TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

Status
Not open for further replies.
Unajua mtu anapokufa naturally kuna stage za kifo anazipitia,hapo ndo watu huanza kuandika vitabu baada ya kuona dalili
Bado nilikuwa sijaanza kusoma kitabu cha Mzee Mengi sasa tena kimekuja cha Mkapa nina homework kubwa.
 
Njia ni moja,sote tuko kwenye foleni tutokako na tuendako hatupajui kwa hiyo tusipigane au kufanyiana hujuma sisi kwa sisi huku tukiwa kwenye foleni...we are all gonna die anyway!

R.I.P Mkapa
 
Kuna jambo la kujifunza kwa kifo cha mzee Mkapa

1. Binadamu wote njia yetu ni moja
2. Kifo sio Mali ya Binadamu bali ni Mungu mwenyewe hivyo hatuna sababu yakutoa uhai wa MTU awaweyote kwa sababu yoyote
3. Viongozi wakiwa madarakani ni muhimu kuacha alama nzuri
4. Hakuna MTU bora zaidi ya nchi maana wote tunapita
5. Kifo hiki kiwakumbushe viongozi wajibu wao kwa wananchi

Pumzika kwa Amani mzee Mkapa
Utandawazi
Ubinafsishaji
Miundombinu
Kuimarika kwa shilingi
Upatikanaji wa bidhaaa
Kujenga misingi ya uchumi
Ubabe katika maeneo Fulani
 
Habari mbaya hii asubui asubui. Pumzika kwa amani Mzee wa Ukweli na Uwazi
 
Apumzike kwa amani mzee wa "Zama za uwazi na ukweli".

Mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe.

Pumzika kwa amani Rais mstaafu Benjamin W. Mkapa.
 
Kifo chake huenda kikamrahisishia yule mlevi wa madaraka mpango wake wa kubaki madarakani, mda utaongea zaidi
Labda awamalize kina JK, kinana na Mangula.

Aliyekuwa na sauti ya mwisho CCM baada ya Nyerere alikuwa ni Mkapa then JK. Sasa Mkapa amefariki it’s obvious anaeenda kuwa na ushawishi CCM ni Jakaya Kikwete.

Mwinyi Hana ushawishi wowote ule kwa CCM. Na Magufuli ndo kabisa, CCM wengi hawamkubali.

Hata ukiangalia kikao cha juzi cha mkutano mkuu wana CCM waliwashangilia sana Kikwete na Kinana nadhani uliona kitu pale.

CCM kwa sasa inaenda kurudi kuwa chini ya vijana wa 1995 na Magufuli akitaka kikutuliza Chama akae vizuri na hawa vijana wa 1995 Yaani Kikwete na Kinana
 
Hata uwe MBABE na MBINAFSI wa viwango vyote, HAKIKA KUFA UTAKUFA TU...!

Hata wanadamu wakupe SIFA zote unazostahili na zote za KINAFIKI kama apewazo Rais wa sasa, Bw. Magufuli, HAKIKA KUFA UTAKUFA TU!

Wanaweza kujitungia sheria zote za KUJILINDA ili WASISHITAKIWE kwa makosa yao (kulinda uovu wao - kibinadamu), lakini hakuna sheria itakayotungwa duniani ama mbinguni kuzuia VIFO VYAO...
na hata uonewe vipi utie huruma uwezavyo.

uwe mwema to the best.

pigia magoti mpaka vinyonga,kufa utakufa tu.

neno la biblia linaseam,mwanadamu yeyote aliyezaliwa na mama,siku zake za kuishi si nyingi nazo zatambaa mawinguni kama moshi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom