Benki gani yenye makato ya mwezi kidogo kuliko benki nyingine au isiyo na makato kabisa?

Benki gani yenye makato ya mwezi kidogo kuliko benki nyingine au isiyo na makato kabisa?

kufanakupona

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2015
Posts
522
Reaction score
421
Nisirembe sana, kichwa cha habari kinajitosheleza.

Benki gani yenye makato ya mwezi kidogo kuliko benki nyingine au isiyo na makato kabisa?

Karibu.
 
Kwa sababu kila mmoja anamiliki account ya kampuni moja au mbili, itakuwa ngumu huyu mmoja kutoa jibu kwa mabenki yote.

Naomba kila mmoja aseme anatumia benki gani na aseme kwa mwezi anaona makato ya sh. ngapi. Wakishataja wengiwengi, tutapata majibu kwamba benki gani ina makato kidogo kwa mwezi.

Haya sasa, njoo, useme unatumia benki gani, na unakatwa sh. ngapi kila mwezi.
 
Au kuna bank inaitwa Amana bank, google hio amana bank alaf iangalie, inaweza kukufaa pia wana kila kitu alafu nahisi haina makato kiivyo
 
Mm kwa sasa niko nje ya nchi, ktk kuondoka kwangu nilitumia bank statement ya hio bank nikaingia nayo ubalozini, wana ATMs, wana tawi pale k/koo mkabala na mnazi mmoja, viza/master card pia, INGIA KWENYE GOOGLE ANDIKA PBZ ISLAMIC utaona matawi yao mbalimbali na huduma zao
Mbona wametoa VISA/master card kimyamya sana? Kwenye website yao sioni tangazo la hizi credit/debit cards.

Hawapatikani mikoa karibia yote, wana matawi matatu tu, Pemba, Unguja na Dar Es Salaam, kwa sasa wako mbioni kufungua lingine Mtwara halafu baadaye kabisa wataangalia kufungua matawi Dodoma, Arusha na Mwanza.

Kwa uchache huo wa matawi na kutotangaza products zao, ni ngumu kujua kama kuna benki inaitwa PBZ na ni ngumu kushawishika kujiunga.
 
Mbona wametoa VISA/master card kimyamya sana?, kwenye website yao sioni tangazo la hizi credit/debit cards.
Hawaptikani mikoa karibia yote, wana matawi matatu tu, Pemba, Unguja na Dar Es Salaam, kwa sasa wako mbioni kufungua lingine Mtwara halafu baadaye kabisa wataangalia kufungua matawi Dodoma, Arusha na Mwanza.
Kwa uchache huo wa matawi na kutotangaza products zao, ni ngumu kujua kama kuna benki inaitwa PBZ na ni ngumu kushawishika kujiunga.
Poa
 
Au kuna bank inaitwa Amana bank, google hio amana bank alaf iangalie, inaweza kukufaa pia wanakila kitu alaf nahisi haina makato kiivyo
Nayo ina matawi machache, Arusha, Dar na Mwanza, sisi kwa wa mikoani inakua ngumu kujiunga.

Kwa sababu ni ya kiislam, itakuwa haina makato, au itakuwa na makato kidogo, kama ilivyo kwa PBZ.

Changamoto na mambo ambayo Islamic banks wanatakiwa kuzifanyia kazi ni kueneza matawi mengi na kujitangaza bidhaa zao.
 
Nenda BARCLAY'S BANK monthly maintenance fee ni ndogo na kutoa hela kwenye Atms ni 600 tofauti na mwengine wanakata 800
 
Nmb kwa account za chap chap,hawakati kitu
Ninavyoona, card ya NMB Chap Chap account huwezi kuibadili kuwa master/VISA cad, wewe unaonaje?, inawezekana?.

Na kama inawezekana, basi hiyo Chap Chap account itabadilika, itakuwa ina makato kwa mwezi.

Maelezo yanahitajika hapa kubadili card ya Chap Chap account kuwa credit/debit card.
 
Kwa Barclays bank utapata kadi mbili ambayo ni debit na credit card na itaenjoy international banking experience ambayo utaweza kutoa(Cash withdrawal) na kuweka hela(Cash deposit) kwenye Atms so zile inconvenience za foleni kwenye branch na Atms hakuna
 
nenda BARCLAY'S BANK monthly maintenance fee ni ndogo na kutoa hela kwenye Atms ni 600 tofaut na mwengine wanakata 800
nenda BARCLAY'S BANK monthly maintenance fee ni ndogo na kutoa hela kwenye Atms ni 600 tofaut na mwengine wanakata 800
Una account Barclays? Account ya aina gani?
Mbona nasikia hao Barclays wana makato makubwa kwa mwezi?
 
Kwa Barclays bank utapata kadi mbili ambayo ni debit na credit card na itaenjoy international banking experience ambayo utaweza kutoa(Cash withdrawal) na kuweka hela(Cash deposit) kwenye Atms so zile inconvenience za foleni kwenye branch na Atms hakuna
Kwani Barclays ipo mpaka leo hapa Tanzania?, si' nasikia imesitisha huduma zake?
Kwa mwezi unakatwa sh. ngapi ya makato?
 
Balance sheet ya BARCLAY'S bank ni mara mbili ya GDP ya Tanzania na kwa tarifa tuu NBC bank ni mali ya BARCLAY'S bank
 
Tuanze kuchambua hiyo chap chap account
*Wacharge sms alert kwa almost 300tsh
*Debit card yao sio Visa&mastercard
*Transaction charges ziko juu almost 900 per transaction
*Gharama zilizojificha ni nyingi so operational yake ni kwenye nmb atms tuu
*Transaction limit per day
 
Back
Top Bottom