Bendera ya Israel ndani ya magari ya Dar ni siasa tu au kuna la zaidi?

Hili ni swala la kiimani zaidi. Sipendi kuingilia au kukosoa imani ya mtu maana hiyo ni kati yake na Mungu wake.Ukizingatia hizi dini ni za kuletewa,tungetawaliwa na wachina au wahindi si ajabu tungekua ma monk,Hindhu,Singh nk. Tuheshimiane kadili ya imani zetu
 
Unazungumziaje juu ya imani yao isiyomtambua wala kumwamini yesu kama masihi?
 
Nikiweka kwenye bar kitatokea nini?
 
Ila kupanga foleni kwenda miji ya watu kufanya Hijah ni sawa kwa nini isiwe pale Makete ndio patakatifu,kwanini Quraan haikushwusha kwa lugha ya kisambaa na mbona hakushushiwa Tuntufye Mwakajila mshangae mungu wako kwa haya kwanza kwa nini kapendelea upande mmoja au weusi ni laana,tunalazimishana tukufuru bila sababu wakati mnajua haya maandiko yana upana wake inafika kipindi inabidi dawa ya chizi kua chizi.
 
Ok sisi wakristo ile bendera inatukumbusha kipind ya daud na inaitwa star of David .na daud ndo chanzo cha masihi Yesu.wao waamin wasiamin ila sisi tunaamin
 
Ni sawa tu na watu kushabikia Man U, Liverpool etc!
Wapo wanaoweka bendera zaa Jamaica na Ethiopia!
Wapo pia wanaoweka picha za misikiti ya Makka, madina na Jerusalem!
Ni symbol ya Imani ya mtu na kwa wakristo waliowengi bendera hiyo inasymbolize imani yao kwa kanisa!
Ni sawa tu na ushabiki wa Barcelona watu wanawekka bendera za team yao!
Na kuna bendera nyingi na fulana nyingi za team za uingereza wenye magari na mitaani kuliko hata hizo za Israel!
 
ISAYA 62:10 , “Tokeni nje! Tokeni nje! Mkaandae barabara ili watu wangu wapate kurudi! Jengeni barabara, ondoeni vikwazo, na
MPEPERUSHE BENDERA YA ISRAELI . ”
Sasa wasikie wana Israeli wanasemaje juu ya Yashua (Jesus)

 
Za saudi Arabia tunatundika mbona Sana..... ila Nadhani za Israel zina market zaidi....
Ishu sio market,ishu ni motive inayosukuma watu kufanya hivyo hakuna mtu anaelazimisha watu wafanye hayo wanayofanya,mpaka inaonekana tishio
 
Waafrika wengine ni kama ng'ombe tu.
Waisraeli wanamuita mtu mweusi NYANI halafu Nyani hao hao wanashangilia Waisraeli.
Dah....
Utumwa wa akili mbaya sana
Hata kama wanatuita hivyo hao ni binadamu,vipi Mungu anatuitaje sisi.
 

Kwani wamarekani wanatembea na Bendera za Tanzania? Mbona hapa zimejaa za Marekani kila mahali na hadi watu wazitumia kama leso na hakuna anaehoji?

Tatizo ni mwamko wa watu kuanza kupenda za Waisrael tu? Acha weeeeewe!!!
 
kun

nadhani ni kasumba tu kwa baadhi ya wafuasi wa yesu kudhani bendera ya kizayuni ya israeli inawakilisha israel ya ndani ya biblia takatifu. israel ya leo ni nchi ya mazayuni wabaguzi wakubwa. ni nchi sawa na apartheid south africa.
Haijalishi
 
kun

nadhani ni kasumba tu kwa baadhi ya wafuasi wa yesu kudhani bendera ya kizayuni ya israeli inawakilisha israel ya ndani ya biblia takatifu. israel ya leo ni nchi ya mazayuni wabaguzi wakubwa. ni nchi sawa na apartheid south africa.
sio wafuasi wa Yesu tu. kwani hata wafuasi wa Muhamadi wanajua ukweli ila hawataki kuukubali,mbona hata qoran imekiri kuwa waisraeli ndio "waliokabidhiwa kitabu" unajua maana ya sentensi hiyo?
 

Kwa kuongezea; Waisrael sio Wakristo bali walio wengi ni wayahudi ambao bado wanafuata imani, mila na desturi zao tofauti na ukristo.....kuanzia mavazi hadi sikukuu...kwa wale wanaotaka kujua zaidi google neno HANUKKAH! Kwangu mimi wanaoweka Bendera ya Israel hakuna tofauti na wanaopeperusha Bendera ya Marekani, Simba, Yanga, au Kubandika Picha za Messi, Ronaldo etc...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…