View attachment 1515334
Rais Magufuli kwa masikitiko amesema mzee Mkapa amefariki katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar alikokuwa amelazwa.
Mkapa alikuwa Rais wa Tanzania kuanzia 1995 hadi 2005.
Rais Mkapa alikuwa mtoto wa William Matwani na Stephannia Nambanga.
Muda wa Utawala : 23 November 1995 – 21 December 2005
Makamu wa Rais wakati wa Utawala wake: Omar Ali Juma (1995–2001), Ali Mohamed Shein (2001-05)
Mtangulizi: Ali Hassan Mwinyi
Aliyemfuata: Jakaya Kikwete
Alishawahi kuwa Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu kuanzia 1992 – 1995, Waziri wa Habari na Utangazaji, 1990 – 1992
Mkapa alizaliwa 12 Novemba 1938 (umri 81) Ndanda, Masasi, Tanganyika
Ameaga dunia tarehe 24 Julai 2020 Dar es Salaam
Ameacha Mjane Anna Mkapa na watoto wawili.
Ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Makerere, Chuo Kikuu cha Columbia.
Fani yake ni mwandishi wa habari, mwanadiplomasia
View attachment 1515344