Benki gani yenye makato ya mwezi kidogo kuliko benki nyingine au isiyo na makato kabisa?

Benki gani yenye makato ya mwezi kidogo kuliko benki nyingine au isiyo na makato kabisa?

Nilipata kusikia kuwa DTB wanayo ambayo haina makato na unapata kadi ya Visa/Mastercard pia
 
*2500tsh kama makato tofaut na wengine wana 3660 na hadi elfu10
*600tsh makato kwenye Atms na tofaut na wengine mpka1000 per transaction
Shukrani leontiff, mpaka sasa hivi tumeshapata majibu ya benki tatu, PBZ bank, Amana bank na Barclays bank.
PBZ na Amana bank hizi ni za kidini, wanasema kwa mwezi hakuna makato.
Barclays makato kwa mwezi ni 2,500/=.
Tusubiri wanaotumia benki nyingine waje watuambie kwa mwezi service charges ni sh. ngapi.
 
nilipata kusikia kuwa DTB wanayo ambayo haina makato na unapata kadi ya Visa/Mastercard pia
Watakuja tu wenye taarifa za DTB, halafu watatuambia kama ni kweli kuna hiyo account ambayo haina makato kwa mwezi na VISA/master card juu.
 
Tuanze kuchambua hyo chap chap account
*Wacharge sms alert kwa almost 300tsh
*Debit card yao sio Visa&mastercard
*Transaction charges ziko juu almost 900 per transaction
*gharama zilizojificha ni nyingi so operational yake ni kwenye nmb atms tuu
*Transaction limit per day
*inawezekana kuwaomba NMB wakubadilishie iwe VISA au master card?
*lisemwalo na watu wengi laweza kuwa lina ukweli, watu wengi wanasema Chap Chap account haina makato. Wewe unasema ina makato yaliyojificha, unatumia hiyo account ya Chap Chap ndiyo maana umesema ina vigharama vidogovidogo vilivyojificha?
 
Mambo kama haya watu hawayadadavui..ila ikiletwa mada ya mapenz,saivi uzi ungekuwa wa page kama 100..

Natumia crdb makato yake sio mchezo,si kushauri sana kuitumia

*Tatizo ya local banks nyingi integrity iko chini na pengine haipo so nachoweza wambia kabla hujafanya chochote na hizi banks jaribu kuomba wakupe tarrif na upewe tarifa mabank mengi yanatumia mwanya wa consumer ignorance kuumiza watu
 
Barclays makato yao hayaeleweki,na ukiwauliza wanakupa maelezo mengi ambayo hata hayaeleweki!
*Sidhani kama ni kweli unachongea kwa upande wa customer care wako vzuri alafu mzee angalia dollar account bank zingine wanakata shilling ngap kikubwa ni wewe uwe mkweli tuu
 
Mambo kama haya watu hawayadadavui..ila ikiletwa mada ya mapenz,saivi uzi ungekuwa wa page kama 100..

Natumia crdb makato yake sio mchezo,si kushauri sana kuitumia
Unatumia account ya aina gani?
Kwa wewe unachajiwa sh. ngapi kwa mwezi as a service charge?
 
Duh!baclays wana makato ya ajabu mno,akaunti ya usd uwa wanakata hadi usd 12 kwa mwezi!
Benki huwa inakuwa na account nyingi, mteja ni chaguo lako uchague ipi, kuna za kawaida(hizi makato yake ni ya kawaida, na ndizo ambazo nataka nijue kila benki wanakate kwa mwezi), za wanafunzi(hizi makato yake yapoje sijui), za USD(hizi makato yake makubwa) na nyingine nyingi.
 
Barclays makato yao hayaeleweki,na ukiwauliza wanakupa maelezo mengi ambayo hata hayaeleweki!
Inategemea na account uliyofungua, kila account ina makato yake, ukienda kufungua account waambie nataka kufungua aacount ambayo makato yake ni madogo kuliko account zote.
Uzuri wa Barclays unapokea fedha kutoka paypal na unazitoa kabisa kwenye ATM, benki nyingine hazina hiyo huduma, ni Barclays peke yake nchi nzima ndiyo mwenye hiyo kitu.
 
Hii account ya Chap chap haifai na inazingua kama utataka kuweka zaidi ya 5 million...
Kuna comment humu ya leontiff inasema Chap Chap account ina makato madogomadogo yaliyojificha, bahati nzuri wewe una hiyo account, ni kweli ina vijigharama vidogovidogo vilivyojificha?
 
Back
Top Bottom