Benki Kuu ya Tanzania: Hatuuzi dhahabu kufadhili miradi ya Serikali

bodi ya BoT imeidhinisha benki hiyo kuwa na hifadhi ya dhahabu isiyozidi dola za Marekani bilioni mbili, wakati thamani ya sasa imefikia dola bilioni 3.24,
Acheni kutufanya sisi ni wapumbavu kama nyie, Kwanini bodi isikae kuongeza kiwango?
Yaani hio dola bil 2 ndio hifadhi ya kutosha? Semeni mnataka kuiba tu
 
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa ina mpango wa kuuza sehemu ya hifadhi yake ya dhahabu kwa ajili ya kufadhili miradi ya kimkakati ya serikali.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Fedha wa BoT, Emmanuel Akaro, amesema madai hayo si ya kweli.

Ameeleza kuwa kinachotekelezwa ni mpango wa kuuza dhahabu iliyozidi kiwango kilichoidhinishwa, kwa lengo la kusawazisha mizania ya hifadhi ya dhahabu ya benki hiyo.

Kwa mujibu wa Akaro, bodi ya BoT imeidhinisha benki hiyo kuwa na hifadhi ya dhahabu isiyozidi dola za Marekani bilioni mbili, wakati thamani ya sasa imefikia dola bilioni 3.24, hivyo kutokana na tofauti hiyo, benki inapanga kuuza kiasi kilichozidi kiwango kilichowekwa.

Amefafanua kuwa fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo hayo zitawekezwa katika masoko ya fedha ya kimataifa kwa lengo la kuongeza mapato ya uwekezaji, na si kwa ajili ya kufadhili miradi ya serikali.

Akaro amesisitiza kuwa BoT ni chombo huru, na uamuzi wowote wa kutumia uwekezaji wake kufadhili miradi ya serikali unahitaji idhini ya Bunge.

Hadi jana Januari 29, 2026, BoT ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni yenye thamani ya dola bilioni 6.52, na kati ya hizo, dhahabu inakadiriwa kuwa dola bilioni 1.2, dola za Marekani bilioni 3.8, na sarafu ya China (yuan) dola milioni 735.

Pia Soma

Hii akili gani ya kuuza dhahabu [RESERVE CURRENCY] halafu uende ukawekeze kwenye masoko ya fedha ambako faida yake utalipwa makaratasi $$$ ambayo thamani yake inapungua kila kukicha!! It does not make economic sense!! LEAVE OUR GOLD ALONE AS IT CONTINUES TO APPRECIATE.
If the government is in short supply of forex due to its wasteful expenditures, it should revisit its budget and cut all the waste that is embedded in it.
 
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa ina mpango wa kuuza sehemu ya hifadhi yake ya dhahabu kwa ajili ya kufadhili miradi ya kimkakati ya serikali.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Fedha wa BoT, Emmanuel Akaro, amesema madai hayo si ya kweli.

Ameeleza kuwa kinachotekelezwa ni mpango wa kuuza dhahabu iliyozidi kiwango kilichoidhinishwa, kwa lengo la kusawazisha mizania ya hifadhi ya dhahabu ya benki hiyo.

Kwa mujibu wa Akaro, bodi ya BoT imeidhinisha benki hiyo kuwa na hifadhi ya dhahabu isiyozidi dola za Marekani bilioni mbili, wakati thamani ya sasa imefikia dola bilioni 3.24, hivyo kutokana na tofauti hiyo, benki inapanga kuuza kiasi kilichozidi kiwango kilichowekwa.

Amefafanua kuwa fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo hayo zitawekezwa katika masoko ya fedha ya kimataifa kwa lengo la kuongeza mapato ya uwekezaji, na si kwa ajili ya kufadhili miradi ya serikali.

Akaro amesisitiza kuwa BoT ni chombo huru, na uamuzi wowote wa kutumia uwekezaji wake kufadhili miradi ya serikali unahitaji idhini ya Bunge.

Hadi jana Januari 29, 2026, BoT ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni yenye thamani ya dola bilioni 6.52, na kati ya hizo, dhahabu inakadiriwa kuwa dola bilioni 1.2, dola za Marekani bilioni 3.8, na sarafu ya China (yuan) dola milioni 735.

Pia Soma
🤣🤣 Eti wanauza dhahabu iliyozidi...
 
Yani uuze dhahabu ukawekeze McDonald, chase, American Airlines na BYD?😁😁😁😁

Hivi sisi kengez tumemkosea nini huyu Mungu (Kama yupo na anaona though)?

Return ni chini ya 11% per annum dah! Gold inapanda value progressively kila siku! Uwekezaji wa kipare? Wauza ng’ombe ununue mbuzi😎😁😁😁
 
Ameeleza kuwa kinachotekelezwa ni mpango wa kuuza dhahabu iliyozidi kiwango kilichoidhinishwa, kwa lengo la kusawazisha mizania ya hifadhi ya dhahabu ya benki hiyo.😂
Kwani zikizidi zitaoza au nafasi ndogo?
Mkuu watafutie eneo hapo Kibaigwa watunze dhahabu watu wanatunza dhahabu za kutosha huko Chunya eti serikali inakuja na maneno ya mizania hawa jamaa sijui walisoma wapi shule zao kazi za kupeana hizi kazi kweli kweli.
 
Yani uuze dhahabu ukawekeze McDonald, chase, American Airlines na BYD?😁😁😁😁

Hivi tumemkosea nini Huyu Mungu (Kama yupo na anaona though) sisi kengez?
Kweli tunapata adhabu sana kwa kweli wenzetu wanaojitambua hiki ndio kipindi mafuta yanashuka bei na hela yetu inakua stable kwa fedha za kigeni ila kwa sababu tunatafuta mizania ya kutunza zhahabu wacha tuendelee kuona moto..
 
Wauze yote hata sisi tuambulie.. hivi wanayofanya utashangaa kuna siku anakuja mtu na makarqtqsi qnakwambia nchi hii ni yangu ondoka, na wewe hujapokea hata senti 10 kipande.
Wasomi wameona ardhi tuliyonayo haina thamani tena kwa kitu chochote sasa wameamua kufanya kazi nyepesi kama za kulima Mchicha pembeni mwa mto wami...ila kwa jinsi walivyo watauza kila kitu tupo hapa ni kama watoto waliorithi mali kutoka kwa baba yao na wao akili ya kuendeleza mradi hawana ni kuuza na kushinda bar..
 
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa ina mpango wa kuuza sehemu ya hifadhi yake ya dhahabu kwa ajili ya kufadhili miradi ya kimkakati ya serikali.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Fedha wa BoT, Emmanuel Akaro, amesema madai hayo si ya kweli.

Ameeleza kuwa kinachotekelezwa ni mpango wa kuuza dhahabu iliyozidi kiwango kilichoidhinishwa, kwa lengo la kusawazisha mizania ya hifadhi ya dhahabu ya benki hiyo.

Kwa mujibu wa Akaro, bodi ya BoT imeidhinisha benki hiyo kuwa na hifadhi ya dhahabu isiyozidi dola za Marekani bilioni mbili, wakati thamani ya sasa imefikia dola bilioni 3.24, hivyo kutokana na tofauti hiyo, benki inapanga kuuza kiasi kilichozidi kiwango kilichowekwa.

Amefafanua kuwa fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo hayo zitawekezwa katika masoko ya fedha ya kimataifa kwa lengo la kuongeza mapato ya uwekezaji, na si kwa ajili ya kufadhili miradi ya serikali.

Akaro amesisitiza kuwa BoT ni chombo huru, na uamuzi wowote wa kutumia uwekezaji wake kufadhili miradi ya serikali unahitaji idhini ya Bunge.

Hadi jana Januari 29, 2026, BoT ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni yenye thamani ya dola bilioni 6.52, na kati ya hizo, dhahabu inakadiriwa kuwa dola bilioni 1.2, dola za Marekani bilioni 3.8, na sarafu ya China (yuan) dola milioni 735.

Pia Soma
wanatuona kama makalio yao
 
Back
Top Bottom