Benki Kuu ya Tanzania: Hatuuzi dhahabu kufadhili miradi ya Serikali

Benki Kuu ya Tanzania: Hatuuzi dhahabu kufadhili miradi ya Serikali

Hiyo sheria inataja thamani ya hiyo dhahabu au kiwango cha uzito?

Na ni busara gani hiyo imetumika kuuza dhahabu ambayo thamani yake bado inapanda kwa kasi ili kwenda kuwekeza katika maeneo ambayo yana faida ndogo zaidi na ambayo yana risk kubwa zaidi?

Hawa watu wamesikiliza hotuba ya hivi karibuni ya Waziri Mkuu wa Canada kule Davos kwenye World Economic Summit?
Hata wakiisikia unafikiri wataifwata?!
 
Tayari mhimili wa dola, mhimili wa Bunge na BOT wapoteza kumbukumbu za Kitaasisi (institutional memory) kwa makusudi au kwa mkakati wa kupora mali ya taifa

TOKA MAKTABA :

15 June 2023
MWIGULU - AKIBA YA DHAHABU

View: https://m.youtube.com/watch?v=rJX8URvdEeA
"Serikali imekamilisha taratibu za kununua dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kuanzisha akiba ya dhahabu ya Taifa (Gold Reserve).

Aliambia Bunge kuwa hatua hii itawapatia wachimbaji bei nzuri zaidi na kuimarisha sarafu yetu,"- Dkt. Mwigulu Nchemba

Nov 27, 2025
Gavana Tutuba - Hifadhi ya Dhahabu tani 15.37 imehifadhiwa nje ya nchi, na yote ipo huko katika Bank of England Uingereza

30 January 2026

Benki kuu yakanusha kuuza akiba ya dhahabu kwa ajili ya kufadhili miradi ya serikali​

View: https://m.youtube.com/watch?v=f1DG0GDFN8o
 
Wasomi wameona ardhi tuliyonayo haina thamani tena kwa kitu chochote sasa wameamua kufanya kazi nyepesi kama za kulima Mchicha pembeni mwa mto wami...ila kwa jinsi walivyo watauza kila kitu tupo hapa ni kama watoto waliorithi mali kutoka kwa baba yao na wao akili ya kuendeleza mradi hawana ni kuuza na kushinda bar..
Na wakiambiwa ukweli wanaona wanatukanwa, ni kweli hawana nia ya dhati wala akili ya kuipeleka nchi katika maendeleo.
 
TOKA MAKTABA:

Nov 27, 2025
Gavana Tutuba - Hifadhi ya Dhahabu tani 15.37 imehifadhiwa nje ya nchi, na yote ipo huko katika Bank of England Uingereza

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, amesema kuwa hadi sasa Benki Kuu imenunua jumla ya tani 15.37 kupitia mpango wake wa ununuzi wa madini hayo, ikiwa ni hatua muhimu ya kuongeza akiba ya fedha za kigeni na kuimarisha thamani ya shilingi.. na kuwa dhahabu ya BoT imesafirishwa na kuhifadhiwa ktk benki kuu ya Uingereza yaani Bank of England

View: https://m.youtube.com/watch?v=ql7hRR5sA08
Source : Bank of Tanzania

Nchi zinazozingatia sovereniti yake kama China, Russia, Algeria n.k haziwezi kupeleka Hifadhi ya Dhahabu nje ya nchi.

Tanzania tunaamini sana nchi za Mashariki ya Kati na Ulaya kuwa ni tawala zisizoweza kuigeuka Tanzania !

ALGERIA INA TANI 173.5 ZA HIFADHI YA DHAHABU BENKI KUU
Algeria’s central bank, the Bank of Algeria, holds and manages the country's gold reserves, which are reported as the largest in Africa at approximately 173.56 tonnes. While specific, precise, and current vault locations are typically classified for security reasons, these assets are managed within the national central bank's secure, official reserves system.
Key Details on Algeria's Gold:
  • Central Bank Holdings: The Bank of Algeria holds 173.56 tonnes of gold to hedge against economic uncertainty, representing a major component of its forex reserves.

Kwamba sisi hatuwezi kuhifadhi, PUMBAVU sana hawa watu
 
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa ina mpango wa kuuza sehemu ya hifadhi yake ya dhahabu kwa ajili ya kufadhili miradi ya kimkakati ya serikali.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Fedha wa BoT, Emmanuel Akaro, amesema madai hayo si ya kweli.

Ameeleza kuwa kinachotekelezwa ni mpango wa kuuza dhahabu iliyozidi kiwango kilichoidhinishwa, kwa lengo la kusawazisha mizania ya hifadhi ya dhahabu ya benki hiyo.

Kwa mujibu wa Akaro, bodi ya BoT imeidhinisha benki hiyo kuwa na hifadhi ya dhahabu isiyozidi dola za Marekani bilioni mbili, wakati thamani ya sasa imefikia dola bilioni 3.24, hivyo kutokana na tofauti hiyo, benki inapanga kuuza kiasi kilichozidi kiwango kilichowekwa.

Amefafanua kuwa fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo hayo zitawekezwa katika masoko ya fedha ya kimataifa kwa lengo la kuongeza mapato ya uwekezaji, na si kwa ajili ya kufadhili miradi ya serikali.

Akaro amesisitiza kuwa BoT ni chombo huru, na uamuzi wowote wa kutumia uwekezaji wake kufadhili miradi ya serikali unahitaji idhini ya Bunge.

Hadi jana Januari 29, 2026, BoT ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni yenye thamani ya dola bilioni 6.52, na kati ya hizo, dhahabu inakadiriwa kuwa dola bilioni 1.2, dola za Marekani bilioni 3.8, na sarafu ya China (yuan) dola milioni 735.

Pia Soma

Mimi na Finance degree yangu ya USA siwaelewi hapa sembuse mtu wa kawaida!!
 
Na wakiambiwa ukweli wanaona wanatukanwa, ni kweli hawana nia ya dhati wala akili ya kuipeleka nchi katika maendeleo.
Sema tamaa ya kupata kingi ndio kimewaharibu wangekua na nia ya dhati wangependwa sana na Nchi ingeendelea sasa wakaja na mambo ya kuwekana jela kesi hazieleweki mara kutekana ndio tabu ilipoanzia hapo..
 
IMG-20260130-WA0040.jpg
 
Kwamba sisi hatuwezi kuhifadhi, PUMBAVU sana hawa watu

India kuna mjadala, hatari ya kuhifadhi Akiba yote ya Dhahabu nje ya nchi zama hizi za ubeberu wa kimataifa.

Je hatua ya Tanzania kutaka kuuza Akiba ya Taifa ya Dhahabu ni woga wa serikali haramu ya chama dola kongwe ya Samia kuwekewa vikwazo na mabeberu au ni njama za wizi mchana kweupe ?

View: https://m.youtube.com/shorts/iiCRLLR6bN0
 
Dhahabu imefika kwenye LUMBESA.....
uzuri wenzetu wazungu wapo transparent kwenye mambo Yao ya uchumi kilakitu wataweka wazi kuanzia uzito wa dhahabu Hadi thamani ya pesa walizonunua.
Hakuna kitu kitafichwa kwenye dunia ya Leo
Tanzania utaambiwa ni Siri ya taifa ili mabeberu yasijue tu na utajiri wa kutisha.
 
Tatizo la Tanzania miluzi mingi mno, kila mtu anajua kila kitu. Kila mada kila mtanzania ana uelewa nayo.

Kule Zanzibar Rais Mwinyi anafanya makubwa hana wapiga miluzi, kaachiwa uhuru na anautumia kuleta mabadiliko.

Huku Bara wajinga wengi sana kibaya zaidi wanataka wakiongea wasikilizwe, watiliwe maanani hata kama hakuna la maana wanalolijua.
 
Kwaiyo dhahabu ambayo ni hazina ya Taifa ukiuzwa watu wakae kimya?
 
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa ina mpango wa kuuza sehemu ya hifadhi yake ya dhahabu kwa ajili ya kufadhili miradi ya kimkakati ya serikali.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Fedha wa BoT, Emmanuel Akaro, amesema madai hayo si ya kweli.

Ameeleza kuwa kinachotekelezwa ni mpango wa kuuza dhahabu iliyozidi kiwango kilichoidhinishwa, kwa lengo la kusawazisha mizania ya hifadhi ya dhahabu ya benki hiyo.

Kwa mujibu wa Akaro, bodi ya BoT imeidhinisha benki hiyo kuwa na hifadhi ya dhahabu isiyozidi dola za Marekani bilioni mbili, wakati thamani ya sasa imefikia dola bilioni 3.24, hivyo kutokana na tofauti hiyo, benki inapanga kuuza kiasi kilichozidi kiwango kilichowekwa.

Amefafanua kuwa fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo hayo zitawekezwa katika masoko ya fedha ya kimataifa kwa lengo la kuongeza mapato ya uwekezaji, na si kwa ajili ya kufadhili miradi ya serikali.

Akaro amesisitiza kuwa BoT ni chombo huru, na uamuzi wowote wa kutumia uwekezaji wake kufadhili miradi ya serikali unahitaji idhini ya Bunge.

Hadi jana Januari 29, 2026, BoT ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni yenye thamani ya dola bilioni 6.52, na kati ya hizo, dhahabu inakadiriwa kuwa dola bilioni 1.2, dola za Marekani bilioni 3.8, na sarafu ya China (yuan) dola milioni 735.

Pia Soma

Dunia hii haina siri tena
 
Back
Top Bottom