika hilo ni kipi? Na wewe si uweke bendera unayoitaka katika gari lako?
Hivi hujui Tanzania una uhuru huo? Kinachofuata ni kipi? Kuhoji kwa nini jirani zako wanakula kuku kila siku au?
 
Mbona hao waisraeli hawabebi bendera za Tanzania. Na haya mambo yanafanyka kwenye nchi za kiafrika maana Marekani PAMOJA NA ushosti wote na Israeli huwezi ona raia wake wakitembea na hizo bendera never ni sisi tu wafuata mkumbo bila kuelewa.
Halafu kuna kitu nakishangaa kwa hawa wakristo wanaobeba hizi bendera maana sio wote. Wanasena wanamuamini YESU Kristo but wanapeperusha bendera za watu wasiomuamini YESU kristo
Kwani wewe ni nani hata kuwapangia watu jinsi ya kutumia resource zao au vitu vya kubandika? Waislam wengi wana picha ya Al Kaaba. Ni Hiyari yao hakuna tatizo. Rastafarians wanapenda kuweka Bendera sijui ya nchi gani ile (Ethiopia?) Na hakuna shida. Kuna wanaoweka picha za Osama, ni hiari yao pia. Hata hao wakristo wanaoweka bendera ya Israel ni hiari yao pia.

Wewe kinakuuma nini? Hangaikia maisha yako badala ya kufuatilia ya wengine. Watanzania kwa usakubimbi hatujambo.
 
TAIFA LA WAYAHUDI LA ISRAEL NI SAFI NA TEULE.HILI TAIFA SIO JIPYA NI LA ZAMANI SANA.WANAOSEMA NI JIPYA WANA HILA ZAO.
HII BENDERA YAO INAPATIKANA WAPI.NAIHITAJI PIA
 
Kitu kilichotuchelewesha Tanzania mpaka kuzalisha umaskini, vita, maradhi ufisadi unaanza pale tulipovunja uhusiano na Israel ashukuriwe
Mungu uhusiano wa kibarozi unarudi, kwa maana hiyo tumeji connect na baraka miaka michache ijayo hatutakuwa kama tulivyo.
 
Watu wenye mawazo mgando kama wewe ndo sababu kuu ya Tanzania kua maskini
 
Sijui tulipatwa na nini sisi watu weusi,dini za babu zetu inaelekea zilikuwa nzuri sana hawa waisrael na waarabu na wazungu na wahindi wanatubagua sana watu weusi hadi wana tu classify kwenye kundi moja la wanyama lakini sie sasa kushbikia nakufia dini zao dah,kama tungekuwa conscious tungejua kuwa tunakitu kizuri sana katika utamaduni wetu ambao umefutwa na hao watu wa races zingine sasa babu pamoja nakutuonea kwa kubaka, kuuzwa, utumwani, kutu rank watu wamwisho kabisa duniani bado hatauna chuki nao.inawezekana utamaduni wa mtu mweusi ulikuwa sahihi sana.kuliko huu ujinga tunaoshabikia sasa.mtizamo tu msijinge chuku mnaoamini dini za wengine
 
Back
Top Bottom