TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

Status
Not open for further replies.
Tuanze kurekebisha na kuyaishi Yale ambayo alidai kuwa amekosea ikiwepo na tume huru ya uchaguzi. My life is my purpose.
 
R.i.p Rais mstaafu William Benjamin mkapa ndoo yako imeshajaa tupo kwenye foleni😞
 
RIP former Tanzanian President. We will miss your Economic Reform Policies.
 
Nimesikia radio Tumaini nikahisi mtangazaji amekosea! Hiki ni kishindo kwa nchi. Tunaomba Mungu nchi yetu ibakie moja kama tulivyopita salama baada ya kuondoka Baba wa Taifa. Pumzika kwa amani mzee wetu, kiongozi wetu, mtu mwenye msimamo ....Mzee Benjamini William Mkapa ...

Kishindo gani? Jana tulipata taarifa tukiwa kwenye sendoff na shughuli iliendelea.
 
Ninachoshukuru Mungu huyu mzee alibadilika sana mwishoni. Hata akiongea alionekana alikuwa anajutia maamuzi mengi aliyoyafanya huko nyuma ikiwemo kumpigia chapuo Magu kuwa raisi. Siku moja aliwaponda hadharani watu wanaosema raisi Magufuli amefanya hivi akawaambia waseme CCM imefanya hivi.

Hata hotuba yake ya mwisho kwa umma wakati anakabidhiwa tausi alionesha hapendezeshwi na sifa zinazoelekezwa kwa Magufuli tu kuhusu kuhamia Dodoma huku akieleza kuwa yeye pia alifanya sehemu na kikwete pia alifanya sehemu kubwa.

Ukisoma kitabu chake ndo utagundua kuwa alijutia mambo mengi ikiwemo mauaji ya wazanzibar mwaka 2001 na kutokuwepo kwa tume huru.

R.I.P mzee Mkapa
 
Hata uwe MBABE na MBINAFSI wa viwango vyote, HAKIKA KUFA UTAKUFA TU!

Hata wanadamu wakupe SIFA zote unazostahili na zote za KINAFIKI kama apewazo Rais wa sasa, Bw. Magufuli, HAKIKA KUFA UTAKUFA TU!

Wanaweza kujitungia sheria zote za KUJILINDA ili WASISHITAKIWE kwa makosa yao (kulinda uovu wao - kibinadamu), lakini hakuna sheria itakayotungwa duniani ama mbinguni kuzuia VIFO VYAO.

Namtakia kila la kheri Mzee Mkapa katika hatua inayofuata ya maisha yake ktk Ulimwengu mwingine tusioujua sisi tulio hai ktk dunia hii...

Neno la Mungu (Biblia inasema), BAADA YA KIFO NI HUKUMU.

Hakuna ajuaye iwapo Mzee Mkapa ata - REST IN PEACE (hukumu ya haki) AU ata - REST IN PAIN (hukumu ya matendo na maisha yasiyo ya haki, yasiyo mtii Mungu).

Poleni sana mtakaokerwa na hiki nilichokiandika. Lakini HUU NDIO UKWELI kwa ajili ya kila mtu, nikiwemo Mimi.
 
Dah home mate umetutoka... Upokelewe huko uliko, pumzika kwa amani ya Bwana
 
Duh.
Mungu aifariji familia yake na taifa kwa ujumla.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom