Bendera ya Rais kwenye kikao cha CCM imefuata nini?

Rais wa Marekani anaweza kushitakiwa kwa tuhuma za uhaini, rushwa, au uhalifu mwingine.
Tuhuma zikithibitika kuwa kweli anaweza kuhukumiwa na kuondolewa madarakani.
Akishaondolewa madarakani bado anaweza kufunguliwa kesi katika mkondo wa kawaida wa sheria.

Rais wa Tanzania ni mtakatifu mwenye kinga ya kutoshtakiwa kwa tuhuma zozote zile.
Hakuna mahakama hata ya kikatiba inayoweza kupokea na kusikiliza mashtaka dhidi yake.
Na hata akitoka madarakani bado hawezi kushtakiwa na hakuna adhabu ambayo anaweza kupewa.
 
Tuonyeshe kifungu kinachomkataza raisi kutinga na bendera ya raisi kwa vikao vya chama .!
 
Wanajadili kati ya haya;
1. Swala la mkataba OVU wa ccm na dipii wedi.
2. Kumpa cheo "Abdul" atambulike rasmi.
3. Kesi za UHAINI walizobambikiziwa wazalendo wa raslimali za inchi badala ya WAHAINI wenyewe wa raslimali za nchi.
 
Tuvunje sheria hizi OVU kwani ndio zinafanya;
Wavunje na kunajisi katiba wapendavyo!
Wafanye mikataba OVU na ya UFISADI bila AIBU,
 
Ndo maana madudu hayaishi uku kwetu.
 

Kwa mfumu wa katiba ya tanzania, huwezi kumtenganisha rais na mamlaka aliyo nayo hata kama atakuwa kwenye sherehe za bathday, licha akiwa kwenye kikao cha chama ambacho ndicho kinasimamia serikali anayoiongoza.

Ndiyo maana hata kweny kampeni za urais, bado unakuta ana maagizo ya kimamlaka na anatumia raslimali za nchi kama vile bado ni rais.
 
Hatutaki kuishi kwakuzingatia taratibu tulizojiwekea wenyewe,alafu tunalalamika kuna mambo hayaendi sawa sawa.tunashindwa kuelewa kua kitendo chakutozingatia taratibu madhara yake yanaenda kuathiri maeneo mengi yakitendaji.mwisho wa siku tunabaki kumwona rais analalamika na wananchi wanalalamika.Wote hatujui tatizo ni nini.Tunasahau kua tatizo ni sisi wenyewe kufanya mambo kwamazoea au kwakutokujali,ubinafsi na uzembe mbele kuliko weledi.
 
Kwa hiyo anapeleka rungu lake la urais kwenye kikao cha chama? mama anapenda udikteta huyu.
 
Yupo sahihi
Mambo kama hayo ndiyo maana awataki kubadilisha katiba yetu maana si umeona hata kule aliyemwakilisha kwa Mu7, toto yake
 
Yupo sahihi
Mambo kama hayo ndiyo maana awataki kubadilisha katiba yetu maana si umeona hata kule aliyemwakilisha kwa Mu7, toto yake
Utasikia wajinga wanauliza "ulitaka uende wewe?"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…