Benjamin Mkapa: Natamani kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Wapinzani wahusishwe kwenye kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa mshindi

Sisi ni malofa, na kwa ulofa wetu mkapa ni muungwana. Tusha msamehe
 
Hodii jamani humu jukwaani,, Kauli ya mkuu huyu wa zamani imenifanya niache kupitia mada na comments za humu jukwaani kama ulivyo kua desturi yangu. Mzee huyu hajitambui kwa uelewa wangu, maana ni yeye alietuitaga malofa wakati wa kampeni zile.
 
Return Of Undertaker,
Ana haki ya asili ya kujutia makosa yake. Ni jambo jema na funzo kwa viongozi wa sasa. Kila mtu ana haki ya kujutia makosa yake. Unataka afe na jambo analodhani ni kosa bila kushauri vizazi vya sasa?
 
Return Of Undertaker,
Angesema kwa uwazi tu kwamba amemchoka Magufuli. Maana anayotamani sasa yalikuwepo hata katika uongozi wake na alikuwa katika nafasi nzuri kuyafanya, na kila atakae maliza muda wake wa uongozi atakuja kuzungumza ata makosa aliyoyafanya kama paukwa pakawa, kwa sababu wanajuwa wana kinga ya kutoshtakiwa.

Huyu mzee alishawahi kusema kwamba wanaotaka mabadiliko ni wapumbavu na malofa. Je alichoandika kwenye kitabu chake kinaitafsiri vipi kauli yake?
 
Mkapa na hao maraisi wastaafu walishiriki kumweka Jiwe madarakani amwambie ukweli hayo anayoyaona si sawa kufanyika kwenye mfumo wa vyama vingi kwani hayo yasiyofaa alishiriki kuyaasisi.
 
Songambele, Uko sahihi Mkuu,Mkapa aliunda tume kama si ya Jaji Kisanga basi ni ya Nyalali lakini ilipomletea ripoti aliichana ripoti yao mbele yao na kuwafokea kuwa hakuwatuma waliyoyaandika. Anahukumiwa na mengi.
 
Mnafiki huyu, hasidi aso na haya

Demokrasia ya kweli si ya maneno au majina tu. Demokrasia ya kweli lazima ianzie kwenye vyama vyetu vya siasa. Huwezi kudai demokrasia ya kweli nje ya chama wakati demokrasia ndani ya chama iko katika jina tu au iko katika maneno tu. Unafiki, uhasidi na kukosa haya ni pale chama cha siasa na wafuasi wake wanapopiga kelele za kudai demokrasia wakati ndani ya chama chao hakuna pumzi ya demokrasia na viongozi wa vyama vyao wapo kama masultan.
 
Kwa maana nyingine Mkapa anathibitisha kwamba NEC ni tawi la CCM na hao CCM ndio huhesabu kura na kuamua yupi wamgawie ngapi.
Usilazimishe mawazo yako ndio yawe ndio uhalisia wa mambo na wala mkapa hakumaanisha kama unavyotafsiri
 
Hii kitaa zamani tulikuwa tunaimba "Danganya toto, kula kunde nyama mbichi".
 
Anajutia cha kwenda nacho kumjibu Mwenyezi Mungu kwa yale aliyoyatenda,Jamani dhambi ya kudhulumu watu ni mbaya sana
 
Return Of Undertaker,
Ana haki ya asili ya kujutia makosa yake. Ni jambo jema na funzo kwa viongozi wa sasa. Kila mtu ana haki ya kujutia makosa yake. Unataka afe na jambo analodhani ni kosa bila kushauri vizazi vya sasa?
Kwa maoni yangu,ni sahihi.Kukosea,hatimae kupevuka na walao kutafakari ulipotoka ukaweza si tu kujuta kimya kimya,bali pia ukaliweka wazi kwa uliowaongoza,ndio ubinadamu na hutoa funzo kwa viongozi waliopo na wanaokuja.
Kwa tendo hili,binafsi limeweka picha njema zaidi kuliko asingetamka haya.

Nadhani kwenye uongozi wa juu,labda presha maamuzi mengi ya kuongoza ni nzito hadi kufisha ganzi baadhi ya hisia za kibinadamu au pia,kwa kuwa kukomaa hakiishi kuendelea hadi/hata uzeeni,nako kunawasaidia kuyaangalia mambo bila presha ya kuongoza (huku wakipata kushuhudia ya wanaoongoza wakiwa wastaafu) wakati busara zimeongezeka zaidi.

Hili liwe funzo na tafakari kwa viongozi waliopo na watakaokuja wajue,kuna siku LABDA wataandika vitabu vyao.Haya majuto,pale inapofaa,vema kuyaepuka mapema.Ukali uwepo inapobidi,ila uwe na human face na pale pa haki,itendeke kwa wote bila kujali sana upande wako au wa watu wa upande wako tu.
 
Nata
Madaraka ni kama uraibu wa vilevi. Mtu anafanya ubabe akiwa nayo na akiyaachia ndio anaona ukweli.

Ukilewa unaweza kufanya mambo ya ajabu halafu ukiwa sober unajiuliza niliwezaje kufanya vile?
Natamani hizi comment humu angekuwa anaziona Nkapa na yule bwana siambiliki ili nae tuje kuona kitabu chake atasema nini?
 
Kashaanza "kuwashwawashwa" huyu!! Ngoja Mwenzake uvumilivu umshinde
 
Return Of Undertaker,
Why did His Excellency Ben Mkapa fail to give hiyo "TUME HURU YA UCHAGUZI" ; kwa sababu he had all the tools and powers at his exposal to do that! Is His Excellency regretting or trying to push the ball in someone else's court?
Mimi nashauri Mh. Rais Mstaafu Mkapa anapokuwa anato ushauri wa kufanya baadhi ya mambo ambayo hata yeye mwenyewe angeweza kuyafanya wakati wa utawala wake pindi alipokuwa madarakani, awe anaenda mbele kidogo kwa kueleza pia sababu ambazo yeye zilimsababisha asikifanye.

Vinginevyo ushauri wake kwa ndani unaweza ukatizamwa kama uchochezi baina ya wananchi na Serikali yao, kumbe hapana. Kwa sababu wakati mwingine anashauri kifanyike kitu ambacho hata yeye mwenyewe angeweza kukifanya, lakini hakukifanya. Nashauri awe anaeleza sababu za kwa nini anaona sasa hivi inabdi kifanyike na si katika kipindi chake alipokuwa madarakani
 
Wanaanza kuelewa nini maana ya binadamu.
 
Yaani mnapoteza mda wenu tu hakuna kipya kwa CCM bila kupambana na kudai tume huru ya uchaguzi tu.

Mshawishi wananchi iwe mtandaoni na press conference vyovyote vile hamasisheni watanzania kwa uwezo wenu wote anzisheni kampeni rasmi kwa mwaka huu 2020.

Leo ni januari mpaka ifike octobaba kimeeleweka ebu muache harakati nyingine muwaze namna ya kuwaamsha watanzania kudai tume huru ya uchaguzi.

Jengeni hoja inayoeleweka kwa watanzania ccm ni wachache sana ukilinganisha na watanzania.

Hata kama mtatiwa kizuizini kwa kudai tume huru mtakuwa na hoja mtaaani kuwa mnapambana na jambo la msingi sana

chonde chonde mkipata tume huru mmeshinda uchaguzi wowowte ule. Wala sio nyie tu na wote watakaofuta katika siasa ya Tanzania

Mungu ibari Africa mungu ibariki Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…