Tutamkumbuka Mzee Mkapa Kwa Mengi Mazuri;
KUTULETEA MWANA BORA NA KIONGOZI WA NDOTO ZA KILA MTANZANIA mh.Dr John Pombe Magufuli.
MZEE MKAPA KAMA MKATA UMEME.
Nakumbuka ilikuwa ni mwezi wa ramadhani July 2015,vijana wa CCM tulijaa pale nje makao makuu ya CCM WHITE HOUSE tukisubiri TUJUE MBIVU NA MBICHI kutoka kikaoni NEC.
Kikao kikaisha salama na GHAFLA tukawaona watu watatu WAKITOKA NJE KWA SPIDI kutupa jicho tukamuona Dr.Nchimbi,Mwenyekiti wa UVCCM Sadifa Juma Khamis na mama yetu mwenyekiti wa UWT Sophia Simba. Nyuso zao ZILISAWAJIKA na HAZIKUONESHA bashasha tulizowazoea nazo. Waliongea maneno ambayo si lazima tukakumbushana.
Baada ya nusu saa kupita,wajumbe wengine wakatoka,nikamuona mzee Mkapa na Dr.Amani Abeid KARUME WAKIWA na nyuso za kutabasamu na haukupita muda MOTORCADES zao zikaondoka.
Tukakaa vikundivikundi kuwasogelea waNEC na kuanza kupata MICHAPO ya kilichojiri.
Ilikuwa hivi;
Mwenyekiti wa CCM mh.Kikwete alishangazwa alipopokewa na HANIKIZO la nyimbo hii "TUNA IMANI NA LOWASSA OYAA OYAA OYAA,TUNA IMANIIIII NA LOWASSAAAA OYAAA OYAAA OYAAA"😂😂😂.
Mwenyekiti Kikwete akaangaza huku na huko alishangazwa Sana hakuitegemea ile Hali...Kama kawaida yake AKATABASAMU lakini kikamanda then akawaomba WAJUMBE WAKETI.
Kikao Cha NEC kikaanza rasmi,kilipofika katikati mjumbe mmoja aitwae Khamis Mgeja,mwenyekiti nguli wa CCM mkoa wa SHINYANGA akatoa muongozo kwa mwenyekiti mh.Kikwete.
Muongozo wa sheikh Arbaab Khamis Mgeja ulikuwa KUHOJI ni kwanini KIKAO KIMEVAMIWA na WASIO WAJUMBE. Waziwazi akamkumbusha mwenyekiti kuwa KATIBA YA CCM iliongezwa kipengele Cha kuwaengua MARAIS wastaafu kutokuwa Tena WAJUMBE WA NEC na kinyume chake wakaundiwa BARAZA LAO.....LINAITWA BARAZA LA USHAURI LA WAZEE. Looh sheikh Mgeja kwa kujiamini kabisa akawataja MZEE MKAPA NA MZEE AMANI KARUME kuwa ni "Intruders wasiotakiwa pale".
Mwenyekiti Kikwete akasimama na kuwaomba WAJUMBE watulie kwani kwa Mamlaka yake amewaalika wazee hao kikaoni pale😁😁😁😁.
Wajumbe wakaanza kuinuka mmoja baada ya mwingine kumpinga mwenyekiti Kikwete kuwa ANAISIGINA KATIBA Ila Kama kawaida ya alivyo na kipawa chake kikubwa Cha SIASA,mh.Kikwete AKAWATULIZA WAJUMBE.
Kumbe wale waliokuwa wakiimba ile nyimbo ya KUMSIFU MH.Lowassa ni wajumbe wengi kwa akidi ya kikao ni almost 2/3 na wote hao walikuwa KAMBI YA MZEE BABA LAIGWANAN FUNDI WA MIPANGO ISIYOFELI😀😀 LAIGWANAN EDWARD NGOYAI LOWASSA. Wakiongozwa na mfuasi wake DIE HARD arbab ashaikhul Kiraam Khamis Mgeja kiboko ya mh.Lembeli. Watu hao WALISHANUSA ya kuliwa "kekundu". Uwepo wa marehemu Mzee Mkapa ULISHAWAPA signal ya nini kinakwenda kutokea💣💣💣.
Kikao kilipokolea mh.mwenyekiti Kikwete akamuomba mzee Mkapa AONGEE ili Mambo mengine YAENDELEE. Mzee Mkapa akasema "mambooooz kidumu Chama Cha mapinduzi".
Kwa sauti ya KUTETEMA iliyo KUU na ya KIMAMLAKA akaendelea kuwaambia WAJUMBE kuwa UMEFIKA MUDA WA KUPIGA KURA NA ASIYETAKA ASIWAPOTEZEE MUDA atoke ukumbini. Akarudia "asiyetaka KUPIGA KURA atoke ukumbini".
Mamengaziiii weee HALI YA HEWA IKABADILIKA....Ukumbi UKAZIZIMA kwa hofu kuu.
UJASIRI ukawapotea "ULIPO TUPO"....NDOTO YAO YA KUMUONA LAIGWANAN anaipeperusha bendera ya CCM kwa Mara ya MWISHO IKAZIKWA.
Jamani Asubuhi hii ya msiba mzito wa Mzee Mkapa(rip).Niishie kusema kuwa MZEE MKAPA aliukata "UMEME" na bilà ya yeye LABDA kipenzi chetu Magufuli asingekuwa RAIS WETU WA AWAMU YA 5.
NITAENDELEA.
Karibuni Al KASUS Kijiweni kwangu Tandale Kwa Mtogole.
Siempre Siempre CCM,
Hasta la Victoria CCM
Aluta Continua CCM
Dr.Jumbe Brown,
Kijana Muuza Al KASUS,
Uswazi Tandale.